Kama kampuni imesajiliwa tayari, kwa kawaida leseni ya biashara inapaswa kuombwa kwa taarifa za kampuni, siyo jina lako binafsi. Kwenye TAUSI, hakikisha umeingia/ume-link taarifa za kampuni husika na una nyaraka zake kama Certificate of Incorporation, TIN na taarifa za biashara.
Kama option ya kampuni haionekani, inaweza kuwa suala la profile/account au aina ya huduma unayoomba. Ni bora usiombe kwa jina lako binafsi halafu baadaye ujaribu kubadilisha.
Ushauri wangu: fika kwenye ofisi ya mamlaka inayotoa leseni eneo ambalo biashara ipo, waonyeshe Certificate of Incorporation na TIN ya kampuni, waombe wakuelekeze namna ya ku-link kampuni kwenye TAUSI. Ukishapata leseni kwa jina la kampuni, ndipo mambo ya akaunti ya benki ya kampuni yatakuwa straightforward zaidi.