Msaada kuhusu king'amuzi cha ting

zaratustra

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
848
223
Wakuu jana nilinunua king'amuzi cha TING, nimejaribu kuki-set lakini napata vizuri station moja tu: ATN, nyingine mbili tatu za nje ziko kwenye mnato tu. Kama kuna mwana JF anayetumia king'amuzi cha TING anisaidie!
 
acha kuchafua biashara za watu, kwani ulinunua kwetu, ulipokuwa unanunua si uliambiwa na namba za siku kupiga unapopata tatizo, mbona zinapatikana vizuri kabisa na hazina tatizo?kwako tu mzee?haukupewa maelekezo, unafikiri maelekezo uliyopewa yatakuwa tofauti ya yale utakayoambiwa na wengine, unachofanya si kizuri..acha kabisa.
 
username yako na maneno yako ni tofauti sana! Hata hivyo nashukuru kwa USHAURI wako nitaufanyia kazi. pia nisamehe sitarudia tena mpendwa Mungu akubariki sana na akuwezeshe!
 
Mkuu mbona jibu lako hali fanani kabisa na signature yako? Mi nadhani hajakosea! Kuuliza si ujinga wala kuchafua biashara za watu! Mbona vifaa vingi sana huwa tunauliza humu esp katika Jukwa la Science and Tech, na waungwana wanatujibu na kutusaidia ingawa namba za simu, na email even websites za watengenezaji zipo? Jamani mwenye jibu amsaidie huyu mwenye king'amuzi cha Ting!
 
username yako na maneno yako ni tofauti sana! Hata hivyo nashukuru kwa USHAURI wako nitaufanyia kazi. pia nisamehe sitarudia tena mpendwa Mungu akubariki sana na akuwezeshe!

Mkuu, ujue katika karibu kila jambo utapambana na negative talkers! Usamehewe kwa lipi? Hutarudia kwani umekosa nini? Nadhani hujakosea kwa hiyo rudia tena na tena kuuliza na wapo watu wazuri sana sana humu katika JF watakusaidia!
 
Mkuu Soki, nilitaka kumuonyesha tu kuwa mimi ni muungwana. Nimeomba anisamehe na pia sitorudia tena, maana aliniambia: ........"acha kabisa"
 
jamani hili jukwaa la kuelimishana sio kubwatikiana k2 ujui potezea sio kuwajb wenzio ovyo mpaka ameomba nikwamba amejaribu unayowaza ww yameshindikana tujifunze kuheshimu mawazo ya wengine
 
kaka sasa hivi hao jamaa wa ting wanafunga software mpya wanataka kuingiza channel mpya 42 nakumbuka niliponunua ile dec walisema na ESPN itakuwepo sasa tusubiri, ila sasa hivi kamanda nakula bata mno maana uki search unapata tv za Kenya Uganda za uarabuni kibao za movie Dubai sports one na two hawa wanaonesha bundesliga Live so nilifaidi sana weekend hii Borrusia dortmund na Bayern Munich, unapata TBC CNN BBC moja kwa moja ila wakishafunga software hiyo mpyaa huo uroda waote utakwisha watarudi kwenye hali yao ya kawaida na malipo yatakuwa elfu kumi na tano kwa mwezi. ku search ni rahisi sana Nenda Menu halafu kuna ki window kiutatokea hapo select option ya mwisho kabisa ina kialama kama cha dish hivi, pale itakupa kibox cha kuingiza password yako uliyopewa ukiingiza window itafunguka tafuta auto search halafu kwenye Channels selec all chini yake select search itakupa channles kibao mkuu jaribu uone.
 
acha kuchafua biashara za watu, kwani ulinunua kwetu, ulipokuwa unanunua si uliambiwa na namba za siku kupiga unapopata tatizo, mbona zinapatikana vizuri kabisa na hazina tatizo?kwako tu mzee?haukupewa maelekezo, unafikiri maelekezo uliyopewa yatakuwa tofauti ya yale utakayoambiwa na wengine, unachofanya si kizuri..acha kabisa.

Kaka twampa YESU sifa yake kwa kuwa yeye ndo mwokozi wetu kwa damu yake katuokoa sisi lkn huyu jamaa hujamtendea haki kabisa, kauliza kiungwana saana tu anahitaji maelekezo kidogo, yeye kashindwa kuipata vizuri si vibaya jamani ndo maana ya JF mkuu plse
 
Wakuu jana nilinunua king'amuzi cha TING, nimejaribu kuki-set lakini napata vizuri station moja tu: ATN, nyingine mbili tatu za nje ziko kwenye mnato tu. Kama kuna mwana JF anayetumia king'amuzi cha TING anisaidie!
Ndg yangu! Bila shaka hata nao wameungana na baadhi ya vi2 feki toka China visivyo ktk viwango na hata hvy TBS wa hajaijali hilo. Nilikuwa na mpng wa kununua ila stk tn.
 
username yako na maneno yako ni tofauti sana! Hata hivyo nashukuru kwa USHAURI wako nitaufanyia kazi. pia nisamehe sitarudia tena mpendwa Mungu akubariki sana na akuwezeshe!
Nikweli mkuu! Maneno aliyoyatoa ni tofaiuti na Utumishi wa BWANA!.
 
I suggest you go kwa customer care na utapata maelezo ya kina kuhusiana na hicho king`amuzi caz I still do beliv upo na guarantee na bado terms na conditions za mkataba wako bado zinakulinda. But angalia pia settings zake na compare na neighbor yoyote ili kujua kama shida ni yako tu ama geog. location pia.
 
Mkuu Soki, nilitaka kumuonyesha tu kuwa mimi ni muungwana. Nimeomba anisamehe na pia sitorudia tena, maana aliniambia: ........"acha kabisa"

kweli Mkuu. Penye wengi kuna mengi! Hukutaka kujibizana naye ingawa ungeweza kumshinda kwa hoja. Huo ni mfano mzuri wa kuigwa!
 
Mkuu Soki, nilitaka kumuonyesha tu kuwa mimi ni muungwana. Nimeomba anisamehe na pia sitorudia tena, maana aliniambia: ........"acha kabisa"

Kama nilivyokwambia hapa katika JF kuna watu wazuri wengi tu! Ebu angalia jinsi watu walivyochangia hoja yako vizuri. Na usishangae kuona posts nyingine nzuri tu zikija ambapo hatimaye utakuwa umepata faida!
 
kaka sasa hivi hao jamaa wa ting wanafunga software mpya wanataka kuingiza channel mpya 42 nakumbuka niliponunua ile dec walisema na ESPN itakuwepo sasa tusubiri, ila sasa hivi kamanda nakula bata mno maana uki search unapata tv za Kenya Uganda za uarabuni kibao za movie Dubai sports one na two hawa wanaonesha bundesliga Live so nilifaidi sana weekend hii Borrusia dortmund na Bayern Munich, unapata TBC CNN BBC moja kwa moja ila wakishafunga software hiyo mpyaa huo uroda waote utakwisha watarudi kwenye hali yao ya kawaida na malipo yatakuwa elfu kumi na tano kwa mwezi
kaka niko interested na hiki king'amuzi cha ting kinapatikana wapi, bei gani
inafanya kazi kwenye madish ya kawaida

natanguliza shukrani
 
Wakuu nina muda mrefu nilikuwa sijaingia kwenye jukwaa hili, nashukuru wote walioniunga mkono na kunifariji kutokana majeraha ya mpendwa hapo juu! @Hinx6 hiki ni king'amuzi cha kampuni iitwayo TING kinasambazwa na ATN (Agape Television Network). Kinapatikana kule kanisani (Pastor Vernon Fernandes)Mbezi Jogoo, ingawa mimi nilielekezwa kununua barabara ya uhuru duka linaitwa RAIA BAZAAR (kama sijakosea).
 
Back
Top Bottom