Msaada kuhusu hii bili ya maji

Missandei

Member
Apr 21, 2023
58
87
Habari zenu.
Ni hivi nyumba ninayoishi ilikatiwa maji sababu mwenye nyumba hakwenda kulipa ingawa sisi tulimtumia bili yake kama kawaida.
Sasa maji yalivokatwa niliangalia deni kupitia application ya kwenye simu yangu, lilikuwa ni 40185.2 wakasema lilipwe kabla ya May 21. Basi sisi tukaachana nalo sababu halituusu tulishalipa ni uzembe wa mwenye nyumba. Baada wiki 2 mama mwenye nyumba akanitafuta kuhusu kurudisha maji mimi nikamwambia mwezi huu nimeshakubaliana na jirani kuchota maji kwake kwa mwezi huu mzima nitachangia bili huko kwaio sitaweza kulipa maji sehemu 2 labda kwa mwezi ujao. Basi akakasirika akasema atayarudisha kwa ajili ya wapangaji wake wengine mimi niendelee kuchota hukohuko siku zote basi ikapita. Lakini maji hapa hayajarudishwa hadi leo hii, nikasema niangalie kama deni limeshalipwa. Aisee nimekuta deni limeongezeka hadi 60340.7 na wanasema ni kwa ajili ya malipo ya bili mwezi wa 5, Na huku maji yamekatwa mwezi mzima huu hakuna aliyetumia sasa hii bili imetokana na nini wakuu?
 
Back
Top Bottom