Msaada kuhusu elimu na Vyeo Jeshini

Oohh shukrani sana mkuu
 
Jeshi Usu nakumbuka kama limeanza mwaka hu au mwaka jana mwishoni.
Mbona vwatu wamekomaa hivi au walichukua watu wa majeshi mengine au umri haukuzingatiwa
 
Yeye analipenda jeshi na amesema ataenda bila kujali vikwazo vya kule ila mimi ndo nimeona nimsaidie tu kuuliza

Kama anapenda basi hawezikuona shida yeyote, passion ndiyo kila kitu kwenye mafanikio ya maisha yetu ya kila siku.

Once you find out what your passion is. You will live the life that matters
 
Every soldier Think to be General.Sasa unataka kuwa askari huna nia ya kuwa kiongozi maana yake utakuwa private sugu na mkorofi usiyekuwa na tija jeshini. Utaratibu kwanza JKT apige jalamba la kufa MTU kisha JWTZ yaani hapo ukifika Unaanza tena A yaani kule JKT kama ulikuwa umetoka chumbani kwenda chooni tu hapo Sasa mziki wake kama kutembea kwa mguu kutoka Kagera kwenda Mtwara .Baada ya kuwa soilder kinachofuata kupiga malindo ya kufa MTU Yale ya hatari tupu si unajua ukianza kazi wanasema kuruta si MTU unafananishwa na Roboti ukishahenya hapo ndiyo upige peper la Officer cadate ukifaulu ndiyo upelekwe Monduli hapo maamaaaa utajuta kwanini uliamua kuwa askari maana haki za binadamu zinaishia getini hapo ni mwendo wa ubabe mapokezi tu mapushapu kama 300 kwa mpigo mmoja kisha karinyekarinye zingine zinaendelea yaani pale kuna ile mikamanda ya kimasai na kikurya elimu kubwa mwili nyumba anapiga ngumi noma halafu hanaga cha kuogopa na huna cha kumtisha .Apo mwendo wa mbwa mwanzo .Mpaka JPM akuvishe Nyota Si kazi ya mchezo mchezo ndiyo maana kwa wale wanawake hata kupata watoto inakuwaga shughuli kweli .Kwa ufupi jeshi si lelemama connection yake kwenye elimu ya chuo kikuu ipo kwenye kipindi cha ratiba za kazi za kawaida mfano We we daktari utakwenda hospitali,Mwanasheria mahakama za kijeshi na Military Police leader,Muhasibu mambo ya pesa ,Sasa kabla ya kukabidhiwa kwenye fani yako mziki wake inakubidi ufungue moyo maana Yale za mazoezi kwamba ukichoka unaacha Bali ni mafunzo hivyo hata ukichoka lazima umalize silabasi na lazima ufaulu. imba kidogo "MAJESHI SI LELEMAMA HAYAHITAJI KUBEMBELEZANA ' mara2
 
Mmhh mkuu sasa mbona nina ndugu yangu ana Diploma ila hivi sasa ninavyoandika ana nyota mbili na hajafikisha hata miaka minne jeshini

Halafu hivi mazoezi yote hayo wanafanya wote wanaume na wanawake au kuna mazoezi ambayo wanawake wanakuwa excluded?
Inategemea na fani yake ila kwa sasa huyo mdogo wako na bachelor degree yake aende uone degree zimekuwa kama mchele jeshini kwanza hazitakiwi zinafanyiwa figisu sana kwa sababu maalumu.
.
Mazoezi ni ya wote usiombe yakukute utakunywa maji sana
 
Unavyowasili mafunzo ya JKT, kama week la kwanza unakuwa Mzalendo, then unaanza ukuruta kufikia uservice man/girl.
Hahaha haya huwa ya kwa mujibu wa sheria naona uzalendo umewakaa sana wadogo zangu vipi zoezi la magobole unalikumbuka?
 
Hii comment ndio imeongea ukweli wa mambo.
Mimi nina rafiki yangu aliingia na vyeti vya form 6 ana miaka zaidi ya 10 kule na hadi Sasa hivi ni koplo.
Mambo siyo rahisi Kama watu wanavyorahisisha na kutengeneza formula.
 
Ndiyo ujue kwamba kule hakuna formula Kama watu wanavyofikiria.
 
Mkuu kwa awamu hii connection nazo zimegoma asee, kuna jamaa yngu yupo jkt anazo tena za wakubwa kabisa lkn naona hazi work out na sasa anajiandaa kurudi nyumbani [emoji23][emoji23][emoji23]
Connections bado zipo kila mahali ila inategemea huyo anayekupa connection ana nguvu kiasi gani,mwingine unaweza ukamuona mkubwa sana kumbe akienda makao hajulikani.
 
Kuna wenzake wana masters bado wanajitolea huko JKT mwaka wa 3 sasa.

Jeshini hamna mshahara kuna 'posho' tu.

Kabisa mkuu. Mimi kuna mwanangu amemaliza chuo mwaka 2015 tena ngazi ya shahada na ana GPA kali sana.

Tangu aende JKT ni mwaka wa 4 huu bado haja panda ngazi yoyote hadi ameshajikatia tamaa ana mpango wa kurudi kitaa aanze kufundisha tuitions au kuuza mitumba tu.
 
Siku hizi jeshi si lelemama hivyo ,hiyo degree yake si kitu tena kwa awamu hii ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…