Mmhh haya mambo yanachanganya sana yaani mtu ana masters ila bado anasota JKT miaka 3?
Mbona nina ndugu yangu mwingine ana diploma lakini hivi sasa ninavyoandika ana nyota mbili na hajafikisha hata miaka minne jeshini au labda jeshini ni connections tu?
Nadhani mambo yamebadirika saizi, nakupa hii ni experience kutoka kwa jamaa zangu nliomaliza nao form six 2015
Kabla yetu, yaani waliomaliza six mwaka 2014 walikua wakienda jkt kwa mujibu wakabakizwa jeshini walifanya course kwa muda wa miezi 9 Tu then wakapata nyota but kwa tuliomaliza 2015 mambo yalibadirika kidogo maana Mimi kuna jamaa zangu walibakizwa jeshini wakakaa kwanza kwa muda wa mwaka mzima bila kufanya chochote just wapo Tu kambini wanaamka, wanakula na kulala ili kupimwa uvumilivu.
Baada ya hapo mwaka uliofata 2016 walipelekwa course ya miezi mitatu, maana wao walikua wamepitia jkt after form6 so ile miezi mitatu waliyopekekwa course ilikua kukamilisha miezi sita ndipo wakapata bakabaka, wakafanya kazi mpaka 2018, ndipo wakapelekwa Monduli kwa ajili ya course ya uafisa (nyota), na course ya uafisa kwa sasa hivi ni kama mtu anaechukua degree, so kwa mtu alietoka six anasoma uafisa kwa muda wa miaka mitatu kama anaechukua bachelor, but kama ana degree tayari huyo basi anafanya course kwa muda wa miezi Tisa tuu
Zamani ilikua mtu mwenye bachelor anenda moja kwa moja kufanya course ya uafisa (nyota) kama akichaguliwa kujiunga na jeshi, but kwa sasa si hivo tena, mtu mwenye bachelor akichaguliwa anaenda kuanza course ya ucadet kwa muda wa miezi 6 (wanaita kumtoa uraia wa kawaida) baada ya hapo anapata bakabaka then anasubiri intake ya kwenda kusoma uafisa (nyota) kwa muda wa miezi Tisa ila inategemea na mambo mengi kama vile Afya, connection, nidhamu, so kwa sasa mtu kuishia ucadet (bakabaka) ingawa ana degree yake ni kitu cha kawaida Sana kama amekosa vitu nilivyovitaja hapo , hope nimesaidia kwa namna moja ama nyingine.
NB: ukimaliza course ya uafisa kama Umetokea form six au Una bachelor unapata nyota moja (ingawa hapa sina uhakika Sana kama nimekosea watanisahihisha wengine)