Kabisa Kabisa, sometimes hadi mwakaDuuh aise kwahiyo inaweza kuchukua hata miezi mtu kusubiri kutoka kwenye course moja kwenda nyingine?
Bachelor ndo usiseme, nina mwanang anamalizia mkata wake wa miaka miwili anarud zake home,, kila sku ni kumtukana magu,Kuna wenzake wana masters bado wanajitolea huko JKT mwaka wa 3 sasa.
Jeshini hamna mshahara kuna 'posho' tu.
as far as Connections zipogo maofisini, basi hakuna kitu cha kuaminika hapa
Sasa huyo si ni mmoja tu mkuu nimehitaji na majibu ya watu wengine maana inawezekana yeye huyo ndugu yangu alipata connection
Shukrani mkuu umesaidia sana.Nadhani mambo yamebadirika saizi, nakupa hii ni experience kutoka kwa jamaa zangu nliomaliza nao form six 2015
Kabla yetu, yaani waliomaliza six mwaka 2014 walikua wakienda jkt kwa mujibu wakabakizwa jeshini walifanya course kwa muda wa miezi 9 Tu then wakapata nyota but kwa tuliomaliza 2015 mambo yalibadirika kidogo maana Mimi kuna jamaa zangu walibakizwa jeshini wakakaa kwanza kwa muda wa mwaka mzima bila kufanya chochote just wapo Tu kambini wanaamka, wanakula na kulala ili kupimwa uvumilivu.
Baada ya hapo mwaka uliofata 2016 walipelekwa course ya miezi mitatu, maana wao walikua wamepitia jkt after form6 so ile miezi mitatu waliyopekekwa course ilikua kukamilisha miezi sita ndipo wakapata bakabaka, wakafanya kazi mpaka 2018, ndipo wakapelekwa Monduli kwa ajili ya course ya uafisa (nyota), na course ya uafisa kwa sasa hivi ni kama mtu anaechukua degree, so kwa mtu alietoka six anasoma uafisa kwa muda wa miaka mitatu kama anaechukua bachelor, but kama ana degree tayari huyo basi anafanya course kwa muda wa miezi Tisa tuu
Zamani ilikua mtu mwenye bachelor anenda moja kwa moja kufanya course ya uafisa (nyota) kama akichaguliwa kujiunga na jeshi, but kwa sasa si hivo tena, mtu mwenye bachelor akichaguliwa anaenda kuanza course ya ucadet kwa muda wa miezi 6 (wanaita kumtoa uraia wa kawaida) baada ya hapo anapata bakabaka then anasubiri intake ya kwenda kusoma uafisa (nyota) kwa muda wa miezi Tisa ila inategemea na mambo mengi kama vile Afya, connection, nidhamu, so kwa sasa mtu kuishia ucadet (bakabaka) ingawa ana degree yake ni kitu cha kawaida Sana kama amekosa vitu nilivyovitaja hapo , hope nimesaidia kwa namna moja ama nyingine.
NB: ukimaliza course ya uafisa kama Umetokea form six au Una bachelor unapata nyota moja (ingawa hapa sina uhakika Sana kama nimekosea watanisahihisha wengine)
Hapana mkuu yeye analipenda jeshi na ataenda jeshini bila kujali vikwazo vitakavyojitokeza ila mimi ndo nimeona nimsaidie tu kuulizaWw na dada yako mnawaza vyeo vikubwa kwa maslahi binafsi....nchi hii inahitaji kujinyima kwa ajili ya watu wote...kuwa mwanachi wa kawaida sio mbaya
Mkuu kwa awamu hii connection nazo zimegoma asee, kuna jamaa yngu yupo jkt anazo tena za wakubwa kabisa lkn naona hazi work out na sasa anajiandaa kurudi nyumbaniUtaratibu sasa hivi umebadilia
MOJA: Askari anayetakiwa awe na nyota kwa UMRI ni chini ya miaka 23 kushuka chini,kwa experience yangu Uncle angu mda huu anapiga hiyo course ya uafsa.
MBILI: Hata kama utakuwa na Masters ni lazima uanzie chini yani nyota moja lakini kabla ya hapo utaratibu ulikuwa mwenye degree mfano ya MD atachukua nyota tatu.
TATU: course ya Uafsa ni miezi 9 na sio chini ya hapo.
Nb: Kuna uncle wangu mkubwa ana elimu ya form six lakini hakupata cheo chochote ila alivaa UKOPLO kwa Sababu ya fani yake CLINICAL OFFICER.
Jeshini usipokuwa na refa utapiga mihayo Sana utashangaa wa darasa la saba anavaa bakabaka ila mwenye Degree ya Engendering anarudi nyumbani.



Hapana mkuu reference ya huyo mmoja haitoshi kwa sababu siwezi jua labda yeye alipata connection na hata hivyo mbona hakuna sehemu niliyompinga mtu kote nimeuliza ili kuondoa utataSasa hayo maswali si ungemuuliza huyo ndugu yako.??
Tatizo umei set akili yako kitu fulani alafu unakuja kuuliza ,unaambia ukweli unaukataa..
Jeshini sikuhizi ni kama enzi za nyerere uzalendo kwanza mbwembwe nyingine baadae..
Ataanza JKT, kisha atasota kwa muda fulani kupimwa uvumilivu, kisha atpewa bakabaka, kisha itamchukua muda si chini ya mwaka mmoja kuwa mwanajeshi wa kawaida, baada ya hapo atapelekwa kusoma u afisa(miezi 9), lakini hii yote inategemea connection pia so anaweza sota zaidi..
Mkuu yeye kasema analipenda jeshi na ataenda bila kujali vikwazo vitakavyojitokeza ila mimi ndo nimemsaidia kuuliza tuKama unawaza vyeo jeshini utapata tabu sana kwa nyakati hizi na degree yako bora ukalime nyanya ziwe resources viwandani huko. Jeshi linahitaji kwanza kuwa na self committment na kupenda sio vipaumbele vya vyeo na mishahara.
Sijui kafanya makusudi au hajui kama Mimi?Dah...we jamaa wewe!! Nungu huwa halali, unapata dhambi!!
Kazi kweli kweli, haya nitaenda na mimi ili nikaipate hiyo 'haki sawa' unayoisemea.Jeshini kunakufaa sana Marianah, huko utakutana na haki sawa ila usiende kwa ajili ya vyeo na mishahara. Jeshi linataka kujitoa na uzalendo kwanza, vyeo na mishahara ni baadae sana.
Kuna fani hapa duniani inabidi uzipende kutoka moyoni, otherwise unaingia then unaanza kujuta. Mimi sina uzoefu na ujeda, nadhani umepata maoni mengi, kila la heri.