dada dori.. hyo biashara ya mchele unataka kuuzia hapo hapo moro au nje ya moro.changamoto zake ni mchele wa teja wanataka uwe super kulingana na soko lilivyo na upatikanaji wake. bei nzur sana ya mchele nikuanzia mwez wa 8-3 kwa huku mbeya lakn coz mwz wa nne mchele mpya uwa unaingia kwa huku mbeya lakn sijuh mikoa mingne..
unatakiwa uwe na mpunga mrefu unanunua mwingi wakati wa mavuno kati ya mwenzi wa 6,7,8 then unauza kipolepole mwingi unauifadhi unakuja kuuza bei nzuri kipindi cha mavuno yameisha
nilipokuwa nipo RUKWA na viunga vyake ndo ilikuwa bznes yngu ilinitoa sana edhi ya miaka 2005 mpk 2008
Mambo ya msingi ya kijiuliza mchele unaupata wapi? kwa bei gani gharama zako (usafiri, malazi, pango, kukoboa, packaging etc) zikoje? Ni aina gani inapenda kwenye soko lako (firedume, shingo ya mwali, katrin 05, etc)? Gharama za manunuzi ukijumlisha na ghara zingine je bei ya kuuzia inakupa faida?
Suala la kuweka stock ni tofauti kidogo maana we mtaji wako ukizunguka ndio unapata faida nyingi wakati speculators wananunua na kuhifadhi bei ikipanda ndio wanauza.
Asante KICHAKORO.Mm kwa upande wangu nimeona wateja wangu wakubwa watakuwa ni mama ntilie ambao wanatumia mchele kupikia wali kila siku.Plan yangu ni kuwa niwe nawasambazia kwenye maeneo yao!Kwa kuwa ndio naanza,nitaanza kununua mchele kidogo ili niangalie hali ilivyo!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.