Msaada kufungua duka la nafaka Jumla na Reja reja

BABU KIDUDE

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,588
904
Habari
Mimi si muandishi sana humu lakini ni msomaji mmbobezi, muajiliwa toka 2008.
Katika maisha yangu sijawai kufanya Biashara yoyote au shughuli yoyote ya kuniingizia kipato zaidi ya Mikopo bank na Ujira wa mwisho wa mwezi.
Hivi Karibu nimapata wazo la kufanya Biashara au kilimo. kama kichwa kinavyosema naombeni mwenye ujuzi wa kuanzisha Biashara ya Nafaka kwa Jumla na reja reja,. Hivi Karibu Natarajia kupata kiasi flani cha kuanzia Kwani Kuna vikoba vya wife turijiweke akiba huko kanisani tutavunja .
Mwenye ujuzi kwenye point zifuatazo
1. Upatikanaiji wa nafaka
2. Vibari husika,
3.Upatikanji wa Faida na Hasara zake
4.Kiasi cha mtaji cha kuanzia
5. Hiana za nafaka Zenye Faida

Kumbuka haswaa malengo yangu Mchele, Maragwe, Soya, Mtama, Mbaazi, Kunde, Mahindi,Choroko nk...
 
Kwanza hongera kwa kuwa na wazo zuri zalishi. Ila ningependa kukuomba haya mambo mawili:-

1: Tuambie mahali (mkoa), unapotaka kuifanyia hiyo biashara.
2: Tueleze pia, ni kiasi gani cha pesa, unachotegemea kukipata....

Note:
Nimekuomba utueleze hivyo vitu viwili kwanza, kwasababu ni vitu muhimu vya kuzingatia, katika uanzishaji wa biashara hiyo.....if ukiwa honest kwenye hayo, utakuwa umetoa room nzuri ya kupewa ushauri mzuri. So ni vema ukawa muelewa chief....
 
Biashara ya nafaka inalipa sana ila inategemeana na vitu vifuatavyo
1. Location ( ukifanyia mjini hapa umewin)
2. Aina ya nafaka(napendekeza fanya mahindi mwaka huu bei inapanda kwa speed ya light.

3. Capital ( hapa ndio kila kitu) kama ndio unaanza biashara usikope pesa anza biashara kwa pesa yako kwanza ukipata wateja basi waweza kopa kuimarisha biashara.
 
Nunua mchele kutoka mbeya na mpanda ule wa kamsamba. Usichanganye mchele wa kutoka mikoa mingine ili u win soko la mchele safi yaani ule grade 1. Nunua mahindi kutoka mbeya na ruvuma na kwingineko kusanya yakutosha weka stoo bei ikiwa nzuri uza. Biashara ya nafaka au chakula ni biashara inayolipa sana na haina hasara maana ni bidhaa inayohitajika na walaji ni wengi. Cha kuzingatia tu ni bei elekezi ya soko na bei ya kununulia shambani au kwa wakulima.
Karibu sokoni tuuze nafakaaaaa...
 
Kwanza hongera kwa kuwa na wazo zuri zalishi. Ila ningependa kukuomba haya mambo mawili:-

1: Tuambie mahali (mkoa), unapotaka kuifanyia hiyo biashara.
2: Tueleze pia, ni kiasi gani cha pesa, unachotegemea kukipata....

Note:
Nimekuomba utueleze hivyo vitu viwili kwanza, kwasababu ni vitu muhimu vya kuzingatia, katika uanzishaji wa biashara hiyo.....if ukiwa honest kwenye hayo, utakuwa umetoa room nzuri ya kupewa ushauri mzuri. So ni vema ukawa muelewa chief....
Kwanza Shukrani kwa muda wako na Kujali pia

1.Nipo Dar na natarajia kufungua Mbezi Mwisho to Manzese haya ni meaneo ninayotembelea sana kwenye shuguli zangu za kila
2.Natarijia kuanza na 5m kila kitu
 
Kwanza Shukrani kwa muda wako na Kujali pia

1.Nipo Dar na natarajia kufungua Mbezi Mwisho to Manzese haya ni meaneo ninayotembelea sana kwenye shuguli zangu za kila
2.Natarijia kuanza na 5m kila kitu
Umefanya jambo la busara, kuonyesha ushirikiano wako kwa kile nilichokuomba.

Kwa kufanya hivyo nami naona sina budi, kukupa ushirikiano wangu wa kukueleza kile ninachokifahamu, juu ya biashara unayotaka kuifanya. Ila kwa sasa nipo busy kidogo, hivyo tafadhali naomba nivumilie kidogo, nikitulia tu nitakurudia....
 
Bado nafatiliaa uzii huu nione mwisho wake mnk na mim Niko mbioni kufunguaa duka LA nafaka uzusan ddm au singidaa
 
Kwa mtaji wako usianze na vibali vikubwa chukua kitambulisho cha mjasiliamali kwanza
1.Nunua mchele gunia kama kumi maana kwa sasa unaelekea kupanda bei
2.Nunua unga wa sembe viroba vya kg25 kama vitano kwa kuanzia na dona moja(ukipata sembe ya iringa itakuwa vema zaidi)
3.Nunua maharage ya Soya(kijivu)kg 50
4.maharage njano kg 50
5.maharage kombati kg 50
Hakikisha unayang'ata kidogo kujua ubora wake na yawe masafi ukipata yale ya bei ya 2000 ni bora zaidi maana yanavutia wateja
6.kunde kg 30
7.njugu kg 30
8.karanga 30
9.soya lishe30
10.mtama
11.na vingine wataongezea wengine
12 .mafuta ya kula dumu moja
13.sukari kg 50
14.chumvi kubwa
15.ngano bora ya azam kg 25
16.sembe kg 5.
17.unga wa lishe bora
Upatikanaji wa bidhaa ni kwamba unaenda kwenye maduka ya jumla ya bidhaa hizo fanya utafiti kwa wafanyabiashara wa maeneo hayo ya mbezi hadi manzese wananunua wapi bidhaa zao na ujiridhishe kwa maduka angalau mawili au matatu ulinganifu wa bei kisha anza kufanya manunuzi na usianze kununua vingi kama nilivyoanisha anza kidogo kidogo sana mfano sukari unaweza kuchukua hata 25 kg
 
Kuhusu faida unapiga tu kama kawaida kwa mfano ukichukua sukari kg 50 ni shilingi 105000 kg1 unauza 2500 hpo utaona faida ni shingapi.
Gunia za mchele unachanganya ili kuwapata wateja wote mfano unaanza na gunia za 1200 ambayo we utauza labda 1500 kisha unachukua ya 1400 we unauza 1600 kisha unachuka za 1700 we unauza 2000 zote hizi ni kg 100 unakuwa na super kabisa unakuwa na wakati na wakawaida kisha unapiga mahesabu ya faida na bidhaa zote unapiga bei namna hiyo
 
Mengine soko litakwambia pamoja na uzoefu biashara ni kitu kizuri jitahidi upange bei vizuri na ukienda sokoni jitahidi kuchukua kitu bora zaidi kuliko vitu vingine mteja akija dukani jitahidi umfafanulie kuhusu bidhaa unayomuuzia kama atahitaji ufafanuzi
Usitukane mteja aliyekuudhi mbele yake au baada ya kumuhudumia na akaondoka waheshimu maana wamevuka maduka mengi hadi kufika kwako
Ukikoseana na mteja leo kesho akija usiache kumuuzia chukua hela yake maana ndio unayotafuta.
 
Hii ndio biashara nzuri kwa kipindi hiki...michango ya wadau ni mizuri ila mngetujulisha na changamoto.
 
Good experience.

Changamoto kubwa ni usimamizi kama unafanya mwenyewe ni vizuri zaidi kama unamuweka mtu ni vizuri akawa mtu unayemuamini sana na awe angalau kijana wa miaka 15 hadi 22 baada ya hapo unastafisha maana atakuwa ameingia kwenye rika la matumizi holela
Waza sana kuhusu usimamizi ni jambo la msingi mno maana hii ni biashara ya uaminifu muuzaji hawezi kuandika kila anachouza
Ununuzi wa vitu uendane na aina ya wateja wa eneo husika usije kuweka sehemu vitu kama Nido Lactogen Murzah na labda blue band ya kg 1 na vitu vingeni vya kifahari kama unakaa uswahilini na kwa sasa middle income wamepungua sana sio kama 2015 kurudi chini
Hii ndio biashara nzuri kwa kipindi hiki...michango ya wadau ni mizuri ila mngetujulisha na changamoto.
 
Usipende kukopesha na unapokataa kumkopesha mtu wala usikasirike tumia tu plastic smile huku ukimpa sababu za kawaida tu mfano kwa sasa biashara sio nzuri sana au labda ni mapema sana unahitaji kuwa mzoefu n.k
Mikopo inaangusha sana biashara
Usishindane na uliowakuta zaidi jifunze kutoka kwao kwa uwazi au kwa siri jinsi wanavyovutia wateja na kufanya biashara zao
 
SHUK
Kwa mtaji wako usianze na vibali vikubwa chukua kitambulisho cha mjasiliamali kwanza
1.Nunua mchele gunia kama kumi maana kwa sasa unaelekea kupanda bei
2.Nunua unga wa sembe viroba vya kg25 kama vitano kwa kuanzia na dona moja(ukipata sembe ya iringa itakuwa vema zaidi)
3.Nunua maharage ya Soya(kijivu)kg 50
4.maharage njano kg 50
5.maharage kombati kg 50
Hakikisha unayang'ata kidogo kujua ubora wake na yawe masafi ukipata yale ya bei ya 2000 ni bora zaidi maana yanavutia wateja
6.kunde kg 30
7.njugu kg 30
8.karanga 30
9.soya lishe30
10.mtama
11.na vingine wataongezea wengine
12 .mafuta ya kula dumu moja
13.sukari kg 50
14.chumvi kubwa
15.ngano bora ya azam kg 25
16.sembe kg 5.
17.unga wa lishe bora
Upatikanaji wa bidhaa ni kwamba unaenda kwenye maduka ya jumla ya bidhaa hizo fanya utafiti kwa wafanyabiashara wa maeneo hayo ya mbezi hadi manzese wananunua wapi bidhaa zao na ujiridhishe kwa maduka angalau mawili au matatu ulinganifu wa bei kisha anza kufanya manunuzi na usianze kununua vingi kama nilivyoanisha anza kidogo kidogo sana mfano sukari unaweza kuchukua hata 25 kg
Shukrani sana hope nitakupa mrejesho wa kila hatua
 
Soko lako likikua utafurahi pale unapo anza kuongeza wigo wa biashara na kupeleka bidhaa nje ya nchi hasa UK kuna uhaba sana wa unga wa sembe nk mo dewj anapeleka lakini bado demand is higher than supply
 
Back
Top Bottom