Msaada kufika Uhamiaji Kurasini kutokea Tegeta

Rihana

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
498
250
Wakuu habari zenu.

Naomba msaada nakusudia kwenda Uhamiaji Kurasini kwa usafiri wa umma ila sijui nipande basi gani natokea Tegeta Nyuki.

Nitashukuru kwa maelekezo ni mimi dada yenu Rihana!
 
Nadhani hapo utapanda ya Tegeta hadi Kariakoo kisha ukifika kariakoo utapanda ya Mbagala/ Temeke kupitia Kilwa Road unamwambia Konda akushushie kituo ambachounaweza enda ofisi hizo
 
Panda gari uende mpj gerezani pale utapata yaendayo mbagala ushukie jitegemee km sikosei ndio kituo kilicho karibu
 
mwendokasi. shuka mwisho gerezani. ukiwa humohumo gerezani uliza zilipo gari za temeke kilwa road. shuka jkt ya kwanza. uliza masela wa bodaboda hapo wakupeleke buku tu naamini wakati wa kurudi utajiongeza hutakubali kutoa buku yako tena.
 
Wakuu habari zenu.

Naomba msaada nakusudia kwenda Uhamiaji Kurasini kwa usafiri wa umma ila sijui nipande basi gani natokea Tegeta Nyuki.

Nitashukuru kwa maelekezo ni mimi dada yenu Rihana!

nikuulize magari ya tegete huwa yanaishia wapi? makumbusho? mawasiliano? posta ?

Ukipata gari lolote la mbagala kupitia kilwa Road....shuka uhamiaji. ....utaona jengo lao na kibao chao.

Magari ya mbagala utayapata posta mpya, feri-kigamboni, kariakoo-gerezani na makumbusho.
 
Tegeta kuna mwendokasi?
 
ita UBER!

AU PANDA GARI ZA KKOO, THEN KKOO UPANDE GARI ZA MBAGALA ZINAZOPITIA KILWA ROAD, UNASHUKIA JKT
 
nikuulize magari ya tegete huwa yanaishia wapi? makumbusho? mawasiliano? posta ?

Ukipata gari lolote la mbagala kupitia kilwa Road....shuka uhamiaji. ....utaona jengo lao na kibao chao.

Magari ya mbagala utayapata posta mpya, feri-kigamboni, kariakoo-gerezani na makumbusho.
Mbagala hafiki posta wala ferry yanaishia gerezani
 
Tegeta kuna mwendokasi?
ukitokea tegeta kupanda au kutokupanda mwendokasi hapo kati (mwenge, ubungo, magomeni) ni uamuzi wako.

ila advantage ya mwendokasi la gerezani hautoki hata tone moja la jasho kuyafikia mabasi ya temeke kilwa road.
 
Wakuu habari zenu.

Naomba msaada nakusudia kwenda Uhamiaji Kurasini kwa usafiri wa umma ila sijui nipande basi gani natokea Tegeta Nyuki.

Nitashukuru kwa maelekezo ni mimi dada yenu Rihana!

Panda ndege za nchini (BODA BODA) mwambie unaenda kurasini.Funga macho ukifumbua utakuwa umeshafika kurasini.Hizo ndege hazioni mataa wala trafiki ikanza safari haisimami popote
 
nikuulize magari ya tegete huwa yanaishia wapi? makumbusho? mawasiliano? posta ?

Ukipata gari lolote la mbagala kupitia kilwa Road....shuka uhamiaji. ....utaona jengo lao na kibao chao.

Magari ya mbagala utayapata posta mpya, feri-kigamboni, kariakoo-gerezani na makumbusho.
shukrani sana mkuu nimekupata
 
Acha
Panda ndege za nchini (BODA BODA) mwambie unaenda kurasini.Funga macho ukifumbua utakuwa umeshafika kurasini.Hizo ndege hazioni mataa wala trafiki ikanza safari haisimami popote
acha dharau ndugu!
 
Panda gari za kariakoo, ukishuka kkoo nenda gerezani panda gari za Temeke zinazopita kilwa road, mwambie kondakta unashukia JKT ya kwanza. Ukifika hapo JKT muulize yeyote yule atakuonesha, usipande bida boda, ni nyuma tu ya huu mtaa wa mbele hapa mdada
 
Panda gari hadi kariakoo,panda la kwenda mtoni au Mbagala maeneo ya jitegemee jkt shuka,ulizia hapo.
 
Wakuu habari zenu.

Naomba msaada nakusudia kwenda Uhamiaji Kurasini kwa usafiri wa umma ila sijui nipande basi gani natokea Tegeta Nyuki.

Nitashukuru kwa maelekezo ni mimi dada yenu Rihana!
Panda gari Mpaka Kariakoo.

Kisha panda magari yanaoenda Temeke, shukia JKT ya pili karibu kabisa na Chuo cha Diplomasia au kituo cha Wokovu kisha waombe watu wakuonyeshe UHAMIAJI HOUSE. Siyo mbali kabisa. Unaeda na miguu hakuna haja ya kulipa Bodaboda
 
Panda gari za kawe ukishuka kawe panda za mbagala afu unaenda shukia uhasibu ukifika uhasibu uliza jengo LA uhamiaji
 
Back
Top Bottom