MSAADA: Kucha kuota kwa kuchimba nyama ya kidole

kiface

Senior Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
151
Reaction score
61
Habari wana jf, nimekuwa na tatizo linalonisumbua takribani miaka minne sasa, kucha zangu za vidole vya miguu zinaota kwa kuchimba nyama kitu ambacho wakati mwinginw hunisababishia maumivu makali sana hata kuvaa viatu siwezi,na nikijaribu kukata huwa kinabakia kama kidonda nilichokatwa na wembe, naomba msaada wenu tatizo hili husababishwa na nini, na tiba yake ni nini. Asanteni.
 
Japo hujafafanua nahisi kucha zako zimepinda ndio maana zinakua kuelekea kwenye nyama. Sababu bila shaka ni viatu ikimaanisha unavaa viatu ambavyo vinabana. Katika hali ya kawaida kucha hazikui kuelekea nyama lazima ziwe zimelazimishwa na kitu fulani na hasa viatu. Unaponunua kiatu hata kama umekipenda vipi kama kinakubana hata kidogo kiache tu. Achana ns lugha za wauzaji za "chukua kutapanuka baadaye" Ukichukua ni kweli baada ya muda unaweza kuhisi kiko sawa kabisa lakini kikaathiri umbo la kucha. Kwa hiyo kama ni viatu jaribu kutafuta ambavyo havikubani wala kupwaya sana. Tatizo litaisha tu. Uwe mwangalifu zaidi unaponunua viatu vilivyochongoka mbele. Kinaweza kutosha mguu kwa ujumla lakini maeneo ya vidole kinabana kidogo usiridhike chagua kingine.
 
mkuu hiyo mimi ilinisumbua sana ila kwa sasa niko poa kama unavaa viatu vya kubana acha kabisa jaribu kuvaa viatu ambavyo ni oversize kidogo zitaacha ukiona bado zinaendelea hapo itabidi ikatwe kucha na hiyo nyama inayochimbwa mimi nilifanyiwa hivyo 1995 mpaka leo niko poa ila navaa viatu oversize kidogo.
 
nashukuru sana kwa ushauri wako,ila toka limeanza hili tatizo sijavaa viatu vya kufunga vidole,nadhani suluhu ni kutoa kucha kama ulivyonishauri. Asante.
 
Japo hujafafanua nahisi kucha zako zimepinda ndio maana zinakua kuelekea kwenye nyama. Sababu bila shaka ni viatu ikimaanisha unavaa viatu ambavyo vinabana. Katika hali ya kawaida kucha hazikui kuelekea nyama lazima ziwe zimelazimishwa na kitu fulani na hasa viatu. Unaponunua kiatu hata kama umekipenda vipi kama kinakubana hata kidogo kiache tu. Achana ns lugha za wauzaji za "chukua kutapanuka baadaye" Ukichukua ni kweli baada ya muda unaweza kuhisi kiko sawa kabisa lakini kikaathiri umbo la kucha. Kwa hiyo kama ni viatu jaribu kutafuta ambavyo havikubani wala kupwaya sana. Tatizo litaisha tu. Uwe mwangalifu zaidi unaponunua viatu vilivyochongoka mbele. Kinaweza kutosha mguu kwa ujumla lakini maeneo ya vidole kinabana kidogo usiridhike chagua kingine.

asante kwa ushauri
 
Back
Top Bottom