Msaada Ku-unlock WiFi Router ya Tigo Huawei B315s-22

utakuja

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
989
797
Habari wakuu, ninahitaji direction kidogo kwa Dar es salaam; ni wapi naweza pata huduma ya kuaminika (fundi) ya kufungua router tajwa kutoka kampuni ya Tigo, ili niweze kuitumia na line nyingine.

images - 2021-04-13T003807.273.jpeg

Hii ni kutokana na Tigo kubadilisha vifurushi vyao vya Home Internet nilivyozoea, na kuweka vifurushi vya kipumbavu (Kwa upande wangu binafsi).

Kabla, kwa sababu za kihistoria, vifurushi vilikua kama ifuatavyo:

Wiki

Standard 12 GB - 15,000

Standard+ 40 GB (20GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 20 GB kutumia wakati wowote) - 25,000

Premium 60 GB (30GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 30 GB kutumia wakati wowote) - 35,000

Mwezi

Standard 60 GB (30GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 30 GB kutumia wakati wowote) - 50,000

Standard+ 100 GB (50GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 50 GB kutumia wakati wowote) - 85,000

Premium 200 GB (100GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 100 GB kutumia wakati wowote) - 120, 000

(screenshot zimeambatanishwa)

Mbaya zaidi hata walivyovibadilisha hawajatoa taarifa, na ndani ya app ya Tigo Pesa mabadiliko haya bado hayaja-reflect. Hivyo, ukinunua kifurushi kimoja wanakupa kifurushi tofauti na ulivyotegemea.

Vifurushi vyao sasa:

Regular 6.5 GB - 15,000
Standard 14 GB - 30,000
Standard+ 30 GB - 50,000
Premium 70 GB - 100,000

(screenshot imeambatanishwa)

Hitimisho, nitashukuru sana msaada wenu wa wapi niende Jijini Dar es Salaam. Pia isingekuwa mbaya na kuweka bei ya huduma hiyo, ili nikirudi Jijini hatua zangu za kwanza ni kufika huko moja kwa moja. Ahsanteni.

IMG_20210413_002722.jpg

IMG_20210413_002737.jpg

IMG_20210413_002748.jpg

IMG_20210413_002757.jpg

IMG_20210413_002806.jpg

IMG_20210413_002816.jpg

Screenshot_20210413-002950.png
 
Upande wangu sijawahi kukutana na hiyo kazi, ngoja tuwaasubiri waliowahi kukutana na hiyo.
Shukrani mkuu nimekuwa naangalia Youtube tutorial na kuna vitu nimejikuta na vikosa, kuweza kui-unlock.
 
Habari wakuu, ninahitaji direction kidogo kwa Dar es salaam; ni wapi naweza pata huduma ya kuaminika (fundi) ya kufungua router tajwa kutoka kampuni ya Tigo, ili niweze kuitumia na line nyingine.

Hii ni kutokana na Tigo kubadilisha vifurushi vyao vya Home Internet nilivyozoea, na kuweka vifurushi vya kipumbavu (Kwa upande wangu binafsi).

Kabla, kwa sababu za kihistoria, vifurushi vilikua kama ifuatavyo:

Wiki

Standard 12 GB - 15,000

Standard+ 40 GB (20GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 20 GB kutumia wakati wowote) - 25,000

Premium 60 GB (30GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 30 GB kutumia wakati wowote) - 35,000

Mwezi

Standard 60 GB (30GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 30 GB kutumia wakati wowote) - 50,000

Standard+ 100 GB (50GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 50 GB kutumia wakati wowote) - 85,000

Premium 200 GB (100GB kuanzia saa 6 usiku hadi 11:59 alfajiri na 100 GB kutumia wakati wowote) - 120, 000

(screenshot zimeambatanishwa)

Mbaya zaidi hata walivyovibadilisha hawajatoa taarifa, na ndani ya app ya Tigo Pesa mabadiliko haya bado hayaja-reflect. Hivyo, ukinunua kifurushi kimoja wanakupa kifurushi tofauti na ulivyotegemea.

Vifurushi vyao sasa:

Regular 6.5 GB - 15,000
Standard 14 GB - 30,000
Standard+ 30 GB - 50,000
Premium 70 GB - 100,000

(screenshot imeambatanishwa)

Hitimisho, nitashukuru sana msaada wenu wa wapi niende Jijini Dar es Salaam. Pia isingekuwa mbaya na kuweka bei ya huduma hiyo, ili nikirudi Jijini hatua zangu za kwanza ni kufika huko moja kwa moja. Ahsanteni.

Nimesha unlock moja ya smile model sawa na hii kwa firmware upgrade na AT commands.
 
Nimesha unlock moja ya smile model sawa na hii kwa firmware upgrade na AT commands.
Kweli, mkuu! Inawezekana Ku-unlock bila kuifungua na kufanya shoti? Maana kila tutorial niliyopita inatumia njia hiyo?
 
Ahsanteni sana wakuu. Nilijitoa muhanga na kwenda kwenye Website yangu pendwa ya Warusi na nikapata tutorial na vitendea kazi (pamoja na za Youtube) nzuri ya kuunlock: https://4pda.ru/forum/index.php?showtopic=700481 hii modem, nimeifungua na kuchukua tweezers ili ku'bootshot' -kitu nilichokuwa naogopa hapo mwanzoni (ilinilitea shida kidogo; Com ports zilikuwa hazitokei ili niweze kuflash custom firmware) but nilivyopiga partition ya pili ya Windows 7 kwenye laptop (warusi kule wanasema windows 10 ina some issues kwenye haya maswala) tofauti, kila kitu kikaenda sawa.

Anyway, haya maswala ya rooting, cracking, unlocking, custom roming niliyaachaga zamani kidogo, but nipo proud kuwa bado kuna kitu kimebaki
.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom