Msaada kisheria

Kalevra

Member
Aug 1, 2016
6
0
Habari za asubuhi ndugu,

Naomba msaada wa kisheria juu ya jambo lililonisibu katika ajira nliokuanayo katika kampuni moja hapa Tanzania. Nimefanya kazi kwa miezi 7 katika kampuni moja na baada ya kumaliza miezi 7 kampuni ilisema imebadili muundo wa kazi (business model) na kuwapa wafanyakazi wote option ya kuendelea au kuacha kazi (retrenchment process).

Basi wengi wetu tuliacha kazi nakufanya clearance process kama kawaida ya utaratibu wa kampuni. Basi makubaliano yetu na kampuni ilikua kulipwa hela zetu (Terminal benefits) kufikia tar 15/7 ila hayo malipo yalianza kuzungushwa mpaka mnamo tareh 21/7 nikapokea barua kua malipo yangu (Terminal Benefits) zimezuiwa kwa sababu kuna upotevu wa vitu ofisini na kwa hiyo sitolipwa mpaka uchunguzi uishe.

Nlifunga safari na kwenda eneo langu nililokua nafanyia kazi ili kujua shida na nini, na pia kwenda police kujua hyo kesi na RB ilikua kwa mpelelezi yupi. Kilichotokea nilikuta hapakua na kesi ila RB ilikua ni taarifa tu ilionyesha upotevu wa vitu ofisini na haikua inanishutumu mie as a suspect.

Na pia RB hii ilionyesha upotevu umetokea mwezi wa 6 na kipindi ambacho sikuepo kikazi mpaka kufikia leo hii malipo yangu hayajatoka na nimedhalilishwa na kushutumiwa kwa kesi ambayo sijafanya.

Naomba msaada na wenu wa kimawazo na ushauri juu ya hili ili kampuni hii itoe malipo yangu na fidia ya gharama ninazoendelea kuingia juu ya hili.
 
Hebu open up kidogo, taja jina la kampuni na mkurugenzi mwendeshaji na kituo chako cha kazi!
 
Ww uko mkoa gani ninajamaa yangu yupo Tuico ndio mtaalamu Wa haya mambo..
Kama vipi nikuunganishe naye
 
Hiyo kampuni ina tabia kama mifuko ya hifadhi ya jamii nayo imepitisha sheria za dhuluma kwa watumishi
 
Pole sana Mkuu. Je ulibaki na clearance form ambayo ilisainiwa na kugongwa Mhuri na line Meneja wako? Ikithibitisha kuwa hakuna kitu unachodaiwa?

Unawadai shilingi ngapi hiyo kampuni?

Uchunguzi kuhusu huo upotevu wa vifaa unaisha lini?

Pia, umedhalilishwa kivipi Mkuu? Kama kweli kuna upotevu na wanafanya uchunguzi sioni sababu ya kusema eti umedhalilishwa mkuu maana kama kuna upotevu ulifanyika na hata kama hauja Fanya wewe huo upotevu kampuni ina haki ya kwenda kutoa taarifa police.
 
Pole sana Mkuu. Je ulibaki na clearance form ambayo ilisainiwa na kugongwa Mhuri na line Meneja wako? Ikithibitisha kuwa hakuna kitu unachodaiwa?

Unawadai shilingi ngapi hiyo kampuni?

Uchunguzi kuhusu huo upotevu wa vifaa unaisha lini?

Pia, umedhalilishwa kivipi Mkuu? Kama kweli kuna upotevu na wanafanya uchunguzi sioni sababu ya kusema eti umedhalilishwa mkuu maana kama kuna upotevu ulifanyika na hata kama hauja Fanya wewe huo upotevu kampuni ina haki ya kwenda kutoa taarifa police.
clearance nnazo, na kituo cha police wamekanusha kuhusu hilo suala la upelelez kwa sabab hakuna kesi iliofunguliwa!

Nakubaliana nawe kua kampuni ina haki ya kupeleka taarifa police pale upotevu unapotokea lakin, hii taarifa haiko sawa kwani mie nlikua likizo kipindi wanachosema vitu vimepotea na pia mie sikua msimamiz wa vitu vya office!
Office ina walinzi na pia ina Office Coordinator anaehusika na office!
Kwa ufupi mkuu yote haya yametokea baada ya mimi kuanza kufuatilia madai yangu. Na sheria haimruhusu mwajili kuzuia malipo yangu baada ya kuacha kazi. Ndio maana nikasema nimedhalilishwa kwa sabab nimeshutumiwa kwa vitu vidogo vya office kama vyombo n. k!
Nadai zaid ya mil 5!
 
Back
Top Bottom