Msaada kisheria: Mpangaji amekaa miezi 6 bila kupila kodi

Mt Paulo

Member
Oct 27, 2018
73
46
Habari zenu wananchi,

Tuna mpangaji ana mwezi wa sita hajalipa kodi na ni mwalimu anafundisha shule za Serikali, tumeazimia kumuamisha na tunataka kupata stahiki yetu tunafanyaje?

Naombeni msaada
 
Mpaka anadaiwa miezi yote nyinyi mlikuwa mmekufa?
Je, mna mkataba wowote kati yenu na yeye?
Kama mnao unasemaje?

Hata kama mna mkataba, naamini kabisa huo mkataba unaeleza ni namna gani mpangaji anapaswa kulipa kodi yake.
 
Kuwa mwangalifu sana hapo. Si rahisi sana kumtoa mpangaji kama mkataba hauelekezi. Hapo anza ofisi ya kata ward tribunal au kwa Mwanasheria uanzishe tenancy notice
 
Habari zenu wananchi,

Tuna mpangaji ana mwezi wa sita hajalipa kodi na ni mwalimu anafundisha shule za Serikali, tumeazimia kumuamisha na tunataka kupata stahiki yetu tunafanyaje?

Naombeni msaada
Kwahiyo mkuu umekuja kunidiss huku? Sasa nasema kodi yako silipi na hapa sihami
 
Mpaka anadaiwa miezi yote nyinyi mlikuwa mmekufa?
Je, mna mkataba wowote kati yenu na yeye?
Kama mnao unasemaje?

Hata kama mna mkataba, naamini kabisa huo mkataba unaeleza ni namna gani mpangaji anapaswa kulipa kodi yake.
ni mkataba wa kupangishana tu bei ya pango kwa mwezi na jinsi inavyopaswa kulipwa
 
Fungueni "application" kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya katika Wilaya ambayo hiyo nyumba mliyompangisha ipo.

Haya ni maombi maalumu ya kumlazimisha mdaiwa alipe deni la kodi lililosalia (arrears of rent) na kumtoa kwenye nyumba hiyo (lawful eviction).

Ni vema mkamuona mwanasheria/wakili kwa msaada zaidi.

Karibuni mnunue kitabu changu chenye jina DONDOO MUHIMU ZA NAMNA YA KUKABILIANA NA KESI ZA ARDHI, JINAI, MADAI, MIRAHI NA NDOA HASA KWA WASOMAJI WASIO WANASHERIA NA WANASHERIA WACHANGA (SOMO FUPI LA SHERIA KWA VITENDO). Kitawapa msaada mkubwa sana. Bei ni sh. 10,000/= tu. Nipo Dodoma ila mikoani natuma.

Aksanteni!
 
Fungueni "application" kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya katika Wilaya ambayo hiyo nyumba mliyompangisha ipo.

Haya ni maombi maalumu ya kumlazimisha mdaiwa alipe deni la kodi lililosalia (arrears of rent) na kumtoa kwenye nyumba hiyo (lawful eviction)...
Ahsante sana
 
Habari zenu wananchi,

Tuna mpangaji ana mwezi wa sita hajalipa kodi na ni mwalimu anafundisha shule za Serikali, tumeazimia kumuamisha na tunataka kupata stahiki yetu tunafanyaje?

Naombeni msaada
Hao wapangaji wa hivyo dawa yao huwa kuwaroga tu full kumchezasha kindumbwendumbwe atahama mwenyewe
 
Ushauri... Cut the Loss..., (unless otherwise unadai millions of money) muondoe tafuta mwingine mwenye historia nzuri endelea na biashara (hizo ndio zinaitwa cost of doing business)

Kibongo wapangaji ni pasua kichwa, sometimes mtu unaweza kuwaza bora hili jengo nifugie kuku...
 
Kuna bibi mmoja alikuwa na tatizo kama lako....alichofanya alisubiri msimu wa mvua akaanza kufanya marekebisho ktk nyumba yake then akaondoa bati zote katika chumba cha mpangaji mkorofi kisha akazifungia ndani ...mpangaji alihama baada ya mvua mmoja tuuu....ila wewe usifanye kama huyu bibi hahaaaaaaaaaa
 
bibi ni muhuni huyo
 
Back
Top Bottom