Msaada: Kilimo cha Matango, Utaalam na Masoko

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Ndugu zanguni naombeni msaada wenu tafadhali.

Kilimo cha matango gharama zake zipoje, kuanzia hatua ya kwanza mpaka hatua ya mwisho kwa ekari moja tu.

Ukiachana na gharama za kukodi shamba kwani shamba nimeshapata tayari. Naheshimu mawazo yenu sana na naamini mtanipa mawazo yanayojenga. Na faida yake ipoje kwa ekari moja.

Thnx in advance

===============================================
MASWALI MENGINE KUHUSU BIASHARA HII
=============================================

Poleni na majukumu wakuu wa jamvi hili maridhawa.
Naomba mwenye utaalamu juu ya kilimo cha matango anisaidie kujibu hoja zifuatazo:
1. Mbegu kiasi gani zinatosha heka moja.
2. Spacing yake kwenye upandaji ikoje?
3. Msimu mzuri wa kulima matango ni upi.
4. Mahitaji muhimu.
5. Wastani wa gharama za kulima heka moja.
6. Wastani wa mapato kwa heka moja.

Natanguliza shukrani za dhati kwa wote wakaochangia mawazo yao hapa. Ahsanteni sana.

Nawasilisha!
 
Ngoja nikuitie mkulima Malila.

Kuna mambo mawili ningehitaji kuyaweka wazi, je unataka kulima matango ya kienyeji au ya kisasa? Matango ya kienyeji mara nyingi soko lake ni Wahindi na yanaweza kukaa muda mrefu. Ya kisasa soko lake ni kubwa na yanaweza kuuzwa hata uswahilini kwetu.

Ukitunza vizuri, unaweza kupata michumo mitano, vigezo vya kupata faida ni vingi; aina na soko lako,ubora wa mazao yako, gharama za uendeshaji. Ila matango hayaangushi watu kama matikiti maji.Nikushauri uende pale soko Mjinga Kisutu ukapate bei ya roba moja la matango.
 
Kuna mambo mawili ningehitaji kuyaweka wazi, je unataka kulima matango ya kienyeji au ya kisasa? Matango ya kienyeji mara nyingi soko lake ni Wahindi na yanaweza kukaa muda mrefu. Ya kisasa soko lake ni kubwa na yanaweza kuuzwa hata uswahilini kwetu.

Ukitunza vizuri, unaweza kupata michumo mitano, vigezo vya kupata faida ni vingi; aina na soko lako,ubora wa mazao yako,gharama za uendeshaji. Ila matango hayaangushi watu kama matikiti maji.Nikushauri uende pale soko Mjinga Kisutu ukapate bei ya roba moja la matango.

Mkuu kwanini unasema Matango hayaangushi watu kama Matikiti Maji? What is wrong with Matikiti Maji? Inamaana Matango yanalipa kuliko Matikiti Maji? nilikuwa nafikiri ni vice versa
 
Mkuu kwanini unasema Matango hayaangushi watu kama Matikiti Maji? What is wrong with Matikiti Maji? Inamaana Matango yanalipa kuliko Matikiti Maji? nilikuwa nafikiri ni vice versa

Matango hayasumbui sana ktk ulimaji wake kama matikiti maji. Na ni wakulima wachache wanalima hivyo kitu kinaingia sokoni na hakikai. Michumo ktk shamba inafika mpaka mitano, tofauti na tikiti maji. Point hapa iko ktk supply.
 
Vp soko lake ni la uhakika?
 
Matango hayasumbui sana ktk ulimaji wake kama matikiti maji. Na ni wakulima wachache wanalima hivyo kitu kinaingia sokoni na hakikai. Michumo ktk shamba inafika mpaka mitano, tofauti na tikiti maji. Point hapa iko ktk supply.

Mkuu Malila vipi kuhusu kushambuliwa kwake na magonjwa na mahitaji ya mbolea hasa kwa kuzingatia na swali la mkuu hapa chini;

Huwa matango yanaota wapi, katika udongo na hali ya hewa ya namna gani?
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na Malila soko ni la uhakika ,ila msimu huu maana ndo tunavuna ,soko si zuri sana bei imeshuka mno kwa sehemu za pwani.

Mkuu bei imefika kiasi gani na kawaida ni bei gani?
Inawezekana uzalishaji umeongezeka ndio maana bei imeshuka.
Ni kipindi gani kizuri kulima matango ukanda huu wa pwani?
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom