Msaada: Kama watu alifunga ndoa wakiwa dini fulani, wakihama dini hiyo watahitajika kufunga tena ndoa?

Hii debate haijapata mjuvi wa kisheria akatufungua.
Maana kumekuwa na makundi mawili bishani! Pia mjadala umeegemea kubadili na kuingia uislam, hakuna popote mjuvi amedadavua kuhusu muislam kwenda ukristu hasa ukatoliki.
Wanajamvi tupate mjuzi hasa wa sheria za ndoa atuondolee kitendawili fikirishi hiki.
Sasa kama hili suala mmelifanya ni debate je unategemea kusiwepo majibu tofauti?

Lingebaki swali tu endapo ikitokea wanandoa kwa pamoja wa dini A wakibadili dini na kuwa dini B je kwa taratibu za hiyo dini B zinasemaje kuhusu ndoa yao kuwa watapaswa kufunga ndoa nyengine kwa taratibu za dini B au hiyo hiyo ndoa yao ya awali tu inatosha?
 
Ndugu yangu unapoizungumzia ndoa unazungumzia jambo la kutekeleza amri ya mungu,hakuna ndoa ya serikali.
Huwezi kukurupuka ukasema ndoa dini inapewa baraka na serikali!!!!huna dini wewe.ndoa hufungwa kidini ktk kutimiza agizo la mungu na kuacha katazo lake la zinaa.hivyo veti vimekuja miaka kadhaa baada ya Uhuru na ndoa zilikuwepo before.tunapewa vyeti kuthibitisha ndoa baada ya changamoto kuzidi kwny ndoa ikiwemo ya wanandoa kukanana.
Wanandoa wasio waislam wanaposilimu na kuwa waislam ndoa yao wataifunga upya sababu ndoa hiyo ya awali ilikua nje ya uislam.
Nje ya uislamu ndoa hiyo ni batili sababu kuna nguzo za ndoa ya kiislam lzm zifuatwe na nje ya uislam wana njia zao pia.
Kinachorudiwa upya ni ndoa si harusi.
Usitoe fat'wa katika dini km jambo huna Elimu nalo. Kukaa kimya ni bora zaid
 
***Kama wameingia Kwenye uislam na kuwa waislam jina basi cheti cha serikali kitawafaa zaidi


***Lakini Kama wameingia Kwenye uislam na kutaka kuwa waumini bora wakislam na kutaka kufata nguzo tano za kiislam

1) Shahada ya Imani

Ushahidi wa Imani ni kusema kwa kusadikisha, “La ilaaha illAllaah, Muhammadur Rasulullah.” “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (Allaah), na kwamba Muhammad ni Mjumbe (Mtume) wa Mwenyezi Mungu.”

2) Swalah (kuswali Swala tano)
Waislamu huswali Swalah tano kila siku. Kila Swalah huchukuwa muda mfupi wa dakika chache tu.

3) Kutoa Zakaah (Kuwakunjulia Wenye Dhiki):


4) Kufunga katika Mwezi wa Ramadhaan Kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani.

5) Kuhiji Makkah.


Itawapasa wafunge ndoa upya ya kiislam Ili wapate kuzitimiza hizi nguzo tano za kiislam
Nauliza kwani wakati wa kufungusha ndoa hizi nguzo tano ni sehemu ya maneno yanayotumika? Mimi nafikiri nguzo hizo zinatumika ktk procedure za kusilimisha ......
 
Kama walifunga kikistu alafu wakasimu wakawa waislam kitendo cha kusilim tuu ndoa ya zamani imevunjika.Wanatakiwa waowane tena
 
Kinachohalalisha ndoa Ni cheti.
Cheti Ni Cha Serikali.
Iwe Ni Muislamu au mkristo Cheti Ni kile kile.
Wewe ukapimwe mkojo.
Hujaoa wala huna dini na huna ulijualo labda bado mtoto ama uzwazwa umekujaa.
Kinachohalalisha ndoa ni cheti????wewe nahisi ni mtu toka kuzimu au bichwa box
 
Kinachohalalisha ndoa Ni cheti.
Cheti Ni Cha Serikali.
Iwe Ni Muislamu au mkristo Cheti Ni kile kile.
Cheti kinatolewa kwasababu tu ya mambo ya mirathi, kugawana Mali pindi wanandoa wanapotalakiana, sheria Lazima iingilie Kati Ukikosoa cheti cha ndoa unaweza Kosa Haki Yako ni km ushahidi tu.
 
Nauliza kwani wakati wa kufungusha ndoa hizi nguzo tano ni sehemu ya maneno yanayotumika? Mimi nafikiri nguzo hizo zinatumika ktk procedure za kusilimisha ......

Hizo ni nguzo tano kila Muislamu anatakiwa kuzitekeleza na hayo siyo maneno . Sio wakati wa kusilimishwa .


Wakati wa kuslimu itampasa atamke

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, wa ashhadu anna Muhammadar Rasuulu-Allaah.
(Nakiri na kutamka kuwa hapana apasaye kwa dhati kuabudiwa ila Allaah, na nakiri kuwa Muhammad ni Mjumbe Wake)

Hizo nguzo za uislam atazitekeleza baada ya kuslimu yaani kuswali Swala tano, kutoa zakka, kufunga Ramadhani na kuhiji makka.
 
Mbona wengine mnatoa mapovu ya omo kumbadilishia swali muulizaji?
Nadhani mtu kama swali hujui jibu lake bora upite tuu na si kumtoa kwenye mstali muulizaji.
Wajuzi waje kumjibu muulizaji nae akiridhika bhasi wengine mtoe maswali yenu kupitia hoja ya muulizaji
 
Mi naamini kama walikuwa waislam wakahamia ukristo esp RC watafunga ndoa tena maana kuna sakramenti kama ubatizo, kipaimara ambazo zinatolewa kabla ya ndoa, itabidi wapitie hizo hatua kwanza ndio wafunge tena ndoa.
 
"Eti, ikitokea watu wawili wamefunga ndoa ya KIKRISTO pindi wakiwa wakristo, halafu baada ya muda wote wawili wakaamua kuslimu na kuwa waislamu. Je watafunga tena ndoa ya kiislamu?

Darasa huru, huu mjadala nimeukuta mahali katika pitapita zangu ila sijfanikiwa kupata jibu... Kama hujui like tu kisha pita soma maoni ya watu na ww utajifunza kitu.
Ndoa ni nini? ni ibada ya muunganiko wa pande mbili mke na mume. muunganiko huu hutokana na ridhaa zao na watu wao wa karibu(wazazi). kwa maana Baba wa mke inabidi akukabidhi binti yake kwa ridhaa yake kwa njia ya kiapo na huyo binti akubali hiko kitendo na mume nae akubali kukabidhiwa aktika kukubali kwao ni lazima kuwe na mashahidi wanaoshuhudia watu hao wakikubali. Kwa hiyo mmoja kati ya hao (mke,mume,baba) akikataa hapo ndoa haiwezi fungwa. nikirejea mada hapo juu ndoa haiwezi fungwa tena kwa sababu wote 3 walikuwa na wako willing na tukio hilo, ila akisilimu mmoja let's say mume inamaana willingness haipo tena kwa mke na baba ake hivyo no ndoa.
 
Mkuu hicho Cheti kinahalalisha ndoa kwa mujibu wa nani? Kama Cheti ndo kinahalalisha Ndoa, Kanisani kinachofanyika ni nn?
Mtu anayefungia ndoa kanisani,msikitini au bomani wote wanasaini cheti kile kile Cha ndoa.
Tofauti Ni kwamba Mkristo anasaini box la ndoa ya Mke Mmoja,na mwislamu anasaini ndoa ya wake wengi.
 
Mtu anayefungia ndoa kanisani,msikitini au bomani wote wanasaini cheti kile kile Cha ndoa.
Tofauti Ni kwamba Mkristo anasaini box la ndoa ya Mke Mmoja,na mwislamu anasaini ndoa ya wake wengi.
Sawa kabisa hayo yanafanyika ili kupatikane uhalali wa Kisheria na kutambulika katika ngazi za Kiserikali.
Je,Kiimani uhalali wa ndoa ni upi? Na je kwa Imani ya Ukristo, Wanandoa Wakiislamu wakibadili dini kuwa Wakristo ndoa yao inaeendelea kama awali au itabidi wafunge ndoa upya?
 
Nikitaka kuongeza mke wa pili au kumlima talaka inakuweje hapo?
Wakati ndoa tulifunga kanisani!
Baada ya kusilimu unaruhusiwa kuongeza mke mpaka wanne ikiwa Una uwezo na hivyo hivyo msipoelewana mtafuata taratibu za talaka wallahu Aalam!
 
sorry mimi sio muislam na sina elimu ya kutosha ya uislam ila ningependa kuchangia mada kwa kutumia utashi na akiri yangu tu alionijalia ALLAH, mimi nazani itabidi wafunge ndoa tena kwasababu
uislamu (dini ya kislamu) hauitambui ukristo kama ni dini na inafata misingi ya ALLAH, hiyo inamaana kwamba yale yote yanayofanyika ktk ukristo si maamlisho ya mungu, hivyo tendo la ndoa ktk ndoa ya kikristo ni sawa na dhinaa katika uislamu.
pili, ndoa ya kiislam ina mashariti na vigezo vyake ambavyo vikifuatwa na kukamilishwa ndio uhesabika kua ndoa na ukristo una vigezo vyake pia ktk ndoa zao hivyo yale yote yanayofanyika wakati wa ndoa ya kikristo ni batili katka uislamu.
hivyo kusema kwamba ndoa itaendelea kuhesabika pindi wanandoa wanapotoka ktk ukristo kwenda ktk uislamu ni sawa na kusema yale yote yaliyofanywa wakati wa kufunga ndoa ya kikristo na hata baada ni halali na uislamu unayatambua!.
kwasababu hizo za kufikirika nahisi hawa wanandoa km watataka waendelee kuesabika kua ni wanandoa basi itabidi wafunge tena ndoa.
sorry kwa kuingilia mada
 
Sawa kabisa hayo yanafanyika ili kupatikane uhalali wa Kisheria na kutambulika katika ngazi za Kiserikali.
Je,Kiimani uhalali wa ndoa ni upi? Na je kwa Imani ya Ukristo, Wanandoa Wakiislamu wakibadili dini kuwa Wakristo ndoa yao inaeendelea kama awali au itabidi wafunge ndoa upya?
katika ukristo hao itabidi wafunge tena ndoa ktk misingi ya kikristo, yale yote yaliyofanyika wakati wa ndoa yao ya kislamu huesabika ni dhinaa na itawapasa kutubia zambi zao
 
hawatafunga tena ndoa ila kama huyo mtu alikuwa na wake zaidi ya wanne basi itamlazimu kuacha hao wengine mpk wabaki wa nne
 
Back
Top Bottom