Msaada juu ya malipo ya bima ya gari:

JituParaTupu

Member
Nov 20, 2008
92
9
Ninamiliki gari ambayo nilikatia bima ya Comprehensive ya kuwa compensated 9m/- na nimekuwa nikikata bima hii kwa takriban miaka 6. Gari yangu ilipata ajali na kesi kufanyika na makosa kuonekana kwa yule aliyenigonga.

Nimeshangazwa kwa kulipwa chini ya milioni moja kinyume na matarajio yangu ya kulipwa 9m au 8m. Naomba kuelimishwa jinsi ya kudai haki yangu. Nawakilisha nikitegemea kusaidiwa gaps jamvini.
 
pole sana kiongozi. Inauma sana

sasa mkuu ulikata bima yako kampuni gani? Comprehensive insurance uliyokata ni kwa kampuni hiyo hiyo au tofauti tofauti? Je ulikata bima kupitia broker/agent au moja kwa moja kwa insurance company
 
Ninamiliki gari ambayo nilikatia bima ya Comprehensive ya kuwa compensated 9m/- na nimekuwa nikikata bima hii kwa takriban miaka 6. Gari yangu ilipata ajali na kesi kufanyika na makosa kuonekana kwa yule aliyenigonga. Nimeshangazwa kwa kulipwa chini ya milioni moja kinyume na matarajio yangu ya kulipwa 9m au 8m. Naomba kuelimishwa jinsi ya kudai haki yangu. Nawakilisha nikitegemea kusaidiwa gaps jamvini.

Mkuu, kwani gari lako lilikuwa total written off?
 
Swali la msingi sana! Pia sielewi issue ya kesi inaingiaje kwenye comprehsnsive insurance, kwa kuwa hata kama wewe una kosa, so long gari yako ina comprehensive cover kampuni yako ya bima lazima ukulipe.

sure, jamaa anabidi aeleze vizuri iyo loss yake ni ya kiasi gani. uwezi pata hasara ya laki tano halafu ulipwe 9m! contract of insurance concern indemnification ie you will be compensated exactly to the position you were before the loss.
 
bima wanalipa kulingana na ukubwa wa ajali kwakuzingatia ripoti ya polisi, makisio ya karakana ulipopeleka gari na ripoti ya mkadiriaji toka bima
kwa mfano gari imeumia ngao ya mbele na taa kubwa na kioo bima watalipa vitu hivyo tu na baada ya kupitia utaratibu huo hapo juu
pia nakushauri usome 'policy' ya kampuni husika ili ujue nini ni nini kikitokea kipi
 
Unalipwa kulingana na damage uliyoipata,
Huwezi kulipwa gari zima kwa ajili ya ka-pasi kadogo tu eti kisa umekata comprehensive
 
mkuu unalipwa kilicho haribika. kama gari haifai kuingia barabarani ndo unalipwa gari jipya. gari yako hata ikitengenezwa kuna gharama hata wewe itakupasa kutoa, 10% ya gharama ya matengenezo utatoa wewe wengine ni zaidi au pungufu ya hapo inategemeana na kampuni ya bima. hiyo gharama ni kama tozo la kukufanya usijiachie barabarani eti kwa kua una bima. hata wewe unachangia gharama. mia
 
Hivi kuna umuhimu kweli wa kufanya bima ya magari binafsi kuwa ya lazima? Naona ingefanywa hiari kwa anayetaka..ni wazo tu wadau
 
Hivi kuna umuhimu kweli wa kufanya bima ya magari binafsi kuwa ya lazima? Naona ingefanywa hiari kwa anayetaka..ni wazo tu wadau

Mkuu nchi nyingi kama sio zote bima za magari ni lazima kutokana na kwamba madhara yanaweza kumpata mtu wa tatu (Third paty) ambae hausiki.. for instance, wewe unatembea barabarani alafu kwa bahati mbaya gari likakugonga hapo unatakiwa kupewa compensation. mfano mwengine, umekaa mahali labda kuna ujenzi unaendelea kwenye jengo tuseme gorofa alafu nyundo ikakudondokea(Public liability)
 
Jitahidi unapokata bima, wakupe maelekezo yote ya bima yako. halafu pia polisi nao wanachangia watu kupunjwa bima zao
 
Mkuu nchi nyingi kama sio zote bima za magari ni lazima kutokana na kwamba madhara yanaweza kumpata mtu wa tatu (Third paty) ambae hausiki.. for instance, wewe unatembea barabarani alafu kwa bahati mbaya gari likakugonga hapo unatakiwa kupewa compensation. mfano mwengine, umekaa mahali labda kuna ujenzi unaendelea kwenye jengo tuseme gorofa alafu nyundo ikakudondokea(Public liability)

Wi-Fi, Nimejaribu kusoma policy ya bima ya gari niliyokata sikuona kipengele kinachozungumzia third party. Mathalani wanasema uorodheshe baadhi ya vitu specific kwenye gari mf windscreen, head lamps etc lakini kuhusu binadamu hiyo sikuona
 
mbona hoja nying hujibu, wewe unataka msaada kweli? bima iliyo kulipa ni yako au ya yule aliye kugonga?
 
Ndugu zangu jamvini nachukua fursa hii kwa wote waliochangia na kushauri kwa njia moja au ingine. Nimeweza kuelewa kila kilichoandikwa nanyi katika kutaka kunisaidia. Kesho naahidi kuja na full information kuhusiana na ajali na tatizo langu katika ujumla wake na nadhani kuanzia hapo mtaweza kunipa ushauri mzuri kuelekea kulipwa bima yangu. Izingatiwe kwamba ni mara yangu ya kwanza kupata ajali ya barabarani tangu nianze kumiliki chombo cha moto mnamo mwaka 1986. Asanteni sana ...ni hapo kesho.
 
mkuu ni kamouni ipi ya bima ambayo ni nzuri?
mkuu unalipwa kilicho haribika. kama gari haifai kuingia barabarani ndo unalipwa gari jipya. gari yako hata ikitengenezwa kuna gharama hata wewe itakupasa kutoa, 10% ya gharama ya matengenezo utatoa wewe wengine ni zaidi au pungufu ya hapo inategemeana na kampuni ya bima. hiyo gharama ni kama tozo la kukufanya usijiachie barabarani eti kwa kua una bima. hata wewe unachangia gharama. mia
 
Bima haipo kumfaidisha mtu yeyote ipo kwa ajili ya kukurudisha katika hali uliokuwepo kabla ya ajali.Kama ulikatia bima kwa milioni 9 na kama ilikuwa total loss, kinachofanyika asesa ataikagua na lazima uchakavu uhusishwe kwenye gari yako (i mean depreciation lazima ita apply).Ndio maana kila unapo renew gari lako lazima umwambie insurer wako current market price ya gari yako baada ya kulipeleka kwa wataalam wakague na wakupatie mechanical report pamoja na thamani.Bahati mbaya watu wengi hatufanyi hivyo na tunaamua ku base kwenye thamani ya zamani.Ukikata Comprehensive ndanimo kuna, FIRE,THEFT,OWN DAMAGE & THIRD PARTY.Sioni unacho lalama ila unatakiwa kabla huja kata Comprehensive lazima ujue policy yao ikoje sio kukurupuka unaenda tafuta vya bei rahisi halafu claim ikitokea unaanza kuhaha.
 
mkuu unalipwa kilicho haribika. kama gari haifai kuingia barabarani ndo unalipwa gari jipya. gari yako hata ikitengenezwa kuna gharama hata wewe itakupasa kutoa, 10% ya gharama ya matengenezo utatoa wewe wengine ni zaidi au pungufu ya hapo inategemeana na kampuni ya bima. hiyo gharama ni kama tozo la kukufanya usijiachie barabarani eti kwa kua una bima. hata wewe unachangia gharama. mia
.Maelezo mazuri lakini kasoro ipo hapo kwenye kulipya gari jipya.most ya magari yetu ni used so utalipwa kulingana na uchakavu wa gari yako.Kama umenunua gari mpya kutoka kwa dealer eg D.T Dobie na bahati mbaya ukapata ajali ndani ya mwezi mmoja hapo unalipwa gari jipya kwa sababu depreciation itakuwa very minimal
 
Ndugu zangu jamvini nachukua fursa hii kwa wote waliochangia na kushauri kwa njia moja au ingine. Nimeweza kuelewa kila kilichoandikwa nanyi katika kutaka kunisaidia. Kesho naahidi kuja na full information kuhusiana na ajali na tatizo langu katika ujumla wake na nadhani kuanzia hapo mtaweza kunipa ushauri mzuri kuelekea kulipwa bima yangu. Izingatiwe kwamba ni mara yangu ya kwanza kupata ajali ya barabarani tangu nianze kumiliki chombo cha moto mnamo mwaka 1986. Asanteni sana ...ni hapo kesho.

Shikamoo mzee, na pole sana kwa maswahiba yalokupata. Umeazakumilikai chombo cha moto nikiwa na miaka mitatu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom