Msaada juu ya IPad

Msaada juu ya IPad

g.n.n

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
407
Reaction score
49
Habari
Swali ni kwamba kitendo cha ku Jailbreak IPad ina bad impacts kwenye IPad?
Kama zipo can u tell me some, na Kama zinaweza kuepukika au la, pia Kama kuna advantages zake pia naomba uniambie.
Hope kwamba wenye uzoefu na jambo hili watanisaidia.
 
Kuijailbreak ni kuitoa jela. Unakuwa umeondoa restriction yao za kununua kila app kutoka APPLE STORE tu, na badala yake unaweza kuinstall apps from outside their apple store.
 
Kuijailbreak ni kuitoa jela. Unakuwa umeondoa restriction yao za kununua kila app kutoka APPLE STORE tu, na badala yake unaweza kuinstall apps from outside their apple store.

Ok, what about the impacts to the device, I mean negative Impacts.
 
Jailbreaking is basically the process of freeing your device (thus the term jailbreak) from the limitations that are imposed by Apple.
Cydia ndo black market/alternative appstore ambayo ndo main reason unajailbreak ur idevice

Advantages of Jailbreaking
1.Third-party Jailbreak Apps and Tweaks
2.Paid Apps from App store unazipata free
3.Unlocking iPhone/iPad
4.Full customization
5.Very easy and fast 2 jailbreak and easily reversible

Disadvantages
1.bugs and glitches:sometimes ipad/iphone/ipod inastuck for a second kama ukiinstall vitu vibaya but inatokea mara chache sana and rahisi kusolve
2.ukiupdate device na jailbreak inatoka
 
Waungwana walionitangulia wameshaeleza faida na hasara kwa vizuri; ninachotaka kusisitiza ni kutumia jailbroken na unjailbroken iPad ni utashi binafsi, kama unaweza kufanya mwenyewe ningekushauri ujaribu ujionee badala ya kukubali kuhadithiwa, ila kama unamlipa mtu akufanyie basi sio jambo la kulifanya. Uzuri wenyewe ukichukizwa na jialbreak ni rahisi kurudi jela.

1. Kiufupi hasara ni kuwa mara nyingine (sio kila wakati) au niseme huenda ikapelekea iPad yako iwe-unstable (apps zinajifunga, kasi inapungua na hata kujizima wenyewe)

2. Hasara nyingine ni kwamba ukianza na kuipenda basi umeingia kwenye mbio za paka na panya. Yaani Apple wanatoa update inarudi kuwa un-jailbroken halafu wewe uanze tena kuhangaika ku-jailbreak upya.

3. hasara ya tatu' wakati mwingine mwengine jailbreak hutoka wakati muafaka na wakati mwengine huchelewa mno, hivyo ama inakubidi ubaki nyuma na ukosefu feature mpya au ukubali kuishi bila ya jailbreak kwa muda utakaosubiri, tatizo apps unazozoea kuzitumia huwa unajenga mahusiano nazo hivyo kuzikosa inakuwa taabu wakati mwengine.

4. Apps ambazo hazikupitia app store zinaweza kuwa na bugs na hivyo kuwa na performance isiyorodhisha, lakini ndio ughali wa bure.

Faida
1. Apps za bure na za ziada ambazo huwezi kuzipata appstore.

2. Njia ya mkato ya kufungua iPad iliyofungwa ingawa inapotoka update inakubidi ufungue tena (unlock) na hii ni kwa iPad zenye 3G/4G ambazo zimenunuliwa kupitia service provider badala ya Apple moja kwa moja.

Kwa ujumla kama ni mtu ambaye hutaki kununua Apps basi jailbreak ni jambo la maana, la kama una uwezo na uko tayari kutoa vijisenti kununua apps basi (kwa maoni yangu) jailbreak haina maana zaidi ya kujiongezea kazi. Binafsi nilikuwa na-jailbreak na sasa nimechoshwa na "mbio za paka na panya" nikitaka ku-unlock naomba official unlock code kutoka Apple au service provider (unalipa mara moja) update zote unapata bila ya kujilock tena, nikitaka apps natoa vijisenti.

There is no harm to jump in the pool if you can swim.
 
Hata mimi sijaona umuhimu wa kujailbreak yangu. Apps zenyewe ziko bei rahisi sana most of them! Sitaki hata kujaribu!
Labda yeye aeleze anataka kujailbreak ili apate nini?
 
Shukran wadau nimewasoma, nimejua nn cha kufanya sasa.
 
Back
Top Bottom