Njia ninayoijua mimi inafanya kazi kama una simu na mtandao wenye 4g. Cha kufanya nenda playstore alafu download application inayoitwa "4G switcher"; hii application itakupeleka kwenye eneo la simu linaloonyesha "Device Info", hapa sasa Nenda kwenye mahala panapoitwa "Set Preferred Network type" Alafu chagua "Lte only". Basi hapo simu hazito ingia kwa sababu mitandao yetu ya Bongo, ukitoa Smile haina VoLTE (voice over LTE). Mtu akipiga utaonekana busy na mtandao wa simu wako kama una support itakutumia message kuwa flani flani alikupigia.