Msaada juu ya aina ya laptop ya kununua

Msaada juu ya aina ya laptop ya kununua

Mwiyuzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2011
Posts
854
Reaction score
447
Habari za jioni wanajamvi

Naomba ushauri juu ya aina ya laptop ya kununua ikiwa nina laki sita mkononi kwa ajili ya laptop.

Nimejaribu kuzunguka nikakuta kuna laptop aina ya samsung ambayo ni laki tano na tisini na tisa 5990000 mlimani city na nikaenda posta na kuona laptop ya toshiba ni 580,000.

Sasa je kati ya SAMSUNG na TOSHIBA ipi ni nzuri zaidi?

Naombeni ushauri
 
Binafsi nakubali sana bidhaa za Samsung sio tu kwenye lap top. bali hata vitu vingine kama TV, friji etc.
Kwa ushauri wangu, Samsung is better.
 
Toshiba. ila unatakiwa ujue vitu kama size ya HDD, Proc. Speed, RAM size, CD/DVD rom, WIFI, BT, Uzito wake, size ya CD, muda battery kuisha baada ya kuwa charged na unaitaka kwa ajili ya kazi gani ili uweze kuchagua laptop nzuri
 
Kaka mm nadhan mashine zote zipo poa ila inategemeana na wewe mwenyewe kua unapenda ipi. Hata hivyo mm nakushauri ununue HP/Compaq hp ni nzuri sana. Suala la bei linategemeana na mkoa ulipo ila kwa sehemu kama Arusha utapata lap safi kwa hiyo bei.
 
Ni kwa ajili ya kusomea tu coz kuna baadhi ya materials yapo kwenye soft copy, ningependa pia yenye uwezo wa kuwekwa CD/DVD ili niweze kurefresh coz cna tv
 
Kaka mm nadhan mashine zote zipo poa ila inategemeana na wewe mwenyewe kua unapenda ipi. Hata hivyo mm nakushauri ununue HP/Compaq hp ni nzuri sana. Suala la bei linategemeana na mkoa ulipo ila kwa sehemu kama Arusha utapata lap safi kwa hiyo bei.
Galaxy Computers Arusha atapata cmptr mtumba nzuri sn kwa 540,000.
Nilimnunulia wife cmptr hapo Dell Latitude 6400 ni kama mpya, betri 3hrs unadunda bila wacwac.
 
Nipo Dar es salaam na siyo Arusha
 
Galaxy Computers Arusha atapata cmptr mtumba nzuri sn kwa 540,000.
Nilimnunulia wife cmptr hapo Dell Latitude 6400 ni kama mpya, betri 3hrs unadunda bila wacwac.

betri inabidi iwe approximately 8 hours when charged. Houni depreciation yake kuwa ni kuuuubwa na scrap value matatizo?
 
Kaka kwa mishemishe za chuo ogopa sana samsung maana zinakufa sana display ukiigongesha kidogo kwenye mishemishe za kugombania shuttle au daladala za mjini me naona bora ununue lenovo hutojuta maana ni jembe ackwambie mtu
 
asante kwa kunitaadhalisha
 
Samsung pc za uongo . .chukua nyingine .duka ni freedom electronics wanauza pc nzuri at the best price
 
Hp,dell ninzuri lakini kama una 600000 nibora uongeze laki mbili ununue brand new na genuine maana zipo kwabei hiyo bati china low qrty
 
Toshiba mi nazikubali sasa tatizo hujasema hiyo toshiba na samsung ni za toleo lipi maana kutaja tu toshiba au samsung bado hakuna aliyekuelewa unamaanisha nini.

MHIMU KULIKO VYOTE HIYO CD ROM/WRITER NI KWA AJILI YA KUFUNGIA WINDOWS PALE ITAKAPOCORRUPT AU KUCHOKA, TAFADHARI SANA USITUMIE KUANGALIZIA DVD AU CD, KAMA UNAPENDA MOVIE ZICHUKUWE KWENYE FLASH NA UZIWEKE KWENYE MASHINE MOJA KWA MOJA NA HIZO MOVIE ZIWE ZINAHUSU MASOMO TU, samahani lakini.
 
Kwa bei hiyo utaishia kupata laptop feki tu!
 
mimi kwa upande wangu a laptop is a laptop as long as inakidhi specification nazozitaka lakini HP compaq presario kwangu hapana nimeshuhudia kama 3 zinaungua motherboard.
Toshba si kati ya laptop nazozikubari.
 
Atapata tena nzuri sana, kwani we unaishi wapi? yeye anataka kwa ajili ya kutunzia vitabu na kama kifaa cha masomo kwa ujumla, kwanza mimi ningemshauri anunuwe used tu kwa matumizi hayo, computer used iliyotengenezwa ulaya ya laki 3 inamtosha kabisa.

Kwa bei hiyo utaishia kupata laptop feki tu!
 
Back
Top Bottom