habari wakuu, nina duka langu nimenunua kutoka kwa mtu, huyo mtu aliniuzia kwa kuwa yeye, alishindwa kuliendesha kwa kuwa mauzo yote aliyokuwa anapata alikuwa anatumia kwenye ujenzi wa nyumba yake na pia alipata kazi ya kuajiriwa. hilo duka ni la bidhaa mchanganyiko yaani vocha, nafaka kama mchele, unga na maharage, pia kuna vinywaji, mfano juice, soda, maji. vitu ambavyo vinatoka sana ni nafaka, vocha na vinywaji. ila duka lenyewe kwa sasa bado kuna shelves ziko wazi yaani bado halijajaa. shida ni kwamba hela yote ya mauzo ya siku husika inaishia kwenye manunuzi ya vitu vya kuuza siku inayofuatia, yaani mimi kama kubakiwa na hela, naweza nikabakiwa na 5000 au 10000 au nisibakiwe na hela kabisa. naomba msaada ni jinsi gani naweza nikasave kwenye mauzo ya kila siku. yaani kila siku niweze kusave hela kidogo na niweze kuongeza vitu ambavyo vinahitajika dukani. dukani nauza mwenyewe.