MSAADA JINSI YA KUSAFISHA KUKU WA NYAMA

MSAADA JINSI YA KUSAFISHA KUKU WA NYAMA

Qsm

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2008
Posts
450
Reaction score
263
Wanakijiji naomba msaada kwa yeyote anayejua jinsi ya kusafisha kuku wa nyama wakishachinjwa na kuwakausha vizuri ili wasibakie na majimaji ya damu kabla ya kufungasha, kwani yale maji maji yanasababisha kuku kuwa na rangi nyekundu badala ya nyeupe inayotakiwa. asanteni kwa ushirikiano.
 
Wafugaji wa kuku wa kisasa please kujeni huku
 
Kuku kuwa wekundu si majimaji na damu tu, bali ni kiwango cha umoto wa maji ya kulowekea: maji yasiwe ya moto sanaa kupitiliza, na usiloweke kuku wengi kwenye maji ya moto kwa wakati mmoja, unaloweka kidogo kidogo na kunyonyoa. Pia kiwango cha maji unachowalowekea ukishawanyonyoa nacho huchangia, unatakiwa uwaloweke kwenye maji mengii wazame kabisa na kwa muda wote halafu ukimaliza unawaweka kwa kusimama kivulini wachuje maji kwa muda mfupi tu, halafu utaona kuku watakavyokua weupe.
 
Kwakuongezea ahakikishe ameondoa vitu vyote tumboni pasibaki mapafu.koromeo.bila kusahau kanyama katako kanatabia ya kufanya kuku aoze haraka.kakate au kaoshe vizuri
 
Back
Top Bottom