Msaada jinsi ya kufika NACTE ukitokea Mbagala

kombaME

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
2,115
Reaction score
2,819
Wazima humu wapendwa,

Samahan, naomba kuelekezwa jinsi ya kufika NACTE ukitokea mbagala, naomba kuelekezwa nipande magari ya wapi hatua kwa hatua ili nifike maana ni mgeni kabisa Dar es salaam.

Ahsanteni
 
Ngoja waje wenye Daslam yao sababu sisi wengine hatujawahi kufika huko.
 
Panda magari ya makumbusho then ukifika makumbusho panda magari ya kwenda Tegeta au bunju then waambie wakushushe ITV hapo utachukua bajaj ya shs 1000 itakupeleka mpaka geti la nacte.
Ahsante boss
 
Panda magari ya makumbusho ukifika stendi makumbusho panda magari yanayoelekea Tegeta au tabata mwambie konda akaushushe kituo cha BAMAGA ukishuka hapo vuka barabara fata ofisi za startimes ukifika TBC ujue umefika NACTE
 
Hapo ulipomwelekeza ni NECTA na sio NACTE.
NACTE inabidi apande ya MBAGALA-MAKUMBUSHO. Akifika Makumbusho, apande ya MAKUMBUSHO-TEGETA/BUNJU/KAWE/UBUNGO na ashuke ITV. Akifika ITV njia rahisi ni Bajaji wanamfikisha ingawa kwa mguu ni km dk 15
 
Panda magari ya makumbusho ukifika stendi makumbusho panda magari yanayoelekea Tegeta au tabata mwambie konda akaushushe kituo cha BAMAGA ukishuka hapo vuka barabara fata ofisi za startimes ukifika TBC ujue umefika NACTE
Hii ni ya TBC ni NECTA sio NACTE
UTAMPOTEZA MKUU
 
Panda magari ya makumbusho then ukifika makumbusho panda magari ya kwenda Tegeta au bunju then waambie wakushushe ITV hapo utachukua bajaj ya shs 1000 itakupeleka mpaka geti la nacte.
Naomba nikushukuru kwa uungwana.
 
Wazima humu wapendwa,

Samahan, naomba kuelekezwa jinsi ya kufika NACTE ukitokea mbagala, naomba kuelekezwa nipande magari ya wapi hatua kwa hatua ili nifike maana ni mgeni kabisa Dar es salaam.

Ahsanteni
Panda mabus ya mbagala - makumbusho kisha shuka makumbusho ukishuka panda büs za tegeta, kunduchi au bunju na shuka kituo cha ITV hapo ūliza kwa madereva bajaji watakuonyesha njia ya kwenda NACTE
 
Ni NACTE, msaada wako tafadhali boss
Mkuu panda magari yanayoishia simu2000 then chukua boda pale waambie unaenda NACTE,buku tu,ungekuwa mwenyeji ungetembea,zipo katikati ya mwenge na ubungo,karibia na mlimani city,utaliona jengo limeandikwa NACTE..
 
Panda mabus ya mbagala - makumbusho kisha shuka makumbusho ukishuka panda büs za tegeta, kunduchi au bunju na shuka kituo cha ITV hapo ūliza kwa madereva bajaji watakuonyesha njia ya kwenda NACTE
Kwa kuongezea, unaweza muomba konda akushushe Sayansi, kutoka hapo unatembea kwa mguu(kama wewe sio mtu wa Dar) mpaka huko NECTA. Au tembea toka makumbusho hadi NECTA sio mbali fanya kama uko mkoani.
 
Duuh, msaada wako.. nafikaje NACTE
Nimeedit kwenye post uliyoniquote.
Fika Makumbusho kisha panda magari kati ya haya; MAKUMBUSHO kwenda TEGETA, BUNJU,KAWE UNUNIO,UBUNGO nk.
Kisha mwambie konda akushushe ITV. Ukifika ITV vuka barabara, chukua bajaji utafikishwa hadi NACTE.
Kama nauli majanga ni dk kama 20 kutoka hapo ITV Ila utapata tabu sana na hili jua, lakini Mimi nishatembea kwa mguu kama Mara tatu hivi
 
Kwa kuongezea, unaweza muomba konda akushushe Sayansi, kutoka hapo unatembea kwa mguu(kama wewe sio mtu wa Dar) mpaka huko NECTA. Au tembea toka makumbusho hadi NECTA sio mbali fanya kama uko mkoani.
Yeye anataka kufika NACTE na sio NECTA mkuu, wewe umeelekeza NECTA
 
Mkuu panda magari yanayoishia simu2000 then chukua boda pale waambie unaenda NACTE,buku tu,ungekuwa mwenyeji ungetembea,zipo katikati ya mwenge na ubungo,karibia na mlimani city,utaliona jengo limeandikwa NACTE..
Wewe ndo unampoteza kabisa

Unampeleka TCU.

Nacte iko mkabala na chuo cha Kodi ITA
 
Back
Top Bottom