Msaada jinsi ya kuandika notice kwa wapangaji

Joined
Nov 7, 2016
Posts
59
Reaction score
38
Plz naomba kama kuna Mtu anafahamu flow ya uandishi wa notice ili wapangaji kuachia chumba
 
Kisheria unatakiwa umuandikie barua miezi mitatu kabla mkataba haujaisha kwamba huna haja ya kuendelea na mkataba utakapoisha.
Kama mkataba umeisha usipokee pesa mwandikie barua ake mwezi bure huku akitafuta chumba
 
ila yeye anataka kufahamu
namna notice inavyoandikwa
 
Kuna masnitch wanaweza kukuelekeza kweli,mi najua ila sikwambii!
 
Kisheria unatakiwa umuandikie barua miezi mitatu kabla mkataba haujaisha kwamba huna haja ya kuendelea na mkataba utakapoisha.
Kama mkataba umeisha usipokee pesa mwandikie barua ake mwezi bure huku akitafuta chumba
kwa sisi walipa kodi ya miezi mitatu mitatu notisi inakuwa hivyo? iNA MAANA SIKU UNALIPA UNAANDIKIWA NA BARUA YA NOTISI AU?
 
Kwako ndugu mpangaji,
Husika na kichwa cha barua hapo juu.

Mimi kama landlord wako napenda kukutaarifu kuwa nimeamua kusitisha Huduma ya pango ulilopanga kwangu,Hii hutokana na kuwa nimefanya uchunguzi wakina kuwa unajihusisha na uasherati na wake za watu.

Hivi karibuni nimegundua unammendea wife wangu pindi tu nitokapo nyumbani kwenda kwenye mizunguko yangu ama kucheza bao na kunywa kahawa na kashata.

Pia umediriki kuingiza michepuko yangu chumbani kwako ambako pia ni sehemu ya nyumba yangu.

Vilevile nimechoshwa na tabia yako ya kupika pika nyama Mara ya ng'ombe,mbuzi hata ile ni ipendayo ya kitimoto bila kunikaribisha au unaogopa kwakua Mimi naitwa Tarek Mansour?

Siku za mechi huwa unajifungia ndani huku ukikata kinywaji kikali hivyo asubuhi hupelekea Mimi na familia yangu kukereka pindi utokapo chooni kwakua huwa unaacha harufu Kali.

Mwisho nakuomba naomba unitumie vocha ya buku mbili ninaahidi nitakuongezea walau wiki moja kabla hujaondoka.

Wakoo mtiifu father house
T.Mansour.
 
Ahaha...Brother
 
Back
Top Bottom