MSAADA:jinsi ya ku-control Fuel consumption kwenye gari

MSAADA:jinsi ya ku-control Fuel consumption kwenye gari

snochet

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
1,488
Reaction score
1,281
habari ndugu zangu,
ninapata shida kidogo juu ya ulaji wa mafuta kunagari aambayo tunaitumia kwa shughuli za kikazi ina 2.5 engine,kila nikiitumia mimi,wanalalamika fuel consumption inapanda from 0.11 kwa km to 0.13....nimejitahidi sana kutotembelea gear kubwa kwa muda mrefu,na kumaintain RPM isizidi 2.0 wakati wa ku-engage gear...lakini bado consumption iko palepale,akiendesha mtu mwingine kwa round moja ya full tank inarudi 0.12.....
je ninaweza nikasaidika,kwa njia mbadala na ushauri ili gari lisitumie mafuta mengi zaidi?
asanteni ,nashukuru
 
mimi hata baiskeli sina wewe unazungumzia gari. Hujui kuwa gia no 1 na 2 ndo inakula mafuta?
 
hao wanaotumia wanatumiaje?

Njia nzuri ni kupiga kibrazil mkuu....

Otherwise weka wese
 
Acha kuitumia hiyo gari, isije kupa utata kwa bosi wako bure
 
snochet,
Hakikisha vitu vifuatavyo viko vema. Ni sehemu tu ya sababu
1. Usitembee gia isyolingana na mwendo. Kila ukiona mwendo umeongezeka ongeza gia na kinyume chake
2. Usipande mlima na gia isyostahili (1 recommended but 2 kwa vijimlima) tumia akili ya kuzaliwa kujua wapi upande na nini
3. Hakikisha hausimami na breki ghafla isipokuwa imebidi. Jifunze kupunguza mwendokasi unapolelekea kusimama (decelerate). Breki za ghafla hutumia nishati ya ziada kusimama na kuibadili kuwa joto na hupoteza ile uliyotumia kukimbia.
4. Hakikisha unanunua mafuta ktk "sheli" zenye majina matukufu na sio ovyoovyo tu.
5. Kama unafanya jambo fulani zima gari usiiache ktk silent mode. Zima hata kama utatumia dakika kumi.
6. Hakikisha gari ipo vizuri: ina mafuta, oil, maji, na upepo ktk tairi wa kutosha
7. Katika safari ndefu usikimbie sana maana utakuwa unashindana na ukinzani wa upepo na hivyo kutmia nishati zaidi. Oanisha mwendo na ukinzani.
8. Kwa sababu na 7 funga vioo na utumie AC badala ya upepo. Sababu ni ukinzani wa upepo na kupoteza upendeleo wa sheria za mwendo-hewa!
..............
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom