Kama hata ukizima ukutani bado linapiga shoti, basi tatizo sio jiko. Tatizo lipo kwenye wiring yako au kuna kifaa kingine cha umeme kinasababisha shoti katika hiyo nyumba aidha katika chumba chako au chumba kingine,(Tatizo kama hili linaitwa EARTH LEAKAGE, yaani kuna muingiliano kati ya LIVE na EARTH).
Solution:
1. Tatuta screwdriver Tester, nenda kwenye soket , zima socket ya jiko chomoa plug ya jiko kama inachomoka kama haichomoki ndenda kwenye soket nyingine yoyote, chomeka tester kwenye EARTH Connector ya socket(lile tundu la juu katikati) angalia kama tester itawaka, endapo itawaka basi ume prove kwamba kuna EARTH LEAKAGE.
2. endapo tester itawaka, basi zima na uchomoe kwenye soket vifaa vyote vya umeme nyumba nzima(vyumba vyote, hata kwa majirani kama wapo). na uendelee kupita earth leakage(rudia hatua namba moja hapo juu ) kama tester haitawaka, basi anza kuchomeka (Kurudishia kwenye socket) kifaa kimoja kimoja huku unaendelea kupima Earth leakage hadi utakapopata kifaa kinachosababisha earth leakage.
3. Kama tester itakuwa inawaka hata baada ya kuchomoa vitu vyote basi tatizo lipo kwenye wiring(Especially darini).
NB: vifaa vinavyoweza kusababisha tatizo hilo ni pamoja na:
- Firidge
- jiko la umeme
- rice cooker
- microwave
- all ovens
- bath heater (All heaters)
- pasi
- na vifaa vyote vyenye plug za pini tatu (3 pins plug)