Msaada: Je, huyu mwalimu hakuelewa somo la ualimu?

Msaada: Je, huyu mwalimu hakuelewa somo la ualimu?

hebu nipe jina la huyo ticha
Hawa maticha wa siku hizi kweli ni tatizo kubwa maana kama huyo ticha sijui alisomea wapi huo ualimu wake nahisi naye atakuwa na vyeti fake kama kile cha yule monitor wa darasa la form six D maana mhh!

Hiyo shule yenu sijui kwa nini imejaa walimu mambumbumbu na wanafunzi wanazidi kuwa mabumbumbu maana hawa muelewi kabisa huyo mwalimu mpya wa shule yenu aisee hasa kwa hivyo viadhabu vyake vya kipumbavu pumbavu , nilipata habari za huyo mwalimu tangu alipo hamia hapo yaani amesababisha sasa hata ufanisi wa shule umeshuka na hadi walimu wenzake nao hawampendi kwa tabia zake hizo za kishetani shetani ingawa nasikia akijua unamchukia utakiona cha mtema kuni na sijui kwanini mkurugenzi anaendelea kumuacha tu huyo mwalimu hapo shuleni.
 
Wanafunzi wa wilaya ya magu full kupenda mvinyo,
Unataka mwalimu mbatizaji awafundishe kutii pasi
Shuruti, walivyo kuwa wakaidi watamwelewa?
 
Natamani kumjua kwa jina moja kwa moja maana bado sijafumbua hayo mafumbo
 
Natamani kumjua kwa jina moja kwa moja maana bado sijafumbua hayo mafumbo
 
Lakini mwalimu huyu huyu kudhihirisha alikua kilaza darasani...kuna watu anawaadhibu tena na kuwaoshea kwenye vyombo vya habari na wengine wakitenda kosa hilo hilo anakaa kimyaaaaa kama hajaona vile!!!

Huyu mwalimu pia ana tetesi za kupata cheti cha tatu kwa njia ya mkato! Ajabu ukiuliza tu ndani ya wiki unakua umetoweka!!
Hapo nimekuelewa sasa,haha wengi hawatoelewa hii fasihi uliotumia,hongera mkuu
 
yan huyo huyo mwalimu ndiye alienifanya mimi nifike hapa yan mpaka na comment hapa ko mpe sifa zakee
 
Hapo zamani baba aliniaminisha kuwa ualimu ni moja ya fani adhimu duniani na ni kazi iliyojaa wito, upendo na uvumilivu kwa wanafunzi, na kuwa moja kati ya somo la msingi linalofanya mwl. awe na moyo huo ni somo la saikolojia, somo hili linamfanya mwl. kuwa mtu mwenye kujaa upendo, uzalendo na moyo wa kujituma huku akiwa amejaa moyo mkubwa wa uvumilivu kwa mwanafuzi na jamii kwa ujumla. pia tuliambiwa kwamba bila kufaulu somo hilo mwanafunzi wa ualimu hakuweza kuhesabika kama ni mwl. hivyo kukosa sifa za kuajiliwa kufundisha wanafunzi.

Kilichonileta hapa ni juu ya tabia ya mwl. wetu aliyepangiwa shuleni kwetu hivi karibuni kama kituo chake kipya cha kazi, tangu afike hapa huyu mwl. hatupumui adhabu zisizo na mpango uwe umewahi au umechelewa lazima tu utachezea kichapo.... kauli zake zimejaa vitisho, ubabe na kejeli mbaya zaidi anatamni hata kila wiki awe zamu yaani ili tu atupe adhabu.


Tangu ahamie hapa shuleni hataki hata walimu/watumishi wengine wapya waje kufanya kazi hapa bali tu ndugu ama rafiki zake wale wanaoongea lugha mama moja wamekuwa wakipewa nafasi za kufanya kazi hapa tena mwenye nafasi zile nzuri. Mbaya zaidi mwl. huyu pia ni mwenyekiti wa chama cha walimu, huko nako mambo ni yale yale walimu wenzie huko wanalia kimyakimya kwa tabia za mwenyekiti wao, wapo waliofukuzwa uanachama kwa kosa tu la kuto msalimia mwenyekiti wao kwa salamu aipendayo hili jambo limemuudhi sana mwenyekiti huyo wa chama cha walimu

Wapo walioacha shule kwa kumwogopa huyu mwl.wapo walioachishwa shule na huyu mwl. halafu anafurahi sana ukimsifia kuwa yeye ni mwl. mzuri na ni mkali kila mwanafunzi anamwogopa yeye tu hapa shule. Na jiuliza huyu mwl. ni kweli alisoma hilo somo ya ualimu na kufauru ili awe na maadili ya ualimu kama baba alivyoniaminisha maana ualimu humfanya mtu awe na staha ya kauli, mstahimilivu, mwenye upendo na wanafunzi maana wanafunzi wanakuwa na tabia mbalimbali ambazo kama mwl. si mvumilivu hawezi kuwafundisha na kueleweka.
Mwalimu J
 
Duh, nimekuelewa mkuu, huyu mwalimu wanafunzi wampige mawe tu akiachwa ataiharibu Shule.
 
Unaweza mezeshwa principles zote za ualimu lakin nafsi yako ya choyo na wivu, vikameza career yako. Jamaa nafsi imemeza taaluma.
 
Unamuogopa hdi umekuj kundik huku huku, ulivyojieeA inaonesha yuko provate school si uhame, kama ni gverment hio inawezeknaje kuwafny watu waache kazi au anaetje dungu zake ilihi yeye ni mgen na si mwajiri
 
Back
Top Bottom