DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Hapo zamani baba aliniaminisha kuwa ualimu ni moja ya fani adhimu duniani na ni kazi iliyojaa wito, upendo na uvumilivu kwa wanafunzi, na kuwa moja kati ya somo la msingi linalofanya mwl. awe na moyo huo ni somo la saikolojia, somo hili linamfanya mwl. kuwa mtu mwenye kujaa upendo, uzalendo na moyo wa kujituma huku akiwa amejaa moyo mkubwa wa uvumilivu kwa mwanafuzi na jamii kwa ujumla. pia tuliambiwa kwamba bila kufaulu somo hilo mwanafunzi wa ualimu hakuweza kuhesabika kama ni mwl. hivyo kukosa sifa za kuajiliwa kufundisha wanafunzi.
Kilichonileta hapa ni juu ya tabia ya mwl. wetu aliyepangiwa shuleni kwetu hivi karibuni kama kituo chake kipya cha kazi, tangu afike hapa huyu mwl. hatupumui adhabu zisizo na mpango uwe umewahi au umechelewa lazima tu utachezea kichapo.... kauli zake zimejaa vitisho, ubabe na kejeli mbaya zaidi anatamni hata kila wiki awe zamu yaani ili tu atupe adhabu.
Tangu ahamie hapa shuleni hataki hata walimu/watumishi wengine wapya waje kufanya kazi hapa bali tu ndugu ama rafiki zake wale wanaoongea lugha mama moja wamekuwa wakipewa nafasi za kufanya kazi hapa tena mwenye nafasi zile nzuri. Mbaya zaidi mwl. huyu pia ni mwenyekiti wa chama cha walimu, huko nako mambo ni yale yale walimu wenzie huko wanalia kimyakimya kwa tabia za mwenyekiti wao, wapo waliofukuzwa uanachama kwa kosa tu la kuto msalimia mwenyekiti wao kwa salamu aipendayo hili jambo limemuudhi sana mwenyekiti huyo wa chama cha walimu
Wapo walioacha shule kwa kumwogopa huyu mwl.wapo walioachishwa shule na huyu mwl. halafu anafurahi sana ukimsifia kuwa yeye ni mwl. mzuri na ni mkali kila mwanafunzi anamwogopa yeye tu hapa shule. Na jiuliza huyu mwl. ni kweli alisoma hilo somo ya ualimu na kufauru ili awe na maadili ya ualimu kama baba alivyoniaminisha maana ualimu humfanya mtu awe na staha ya kauli, mstahimilivu, mwenye upendo na wanafunzi maana wanafunzi wanakuwa na tabia mbalimbali ambazo kama mwl. si mvumilivu hawezi kuwafundisha na kueleweka.