Msaada jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada jamani

Discussion in 'JF Doctor' started by Laura Mkaju, Jun 29, 2011.

 1. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenzenu jamani naomba msaada wenu wana JF, mwanangu ana KIGUGUMIZI KIKALI SANA yaani kadri siku zinavyokwenda ndio kinazidi kuongeza kasi. Naomba mnisaidie nifanyeje?? Ila tatizo hili na ujombani kwao lipo sana sasa sijui ndio amerithi ama??
   
 2. k

  kamili JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 714
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Tatizo la kigugumizi huwaathiri kiasi cha aslimia moja ya watu wazima katika jamii yoyote duniani. Mara nyingi ni tatizo la kurithi. Wanaume wengi huwa na shida hii ukilingainisha na wanawake. Kwa watoto chini ya miaka 5, asilimia 5 huwa na kigugumizi, bahati nzuri kati ya hao wengi kigugumizi hupotea wakati wanapoanza shule ya msingi, na ndio maana idadi hupungua kutoka 5% hadi 1%.
  Tiba nyingi zimejaribiwa bahati mbaya hakuna ambayo imeleta mafanikio ya kutosha.
  Hata hivyo kuna tabia za wazazi ambazo zimeonesha kuzidisha hali hiyo au kuzuia kabisa isipotee, au kuzuia watoto wenye shida hiyo wasipate nafuu. Tabia hizo ni za ukali na kujaribu ama kuwakosoa wanapoongea au kuwasahihisha.
  Kwa hiyo kama mtoto wako ana shida hii usijaribu kumkaripia anapoongea au kumkosoa au kumsahihisha, na unapoona amekosoa jaribu kumweleza polepole. Kama anaongea na anachelewa kumaliza sentence usijaribu kumsaidia kumalizia hiyo sentenci. Ishi naye kama vile hiyo shida haipo na baada ya muda utaona imeisha au imepungua kwa kiasi kikubwa,
   
 3. k

  kamili JF-Expert Member

  #3

Loading...