Nawasalim wana MMU,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa MMU na nimepata kujifunza mambo mengi sana lakini kuna jambo limenitokea naombeni ushauri wenu.
Kwa sasa ninaishi Dar nimetokea kumpenda mdada mmoja yuko Shinyanga (ndiko anakoishi), kwa sasa yapata miezi saba tokea tujuane (tulikutana Shinyanga nilienda kusalimia ndugu); mimi ninafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi (temporary) na huyu dada anayo saloon ya kike hapo shinyanga mjini.
Tatizo langu linakuja kwenye suala la pesa; kwani kila mara nikipokea simu yake baada ya kujuliana hali anaomba pesa mara shampuu na mafuta mengine zimeisha za saloon mara nimtumie pesa za matumizi mara wateja wamepungua sana anadaiwa kodi la nyuma (saloon).
Yote hayo yaweza kua sahihi lakini linapokuja suala la mafuta na shampuu huwa nashindwa kuelewa make haviwezi kuisha bila kuingiza pesa kwani zinatumika kwa wateja, pili kwa nini anapiga simu akiwa na shida la pesa tu? yungali tuko wachumba?
Mimi nilishamweleza hali halisi ya kipato changu na msaada ambayo twaweza kusaidiana, lakini niliona kama hajaelewa make alikua akipiga simu analalamika mithili ya mtu anaelia kitu ambacho sipendezwinayo. Kutokana na hiyo hali nilipanga safari adi Shinyanga wiki mbili zilizopita wala sikuona hali mbaya sana kwenye saloon yake, kurudi Dar baada ya wiki moja ameanza tena mara anataka kuleta mfanyakazi anejua kusuka vizuri kwa hiyo nimsaidie kulipa mara amepata chuo uku Dar kuna kozi anataka kuja kusoma nimchangie,,jamani!
Naombeni ushahuri huyu mdada anayo nia nzuri na mahusiano YETU? au anataka kula PESA na kusepa?
MUHIMU: SIJAWAI KUFANYA NAE MAPENZI