Msaada jamani njia panda hapa

Msaada jamani njia panda hapa

Mastamind

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
1,316
Reaction score
840
Yule Mke wangu aliyenitoroka miezi miwili sasa bila kwao wala mimi kuju aliko, majuzi nilipiga simu kwa mama yake mdogo kutaka kujua kama walishampata, bahati mbaya kwangu alipopokea alinipa habari mbaya kwangu za kuwa tayari ameshachumbiwa, sikuwa na maelezo zaidi ya kukata simu na kumpigia mama yake mzazi kuthibitisha hilo, cha ajabu mama yake hakupokea licha ya kupiga zaidi ya mara moja kitendo ambacho haikua kawaida yake, baada ya hapo jibu likaja anaogopa kuthibitisha hilo nikaamua kuanza kuzifuta namba zote za ndugu yake pamoja na wazazi wake, hapo sasa nikaanza kujikita vilivyo kwenye penzi jipya la mwalimu ambaye anajua maisha ni nini ambaye tuko mikoa tofauti ila tushado sana pasaka alikuja mwenywe nikajiridhisha niya yake thabiti ya kuishi nami.

Sasa juzi nimekua nikipata simu mpya ambayo sikuifahamu ni nani sana zaidi anajitambulisha kwa jina la G ambaye anasema anaebipu kwa simu yake ni yule mke wangu aliyetoroka leo wamenitumia sms wakanambia niwapigie, kuongea naye anadai yuko Mara alipelekwa na mama mdogo wake, kumuuliza kwa nini simu zake kaziacha kwao Mwz anasema mama yake alimnyang'anya bila sababu, nikamuuliza anataka nini sasa kunibip hajibu, nikamueleza kua nimeambiwa ashachumbiwa na ni mke wa mtu sasa ila amekataa katu.
akaniuliza niko wapi nikamjibu Dar nafanya interview alizoniacha nimeombea kazi, Baada ya hapo tukaagana ila ikanigusa sana ikabidi niitafute sana namba ya maza wake nimtege nae nione majibu yake, bahati nilimpata akanijibu kweli binti yake kachumbiwa na yuko Arusha tofauti nawanae alivyonambia
1.Sasa wajameni nashindwa kuelewa huyu mwanamke anataka nini tena kwangu?
2.Nani muongo kati ya mama vs mwanae?
3.Nina mke mpya mwenye kazi na nia ya maisha na habari yakutorokwa na mke huyo anayo na anawacwac nae mkubwa, Sasa hapa nilikua nawaza aweke profile picha yetu mimi na yeye FB ili yule aliyetoroka akiona asinisumbue licha ya kumpenda sana mpaka sasa sijaona mbadala kwa kweli, she is so beautiful in nature
WAUNGWANA MNISAIDIE,!!
 
We ukiisha ona Hivyo ujue !

Ndugu zake hawakupendi !
Tulia tu Zao jipya hilo !

:msela:
 
Wewe huyo mke au mzinz mwenzako? hivi unafahamu neno mke linathamani sana mbele ya Mungu na Wanadamu,Halafu Facebook ndo inaweza ikakuamulia kumbe? Maana yake wewe unamuogopa huyo unayedai ni mke na mke siku zote hatoroshwi kama ameamua kutoroka mwenyewe kwa akili yake sawa na huyo watakaye mkuta naye ana hali mbaya ndo maana nimekuambia Mke anathamani sana huyo wako siyo mke
 
Wewe lafa nini? Jengo linaungua nawe umefanikiwa kutoka salama, sasa unataka kuirudia saa ya ukutani? Ningekua karibu yako ni vibao tuu. Concentrate na kilichokuleta mjini (kazi yako right?) Ukirudi kwenye hiyo familia ya vichaa na ww utakua Psycho.
 
Wewe mwenyewe una kigeugeu!mbele hausimami,nyuma haukai! Asa kama una demu mwngne si ukaushe..nini kutaka vya zaman?au ndo mav ya kale hayanuki?hebu jipange kwa hili vngnevyo yatakushnda
 
Hakunagga replacement ya mpenzi jamani,, wa zamani ni mkali na ana haiba ya uanamke sana,, kila m1 humu akimuona lazima acmamishe mnara hata km dem mwenzie, nilikua najidaia sn asee
 
duniani kuna mambo
Hakunagga replacement ya
mpenzi jamani,, wa zamani ni mkali na ana haiba ya uanamke sana,, kila
m1 humu akimuona lazima acmamishe mnara hata km dem mwenzie, nilikua
najidaia sn asee
 
Hakunagga replacement ya mpenzi jamani,, wa zamani ni mkali na ana haiba ya uanamke sana,, kila m1 humu akimuona lazima acmamishe mnara hata km dem mwenzie, nilikua najidaia sn asee

kweli ushalogwa weye yaan kaenda huko kagongeeeesha weee na bado unataka duh yaan kwa kawaida tetesi tu unatakiwa umteme sasa wa kwako kasepa kabisa
 
ungekutana na mimi nisie na account fb picha ungebandiks usoni??

hivi ndugu mbona km hujisomi?hebu fumbua macho kwanza m naona huna maamuz kbs...
 
Hakunagga replacement ya mpenzi jamani,, wa zamani ni mkali na ana haiba ya uanamke sana,, kila m1 humu akimuona lazima acmamishe mnara hata km dem mwenzie, nilikua najidaia sn asee

wake up hakuna kizuri hapo km kashindwa kukuthamini...jisifie km anaijua thaman yako na angeijua asingeenda kwa mwenzio
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom