Msaada: Huyu Binti haelewi nia ya baba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Huyu Binti haelewi nia ya baba yake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eeka Mangi, Dec 24, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wana JF
  Habari za masiku. Kuna binti mmoja rafiki yangu ( msinishambulie sio mpenzi wangu ni rafiki tu basi) amekwisha mpata wake na wameamua kuishi pamoja. Binti ni muislamu na kijana mkatoliki. Kimsingi wamekwisha kukubaliana kuwa mke na mme. Binti alimpa baba yake taarifa kitambo sana. Baba alileta ubishi kwa kuzingatia tofauti ya udini. Binti alisimamia msimamo wake na pia aliahidi kuwa hatobadilisha dini na kuwa mkiristu. Baba alikubaliana na binti yake. Tarehe zikasonga mbele na binti akawa anamwambia baba yake kuwa upande wa kiumeni wanataka kuja kujitambulisha. Danadana zikaanzia hapo. Mara keshokutwa mara mtondogoo. Binti alivyoona ubabaishaji unazidi akamwambia kuwa mume wake mtarajiwa anataka kufungoa harusi mapema mwakani ( Yaani January 2012 mwanzoni). Binti akaweka msimamo kuwa hatohitaji makuu ila anaomba baraka zake. Mzee akajitutumua akamwambia binti kuwa hawezi kuolewa mpaka amfanyie send off! Binti akamtii baba yake! Vikao vikaanza vya hapa na pale! Tarehe zimefika mzee anaulizwa anasema kuwa anazo ka shs laki nne tu! Kuwa rafiki zake hawakumchangia na mbaya zaidi naye kakimbilia kwa mkewe Nairobi. Na hata hiyo laki nne anayo yeye. Binti amebakia njia panda anaomba ushauri wenu afanyeje?
  Anasubiri ushauri wenu.
   
 2. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  No msaada? Send off date 27th December 11. Kabinti ka watu kanachanganyikiwa. Na mbaya ameomba hata ruksa kazini kuwa wanamsend off tarehe hiyo.
   
 3. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Sasa kama baba kakimbia na ile laki nne..
  Anyway, send off sio muhimu, cha muhimu harusi.
   
 4. s

  sibuga Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hayo magumu sana.
  Afanye awezavyo kumubembeleza mamaye
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Baba hataki ndiyo ndoa, analazimika kufanya kwa shingo upande ndio maana anapiga dana dana.
  Ni mzazi gani atakayepewa taarifa na binti yake juu ya send off apige dana dana?
  Hilo ni jambo la kheri!
   
 6. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sasa msaada wa nini? Anaolewa baba yake au yeye? Si mwanzo walitaka kufanya mambo bila send off sasa nini kinazuia hapo. Wao waende zao wakafunge ndoa waanze kutafuta watoto. Hata siku moja mzazi hawezi kukomplketi maisha yangu kwa imani yake. Kuna mambo ya kuelekezana lkn sio yanayohusisha imani kwani kila mtu na kaburi lake
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  ahairishe hiyo send off, aamue kufunga ndoa bila send off. Hayo ni mambo ya kizungu, wao waamue kwenda kanisani kukamilisha hiyo maneno. Tena ningekuwa mimi hakuna sherehe hapo ni ndoa kimyakimya then honeymoon kiaina maisha yanasonga mbele nchi yenyewe isha liwa hii macomplication ya kazi gani bwana, agrrrrrrrr!
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Msaada wako afanye nini ukizingatia kuwa hata mialiko keshaanza kutoa. Wenzake watamfikiria nini akiamua kujiondokea kimya kimya!
   
 9. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  sendoff kitu gani?

  akafunge ndoa, maisha ya amani, furaha na mapenzi ndo ya msingi sendoff haimuongezei wala kumpunguzia chochote zaidi ya stress na madeni. mwambie akafunge ndoa aachane na masendoff
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Hakuna ndoa hapo Kiislaam, waende tu wakafanye zinaa.
   
 11. Mnyamwezi wa Urambo

  Mnyamwezi wa Urambo JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani mkristo anaruhusiwa kumuoa/kuolewa na muislam ki-imani yake?je muislam anaruhusiwa kumuoa/kuolewa na mkristo kwa imani yake?Sasa hiyo wanayoiita ndoa imetokea wapi?mimi nawashauri waendelee tu kubwengana haina haja ya kupoteza muda wala fedha kwa hicho kiini macho cha harusi then watajua cha kujibu siku ya mwisho!!
   
 12. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 624
  Trophy Points: 280
  Haswa ndicho kilichomkibiza mzee!! FF jaribu kupata picha hii mwanao binti anakuletea hadithi kama hii, gozi laweza kukimbilia Mombasa kuepuka fedheha, lakini huyo baba anampenda mwanae sema hiyo ndoa imemshinda!
   
 13. sambenet

  sambenet Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeshanisemea FF, ila kama Huyo Dada hajali dini yake na hafuati mafundisho na yuko tayari siku ya siku akajibu hilo Swala Mbele ya muumba wake basi muache wacha aendelee tu. Halkadhalika na huyo kaka je Jee dini yake inamruhusu kufanya hivyo.

  mabinti na Vijana wa kiume wacheni kuwakwaza wazee wenu kwa ishu kama hizi, Huyo mzee kakaimbia kwani hawezi kushuhudia hayo yakitokea na hataki kuwa yeye ahusike na kutoa Idhini ya hio ndoa pia.

   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Imeshawahi kutokea hali inayofanana na hiyo hiyo two times kwa watu ninaowafahamu. Wa kwanza baada ya baba kukataa mwanae asiolewe kila wakati anaweka ngumu, ikaja kubainika kuwa kumbe baba alikuwa anakula mayai yake mwenyewe (serious: alikuwa analala na mwanaye wa kumzaa), ilipobainika kuwa anazuia ndoa kwa sababu hiyo hali ya hewa ilichafuka!
  Wa pili ilikuwa katika mazingira kama hayohayo, lakini mwisho wa siku ikaja kubainika kuwa kumbe baba alikuwa na uhusiano wa kifirauni na mkwe wake yaani yule aliyekuwa anataka kumuoa mtoto wake na hata huyo 'mkwe' alimuona huyo binti na kumpenda wakati wakiwa na uhusiano wa kifirauni na baba wa mtoto! Dunia imeharibika hii!
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  pole yake huyo binti
  anachanganyikiwa nini, kwani keshaalika watu?
  Aolewe tu kimya kimya
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Hapa sikai hata mkinipa kiti ninywe chai, ntakunywa wima!
   
 17. w

  wisenhero New Member

  #17
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 24, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  katika maisha mapenzi sio kila kitu, baada ya muda fulani kupita kama mlilazimisha ndoa bila ya ridhaa ya mmoja kati ya wadau wakuu au bila ya kufata utaratibu unaokubalika mtajikuta mnasutana wenyewe na hiyo ndoa haitadumu
   
 18. i

  iMind JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,908
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hata harusi siyo muhimu. cha muhimu ni kuishi pamoja as a family.
   
Loading...