Msaada: Hedhi mfululizo/over bleeding

Msaada: Hedhi mfululizo/over bleeding

Full charge

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
1,711
Reaction score
1,663
Natumai mu wazima,

Mpenzi wangu akiingia kwenye mzunguko wa hedhi anatokwa damu nyingi sana hadi hufikia mpaka kuongezewa damu. Hali hii ikianza yaweza kuchukua hadi wiki 3 bila kukata, nampenda sana japo hashiki mimba.

Watalaamu nisaidie nini tatizo la hicho kitu pia nini kifanyike ili awe kawaida.

Asante.
 
Anatumia uzazi wa mpango wowote?? umpeleka hospital??
 
Mpe pole sana
Kwani ulishawahi sikia kitu kinaitwa mchujo
 
Ok tigo itaacha.Naomba msaada mkuu
Tatizo linaitwa Haemophilia

Haemophilia is a mostly inherited genetic disorder that impairs the body's ability to make blood clots, a process needed to stop bleeding. This results in people bleeding for a longer time after an injury, easy bruising, and an increased risk of bleeding inside joints or the brain

Mpeleke hospital haraka
 
Natumai mu wazima....

Pole ndugu,
Mambo matatu naweza kuyahusisha na tatizo analolipata mwenzio:

1: Inaweza kuwa ni mfumo wa vichocheo vya mwli/hormones haujakaa sawa.

2: Mfumo wa kimaumbile wa mji wa mimba ukawa na kasoro.

3: Mfumo wa kuganda damu ukawa una kasoro.

Ni vyema kumhusisha daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama juu ya hili, lakini daktari bingwa wa mfumo wa damu pia kama hakutakuwa na ufanisi kwa huyu wa kwanza.
 
Mimi nilliambiwa sijui inaitwa Polystitic ovarian Syndrome(kama sikosei)...huku hutapata majibu, nenda kwa mtaalamu wa magonjwa ya wanawake
 
Mimi nilliambiwa sijui inaitwa Polystitic ovarian Syndrome(kama sikosei)...huku hutapata majibu, nenda kwa mtaalamu wa magonjwa ya wanawake

Kuna issues nyingi zinahusika hapo ukishataja abnormal uterine bleeding. Ni suala la nice step wise approach ili upangue moja baada ya nyingine. La sivyo u get confused au gharama iwe kubwa kwa mgonjwa
 
Tatizo linaitwa Haemophilia

Haemophilia is a mostly inherited genetic disorder that impairs the body's ability to make blood clots, a process needed to stop bleeding. This results in people bleeding for a longer time after an injury, easy bruising, and an increased risk of bleeding inside joints or the brain

Mpeleke hospital haraka
Asant mkuu
 
Natumai mu wazima,

Mpenzi wangu akiingia kwenye mzunguko wa hedhi anatokwa damu nyingi sana hadi hufikia mpaka kuongezewa damu. Hali hii ikianza yaweza kuchukua hadi wiki 3 bila kukata, nampenda sana japo hashiki mimba.

Watalaamu nisaidie nini tatizo la hicho kitu pia nini kifanyike ili awe kawaida.

Asante.
Anatumia njia gan ya uzazi?

Na anapata Maumiv ya mgongo yanayoshuka kiunon na miguu kuuma??Kukoswa choo?? Tumbo la chin kuuma ? Maumivu wakati wa kugongana ? Maumivu makali wakati wa damu ?

Mpeleke hosp akafanye

Ultrasound , Thyroid function test, E.Biopsy , n.k kutegemea na dalili nyinginezo.

Tiba yake itategemea na kisababishi, pamoja na sababu nyingnezo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom