Unaenda kuifanyia nini hio laptop? Kwa matumizi ya kawaida inatosha kabisa
Mkuu kuna
Asus core i3 Intel inside, ram 4GB
full windows touch support with 10 touch points
Vipi Vipi Nzuri kwa matumizi gani nishauri
Kaka matumizi niambie wewe unataka uitumie vp na ni i3 ipi? Zipo nyingi
nimepitia hio website hizi hapa laptop kali
1. asus yenye nvidia gtx760m na i7 4700hq. hii laptop chochote utachotupia itafanya ila bei ni dola 650 (around 1,300,000)
ASUS N56JR-MH71 Notebook Intel Core i7 4700HQ 2 40GHz 16GB Memory 750GB HDD NVIDIA GeForce GTX 760M 2GB 15 6 Windows 8 64-bit
2.hp pavilion yenye nvidia gtx 740m na i5 4200u hii ni dola 380 (around 760,000)
HP Pavilion TouchSmart 14-N033tx Ultrabook 4GB RAM 500GB HDD 24GB SSD 2GB Nvidia 740M Graphics
3.hp pavilion kama namba 2 ila yenyewe ina i7 4500u kwa dola 400 (around 800,000)
hp pavilion 14 core i7 750gb 4gb ram 2gb nvidia dvd Window 8
4. acer v3 yenye i7 (isio na jina) ila ni quad. probably ni 3rd generation kende hii ni dola 500 ndani ya budget yako na kama ni i7 quad itakufaa
Acer V3-571 Quad Core i7 4GB 500GB Windows 8 Laptop in Black
on budget
kuna hii toshiba kwa dola 150 ina i5 3230m ambayo ni processor nzuri
Toshiba Satellite Pro C50-A-137 Intel Core i5-3230M 4GB 500GB 15 6 Windows 7 Pro Windows 8 Pro
ina uhakika gani hii website?
Daaa basi tushakosa mambo mkuu
Sijajua ni i3 gani Ila ni ASUS LAPTOP TOUCH SCREEN
i3 utafanya mambo yote ya kawaida hadi games ndogo ndogo kama pes, fifa nk ila kwenye games kubwa kubwa itakuwa slow na hasa kama haina gpu nzuri.
Pia inabidi uijue i3 ipi maana vipo vimeo pia.
Ila kama ina touch na win 8 itakuwa ni nzuri
Wameniambia wanadeliver Tanzania through Fedex or DHL within 3days, free delivery. Wenye uzoefu na biashara ya mitandao wanisaidie hapa
Yap Ina windows 8
Sio mbaya matumizi yote ya kawaida itafanya fresh tu.
Gpu muhimu tena sana kwenye games, elewa concept hii itakusaidia kufanya maamuzi.
-kila cpu inakuja na gpu yake ya ndani
-si dedicated graphics zote zina nguvu kushinda gpu zinazokuja na cpu
Hivyo unaweza nunua laptop yenye gpu ya nvidia ikawa kimeo kushinda hata laptop isio na dedicated gpu.
Kujua gpu nzuri ya nvidia unatakiwa uangalie namba ya yapili (yakatikati) hio ndio inamaanisha power
Mfano angalia hizi score za benchmark
Nvidia gtx 275 = 1215
Nvidia gt 610 = 356
Kikawaida ukitajiwa 610 na 275 utasema 610 ni kubwa ila kwenye gpu mambo yapo tofauti 275 ni kubwa sababu namba ya katikati ni kubwa namba ya mwanzo ni version tu.
Hivyo angalia hio gpu ya nvidia kama ni
X10
X20
X30
*x inaweza kuwa namba yoyote
Achana nayo ila kama namba ya kati ni 4 kupanda juu ni nzuri, au kwa uhakika zaidi unaweza ileta humu tukaiangalia.
Kwenye gpu zinazokuja na processor tafuta atleast hd 4600 au intel iris pro ndio utaenjoy game kwa 720p
Safi sana mkuu. Nimepanua uelewa wangu kwenye GPUs. I once had an nvidia nvs 3100 gpu ilikua poa kwenye games za kawaida, though after sometime ikazingua. Kumbe inawezekana na yenyewe ni ndogo.
Yah ni ya zamani, ila hizo zinaitwa quadro series zenyewe zilitengenezwa kwa ajili ya kueditia video na driver zake zimekuwa optimized kwa kazi hio. Japo unaweza cheza games ila hazina nguvu sana kwenye games
vip kuhusu nvidia sometimes nakuta GTX,GT, GEFORCE