Msaada: Gono isiyopona kikamilifu

Ceftriaxone ni nzuri sana lbd kama ukumaliza dose yyte kati ya hizo ulizopewa
Tafuta hospital nyingine upate matibabu zaid. Na utulizane wee kaa kichwa juu juu kama beberu
 
Acha utani nenda kaonane na watu wakienyeji Hawa wamama inaisha bro wamtu alikuwa na Ile mbaya sana unatoa usaha na harufu hadi anakimbiwa nainamuwasha kila akioqta mkojo inauma kitoka analia sana akapona kabisa Sasa yupo tu.


Ila Vaa kondom haya yote yasingekukuta hiyo ni ngono zembeee
 
Usitumie dawa bila kupima. Nenda hospital inayoeleweka, ufanye kipimo cha culture and sensitivity. Wanaotesha wadudu wanatest na dawa tofautitofauti kuona ni ipi inaua hao wadudu ndiyo unaanza dozi.
 
Usiende kwenye dawa za kienyeji. Nenda hospital.
 
Pole sana mzee piga dose hiyo lazima upone

Cefixime 400mg start
Azithromycin 1g start
Doxycycline 100mg bd 5/7
Vivian tbs 1 tds 3/7
 
Pole sana mzee piga dose hiyo lazima upone

Cefixime 400mg start
Azithromycin 1g start
Doxycycline 100mg bd 5/7
Vivian tbs 1 tds 3/7
nje ya mada
mapunye yananisumbua nimejaribu dawa nyingi lakini bado
sijawahi ugua huu ugonjwa yaani unanifanya mnyonge sana naomba anayejua dawa anisaidie
 
Naomba tusaidiane hapa, hivi kwanini watu wengi wanaumwa magonjwa serious kabisa na hawataki kwenda hospitali wananunua dawa kwenye maduka ya mtaani?
Watu wanaona aibu.
 
Ghonorhea,kwa bodaboda limetamalaki,na wao wanaenda wanakula wake za watu,hao wake za watu wanaenda wanawapatia waume zao,waume zao,wanaenda kuwapatia michepuko yao,the circle is endless kwani wale wa 'kula tunda kimasihara' wakikutana na mmama au dada,hawatumii kondom,hali inakua mbaya.
Jamani tutumie kondom,hiyo gono mbali na madhara ya hapohapo,kuna madhara ya baadae,nadhani wale watu wanaoendaga urology,wanaonaga wale watu wanaowekewaga mipira ya kukojoloea,inasemekana gono likipona,huacha makovu kwenye mrija wa kukojolea,baadae yale makovu huvimba.
Hata kama huogopi gono,jamani kuna VVU,kama navyo huogopi,Kuna hepatitis B ni mbaya sana.
Anayway,tujijali,kupunguza usumbufu kwa ndugu na jamaa,pale tunapougua.
 
leo ni tarehe 1/12/2022, twendeni tukapime vvu.
kupima ni buree hutoi hata shilingi.
ushauri nasaha bureee.
Umenikumbusha kuna jamaa zangu nafanya nao kazi,wakisikia kesho watu wa afya watakuja kwa ajili ya kupimwa UKIMWI huwa hawaji kabisa kazini...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…