Ahsante sana mkuu, hilo mimi pia nililliona wenzetu wajanja sana, kwao kuna masoko yani demand is very high tena sana na kama hawapeleki kwao wanapeleka nchi za jirani tatizo sisi hatuwazi nje ya box, mkuu yani my bro ambaye yupo UK amenitia hamasa sana hii kitu lazima niifanye, hapa nipo kukusanya tafiti mpaka kieleweke,Mkuu,
Kuna mambo mengi ya kuendelea kujiuliza na kufanya utafiti wa kutosha.
Mfano: Kuna kampuni/jamaa wanakuja nchini kutokea nje ya nchi na sanasana ni Wahindi, wanaweka kambi humu nchini na hasa mashambani huko, wananunua mazao kama Ufuta, Choroko, Mbaazi, Dengu na mazao mengine ya jamii ya Mikundekunde, wanapopeleka huwa hatupajui na hakuna anayejishughulisha kujua huwa wanayapeleka wapi, kwa kifupi hapa namaanisha MASOKO.
Kama bidhaa hizi zipo hapa nchini kwetu kwanini sisi tunaishia tu kuwauzia hawa wanaotulangua, ina maana sisi hatuwezi kupeleka huko wanapopeleka wao.
Hebu tufunguke vijana. Na kwa sasa nina imani na serikali tulonayo.
Sasa kama hakuna demand mbona South wanahangaika kupeleka unga watanzania bana, tulia kama hujuwi, mtu ambaye amenilisha ili wazo ni kaka yangu kabisa hawezi kuniongopea na ili iweje sasa anidanganye pia pesa tunayo vuna ni ya mimi na bro, pita kimya kimya sio lazima uchangia maana kuna watu mpo kwajili ya kupinga kila kitu.Mimi sidhani kama kuna market ya unga wa sembe England,wazungu hawatumii hii kitu- South Africa wanapeleka sembe uk,trade name Iwisa,Azam nae anapeleka lakini naona ni quantity ndogo sana
Sawa kabisa mkuu, nashangaa yeye anapingana nami wakati mimi nataka kujikwamua kichumi kauzibe sijuwi kanini, hasara nitapata mimi yeye kakazania hakuna masoko..Lakini mleta mada kasema kuna kaka yake huko ndo aliyemwambia kuwa demand ni kubwa mahali alipo.
Funguka Kamanda, kama una details ndo tunazihitaji hapa. Kwani sisi hatuwezi kukomaa kuzifukuzia hizo fursa huko UK!!?
Tiririka hapa mkuu .
Aisehhh hata mimi simuelewi kabisaJackline unatuchanganya sasa, mwanzoni umesema Wazungu hawatumii hiyo kitu na ukadai hata Azam na kutoka South Africa wanapeleka kwa kiwango kidogo sana, sasa hivi unasema Sembe imejaa supermarkets, so which is which maana kama Sembe ni nyingi kwenye hizo supermarkets unazosema maana yake uhitaji ni mkubwa. It's just a simple science.
Sina details nyingi. Ila kama unaweza kupata watu wanaofanyakazi kwenye kampuni za ukaguzi wa mizigo bandarini, hawa watakuwa na info za kutosha. Sisi kufanya biashara hii inawezekana kabisa ukishapata soko na mtaji.
Mkuu kwenye swala la usafirishaji nimemuona mdau, wanajiita Premier freight agent naona hii team wanaweza kutupa info za kutosha namna ya kusafirisha hizi nafaka nje ya nchi...Hakuna zaidi ya meli. Ukitaka kutumia ndege ni gharama kidogo labda itokee unatuma perishable products.
Kumbuka ukishafikisha mzigo bandarini na umeshakabidhi kwenye meli huo mzigo sio wako tena unless itokee issue ya kuwa chini ya specifications au kiwango.
Ila kama mzigo umeibiwa au kupotea mwenye meli ambaye ana bima ataulipa huo mzigo.
Nashukuru sana kwa mawazo kuntu mkuu,Mawazo na malengo mazuri. Zingatia yafuatayo kabla ya kufikiria mtaji.
Umoja wa Ulaya unafanya kazi kwa viwango na afya ya jamii kwao ni sehemu ya kipaumbele hivyo kwanza soma sheria ya uingizaji vyakula katika nchi hizi.
Ukijiridhisha na uwezo wako wa kutimiza vigezo hivyo nadhani mengine hayo yatakuwa historia. By the way, unga juzi kati nilinunua kilo moja 6€ sawa na 14,000/= kama sijakosea alafu hauna ladha kama unga wetu.
Inawezekana ukiamua
Mimi niko Spain,lakini UK kwa sana,anyway all the best,tunaomba tuu usibanie feedbackWewe upo nchi gani
Mkuu kwenye swala la usafirishaji nimemuona mdau, wanajiita Premier freight agent naona hii team wanaweza kutupa info za kutosha namna ya kusafirisha hizi nafaka nje ya nchi...
[emoji120] [emoji120] much respect mkuu, bavaria kanifungua macho na wachangiaji wengine pia, mimi naamini hakuna linalo shindikana kama tunatia nia katika kila jambo mkuu, hapa jf kwa kupitia huu uzinimepata info ambazo kwa asilimia kubwa zitanisaidia sana, na mfanyabiashara makini nilazima Preliminary stage inakuwa ni yakufanya tafiti...Mtoa mada nakupongeza sana kwa kuwa una mtizamo wa mbali kimaisha na kimaendeleio utafanikiwa sana ,Kuna watu humu wameonyesha kukukatisha tamaa, lakini nampongeza sana Bavaria kwa kujitolea kufungua njia na kukuelekeza akiwa free without cost,Bavaria your a real entrepreneurship and hero of Tanzania development
Wazo zuri sana kaka...nakutakia mafanikio. Nilikaa dubai kipindi flani. Wakati naenda nilipakia Kilo 40 za unga wa ugali, mchele na maharage. Kule nako unga ambao tumezoea huku ni adimu. Kuna unga wa India ambao ni wa njano flani naona wa Tz hawaupendi.
Aisehhhh kumbe fursa zipo all over the world, south Africa, Nigeria... Mimi naona uzi huu tafiti hizi zitawasaidia wengi kufanya hii biashara, watanzania tuache kuwaza ndani ya box au sio mkuu maana fursa kibao
Okey kwanza ninawashukuru wachangiaji wote waliopita kwenye uzi na kutoa mawazo yao nilikuwa offline kidogo, ngoja nianze kujibu, nitaanziana mkuu hapa...
Premierfreights team nashukuru kwa kunifanya kuona zoezi langu litakuwa rahisi hasa kwenye swala la usafirishaji maana katika vitu vilinifanya kuwaza ni namna ya kusafirisha mzigo,
Kabla ya yote ningependa kujuwa PREMIERFREIGHT ni wakina nani,mnapatikanika wapi hapa Tanzania, how reliabe are you? mnautaratibu gani mtu akitaka kusafirisha mizigo yake eg nafaka hususani nje ya nchi, na je mnatoa bima ama warrant kwa mzigo naosafirisha, na je gharama zenu zikoje, hebu tuanzie hapo,
Kwa upande wangu mzigo utatoka hapa utapokelewa na ndugu yangu destination ni UK_Middlesbrough...
Mahindi sio unga mkuu,Mkuu demand ni kubwa sana yani hatari, napata wasiwasi kama serikali itafungua milango, maana nakumbuka kuna kipindi serikali ilipiga marufuku kusafirisha mazao nje ya nchi.... Sasa sijajuwa sahivi utaratibu ukoje