Msaada Chuo kizuri kusoma BBA hapa Tanzania
Ipo hivi mkuu BBA yani ina specialization yani kuna BBA in MARKETING, ACCOUNT AU HR
Sasa basi kwa ushauri wangu mimi naomba asome BBA general isiyo na specialization kwa sababu zifuatazo
BBA in MARKETING maana yake kashajifunga na hatoweza kudeal na mambo tofauti na hayo kama HR
BBA in ACCOUNT hii ni nzuri sana ila ina mbadala wake kama ifuatavyo mtu aliyemaliza ACCOUNTS hatambuliki na bodi ya wahasibu kama hajasajiliwa na bodi na kufanya ile mitihani ila faida yao ni kwamba wanafutiwa masomo yote ya level ya foundation ataanzia level ya pili ya intermediate na kumalizia final stage ambayo ni professional
kwanini nikasema ina mbadala mtu aliyesoma BBA ile general kwa kuwa kuna module za ACCOUNTS kuna masomo pia huwa wanafutiwa kabisa lakini kwa level ya foundation na yatabakia 3 mfano kama QM, BUSINESS LAW yote anafutiwa hivyo akikomaa vizuri atamalizana na foundation na kuendelea level inayofuata
BBA in HR nayo ni vile vile hamna wigo mpana zaidi ya hiyo
ila sasa BBA general kwa miaka 3 inameza kila kitu hapo kwa Ukubwa wake maana yake itameza HR,MARKETING na ACCOUNTS
Ndio maana nikasema BBA general ni course itakayomfaa kwa haraka haraka chuo wanachotoa hii course ni NIT japo naamnini kuna vyuo vingine
Tukirejea matangazo ya kazi mfano wakitaka HR wanasema kabisa walisoma HR,BBA, public administration
wakitoa tangazo la kazi la marketing Manager hutokuja kusikia wanasema wanahitaji mtu aliyesoma HR
Wakitafuta Accountant watasema BAF,ACCOUNTS NA BBA tena huyo wa BBA akiamua anaitafuta CPA anatulia zake maana yake anapata wigo mpana wa kukaa hizo sehemu zote 3