Wasalaam ndugu zangu.
Aiseh haya maisha akili ni kitu ambacho hupaswi kukosa kabisa.
Kifupi niko na pikipiki tatu zote za mkataba. Kuna pikipiki moja ina mwezi wa tatu sasa, lakini imekumbwa na hii shida.
Huyu nilomkabidhi kuendesha alikua mzito kurejesha pesa na sababu kuu aliugua kwa muda karibu siku 20, lakini pikipiki alidai kuwa aliipark lakini ukweli ni kua ilikua inapiga kazi, namimi sikutaka kuharibu mipango yake ukiangalia alikua mrejeshaji mzuri wa pesa.
Majuzi akaomba kusitisha mkataba maana deni lilikua kubwa. Tuliandikishana marejesho ya deni. Siku ya juzi nilipokua nafanya service ili nimakabidhi boda mwingine ndo nikagundua kuwa engine imewekewa chumvi. Taratibu za kisheria zikachukua mkondo wake na jamaa yuko ndani (maisha yake ni magumu, sioni uwezekano wa kulipwa gharama za matengenezo bali naiona jela mbele yake tu endapo nitaamua kusimamia kidete).
NAOMBA MWONGOZO JINSI NINAVYOWEZA KUTOA HILI TATIZO NA PIKIPIKI IENDELEE KUFANYA KAZI KAMA KAWAIDA.
NB.
Wale wataosema ni biashara kichaa, niwambie tu hii biashara kwangu mimi inalipa na imenitengenezea faida.
Pikipiki inatembea vyema tu, shida ni hili tatizo.
Nawasilisha