Msaada: Basi la haraka kutoka Dar-Kilimanjaro

Msaada: Basi la haraka kutoka Dar-Kilimanjaro

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,785
Habari wandugu.

Kama kichwa cha habari kinavyosomeka naomba msaada kwa anayefahamu mabasi mazuri na yanayowahi kufika Kilimanjaro kwa uharaka kwani kuna shughuli nataka kuwahi majira ya saa 9 alasiri.

Gari litakaloweza kufika Kilimanjaro majira ya saa 8-9 alasiri litanifaa sana.

Wale wazoefu wa route hii nasubiria ushauri wenu ili kesho niwahi Ubungo kukata tiketi.

Natanguliza shukrani.
 
Kamata Kilimanjaro au dar express zinazoenda Nairobi utawahi
 
Panda Saibaba ya nairobi au dar express ya nairobi au karatu na kama unaweza vumilia mwendo rafu panda modern ya nairobi saa 8 goma linakatiza sakina
 
Panda ungo kufumba na kufumbua umeshafika salama, mabasi utapata ajali bure.
 
Panda Saibaba ya nairobi au dar express ya nairobi au karatu na kama unaweza vumilia mwendo rafu panda modern ya nairobi saa 8 goma linakatiza sakina

Kuna jamaa alishawahi panda kwenda chugga akaambiwa alipe nauli ya nairobi kwamba hakuna nauli ya njiani
 
Ushauri uliopewa ni mzur wa kupanda gari za nairobi , Modern, da express au Saibaba ila kama hujali confotability unaweza kupanda pia Ngorika .
 
Kamata Kilimanjaro au dar express zinazoenda Nairobi utawahi

sio kama nawapigia promo bali wako vema ... nawazungumzia ngorika hawa hawana biashara ya kuweka bus kwenye hotel za njiani nusu saa na ukipanda la kwanza saa saba uko moshi
 
Bufalo na ngorika ndizo gari za fasta dar express myeyusho hadi bajaji inaweza ikawapita
 
Bufalo na ngorika ndizo gari za fasta dar express myeyusho hadi bajaji inaweza ikawapita

Ushawahi kupanda dar express ya nairobi? hiyo gar inatangulia na haipitiki labda kwa modern ndo zinakimbizana na kuikuta ni namanga boarder
 
Lini unaondoka ?? Nikupe lift Nina private car ila naishia kibaha maili moja dar sifiki
 
Back
Top Bottom