Mtwakulyalam Chotipango
Member
- Mar 19, 2018
- 83
- 54
Asante kwa ushauri mkuu,kuhusu kulipa nilishasema nitalipa mwanzoni mwa mwezi wa NNE,tena hata sio laki tano nataka nilipe m1 kabisa,Mzee alichosema yeye ni kwamba hataki hela nusu,anasema kama inawezekana nichukue hiyo hela niitunze kwa mtu ikitimia ndo nimpatie!!
mkuu sheedah uliyo nayo ndyo niliyo nayo mimi, na kwa uelewa wangu mdogo nilio nao, itakuwa ngumu kidogo ukienda tofauti na baba mkwe anavyo taka, binfsi nimepeleka mahali mwezi ulio anza juzi mean tarehe 5/3/....
posa nilipiga mahesabu ya laki , washenga 30,. pamoja na nauli nilikuwa na bajeti ya laki mbili na nusu, ila nilicho kikuta kule ni tofauti kabisa na nilicho pigia mahesabu, nashukuru mungu nilkuwa na hakiba kama ya laki tano pembeni bila hivyo ninge adhilika mbele ya wazee pengine na kumkosa mke kabisa.
Nime waahidi kuwapelekea mali kidogo mwezi wa nane , kwahiyo mbaka mda huu nachart na wewe sijapoa bado kwenye hili suala....., kibarua nilichokuwa nategemea kingeniweka sawa kidogo ili mwezi wa nane niwe mwepesi kusafiri kwenda mkoani kwa wakwe kimeyumba tayari mean nipo natafuta kazi. kichwa changu cha moto kuliko hata wewe mkuu.