Msaada: Baba mkwe anakwamisha ndoa yangu

Msaada: Baba mkwe anakwamisha ndoa yangu

Jaslaws

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
6,016
Reaction score
5,301
Habari za mchana wakuu..

Naombeni msaada katika hili swala, japo sipendi sana kuanika Maisha yangu katika mitandao lakini kwa hili nimekwama kidogo nahisi nahitaji busara za watu wengine tofauti.

Naishi na mke wangu japo hatujafunga ndoa..tumebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume, ametimiza mwaka mmoja mwezi huu..

Tatizo linalonifanya kuomba msada kwenu ni, katika ya mwaka jana tulianza michakato ya ndoa tulianza kwa kulipa mahari, nilipangiwa mahari kubwa kidogo, mfano vitu vidogo vidogo kama sijui blacket la bibi, mbuzi sijui wa mjomba, vilikua vingi sana kwa ujumla wake nilitumia kama milion mbili hivi na kidogo, nikichanganya na nauli yangu na ndugu zangu tuliobebana kwenda kutoa mahari, kwa bahati mbaya sikuweza kutoa mahari yote kiukweli kama mnavyojua hali ya Maisha inabana sana siku hizi, nilibaki nadaiwa milioni moja na nusu ambayo kwao na binti wanaita mahari kuu, hiyo wanasema kwa kawaida inaenda kwa baba yake na binti,

Ishu inakuja mwaka huu tulipanga kufunga ndoa, tuliwasiliana na mshenga awape taarifa kwao na mke wangu kwa bahati mbaya mzee wa binti hakulipokea vizuri, alitaka kwanza mahari yake yote, nilifanya juhudi kuwaeleza kwamba kabla ya mwezi wa 4 ningepunguza angalau nilipe m1, mzee aliendelea kushikilia msimamo wake anahitaji hela yote, baada ya kubembelezwa sana alikubali kwa shingo upande, akatoa sharti kwamba vitu vyote atafanya yeye, kwa bahati mbaya huku kwetu tumeshaanza vikao ila kwao hata kutoa taarifa tu kwa ndugu hajafanya..kifupi hakuna kinachoendela na harusi imepangwa mwezi wa 6 inavyoonekana Mzee alikubali tu lakini hana nia ya dhati huku kwetu taarifa nilizowapa ni kwao na binti pia mipango inaenda vizuri...

Hapa nilipo kichwa kimejifunga kabisa. Niachane na harusi ama niendelee tu bila ridhaa ya baba wa mke wangu? Maana mke wangu yeye yuko tayari kufanya harusi bila hata kumshirikisha mzee wake

NB: Mzee wa mke wangu alioa mwanamke mwingine baada ya kuoa alihamia mji Mwingine..
 
"Mzee wa mke wangu alioa mke mwingine baada ya kuoa alihamia mji mwingine."

Kwan unadhan hiyo ndo sababu mzee akuwekee ugumu??

Lipa chake tuuu mzee akuruhusu kiroho safi[emoji23].

Sema nn ,mbn rahisi sana ,niivi umeshaanza vikao , ungekua bao ungetulia zako ilimradi mwanamke yuko ndan mwako angekuja kudai mahari ushamzalisha watoto wawili.

Hata ivo kama mkeo yupo tayar kwa lolote its okay wee funga naye ndoa japokua mzee hatokua amelipokea ,kitu pekee nikwamba kuna wakati unapaswa kuamus maamuzi mazito mazito bila kujali nani,na nini !!

Wazeee wengine hawafai kweli kweli.
 
*STRICTLY FOR MEN ONLY*

*When a man steals your wife, there is no better revenge than to let him keep her.*[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23]
_~By Lee Majors_

*After marriage, husband and wife become two sides of a coin; they just can't face each other, but still they stay together.* [emoji36][emoji23]
_~By Al Gore_

*By all means marry. If you get a good wife, you'll be happy. If you get a bad one, you'll become a philosopher.*[emoji848][emoji36][emoji23]
_~By Socrates_

*Woman inspires us to great things and prevents us from achieving them.* [emoji36][emoji23]
_~By Mike Tyson_

*The great question... which I have not been able to answer... is, "What does a woman want?*[emoji36][emoji23]
_~By George Clooney_

*I had some words with my wife, and she had some paragraphs with me.* [emoji1][emoji23][emoji36]
_~By Bill Clinton_

*"Some people ask the secret of our long marriage. We take time to go to a restaurant two times a week. A little candlelight, dinner, soft music and dancing. She goes on Tuesdays, I go on Fridays."*[emoji36][emoji36][emoji23]
_~By George W. Bush_

*"I don't worry about terrorism. I was married for two years."* [emoji36][emoji23]
_~By Rudy Giuliani_

*"I've had bad luck with all my wives. The first one left me and the second one didn’t.” The third gave me more children!*[emoji23][emoji23]
_~By Donald Trump_

*Two secrets to keep your marriage brimming*[emoji848][emoji36]
*1. Whenever you're wrong, admit it,*
*2. Whenever you're right, shut up.*
_~By Shaquille O’Neal_

*The most effective way to remember your wife's birthday is to forget it once.*[emoji33][emoji27][emoji109][emoji36][emoji23]
_~By Kobe Bryant_

*You know what I did before I married? Anything I wanted to.*[emoji6][emoji36][emoji23]
_~By David Hasselhoff_

*My wife and I were happy for twenty years. Then we met.*[emoji12]
_~By Alec Baldwin_

*A good wife always forgives her husband when she's wrong.*[emoji23]
_~By Barack Obama_

*Marriage is the only war where one sleeps with the enemy.*[emoji36][emoji23]
_~By Tommy Lee_

*A man inserted an 'ad' in the classifieds: "Wife wanted". Next day he received a hundred letters. They all said the same thing: "You can have mine."*[emoji23]
_~By Brad Pitt_

*First Guy (proudly): "My wife's an angel!"*
*Second Guy : "You're lucky, mine's still alive."* [emoji36]
_~ By Jimmy Kimmel_

*“First there is the promise ring, then the engagement ring, then the wedding ring...soon after....comes SuffeRing!*[emoji36][emoji23]
_~By Jay Leno_

*"The reason why wives live longer is because they don't have a Wife"*[emoji36][emoji23]
_~By Brandon Breezy_

*Forward this to all the guys to give them a good laugh .......and to the ladies with good sense of humour who can handle it!!!!!!![emoji3][emoji3][emoji3]*
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] vyuma vimekaza hadi kene ndoa
 
"Mzee wa mke wangu alioa mke mwingine baada ya kuoa alihamia mji mwingine."

Kwan unadhan hiyo ndo sababu mzee akuwekee ugumu??

Lipa chake tuuu mzee akuruhusu kiroho safi[emoji23].

Sema nn ,mbn rahisi sana ,niivi umeshaanza vikao , ungekua bao ungetulia zako ilimradi mwanamke yuko ndan mwako angekuja kudai mahari ushamzalisha watoto wawili.

Hata ivo kama mkeo yupo tayar kwa lolote its okay wee funga naye ndoa japokua mzee hatokua amelipokea ,kitu pekee nikwamba kuna wakati unapaswa kuamus maamuzi mazito mazito bila kujali nani,na nini !!

Wazeee wengine hawafai kweli kweli.
Dah em puzzled..sikuwai kujua kama mahali ni deni kubwa kiasi hiki,mwanzoni nilijua ni formalities tu.
 
Wewe ilipe yote ikiwezekana kakope ili upate baraka zake
 
Ninavyojua mimi mahari huwa hailipwagi yote
Huyo baba mkwe ameamua tu kukomaa makusudi ni kama hataki mwanae aolewe
Naona hivyo pia.. lakini sasa tumeshapata mtoto hata sielewi anakataa nini.
 
Wewe ilipe yote ikiwezekana kakope ili upate baraka zake
Kulipa yote ndio naweza hata bila kukopa lakini kuna mambo mengi yamenibana kumbuka nnaharusi pia inanisubilia!!
 
Huyo anaitwa mzee pesa mbele...

Baba mke kama huyo atakusumbua sana...

Hutakaa uwe na amani...

Cc: mahondaw
 
mkuu kosa unalo kubwa , ndoa haifungwi kabla hujalipa nusu mahali ukiacha ile posa uliyo toa , mahali laazima itolewe nusu ndipo ufikrie habari ya ndoa, Unajua why mzee amekomaa na mahali yake ....??? Mzee anajua kabisa ukisha funga ndoa itakuwa ngumu kupata chake....., pia utakuwa na maujukum mengi pia , kulea familia, (kama umepanga) kulipa kodi ya nyumba , upeleke watoto shule, na n.k kwa picha hii si dhani kama utapata nguvu ya kulipa mahali. Binfsi nashuri upeleke nusu hata laki tano inawatosha sana, ukitoka hapo ndiyo mazima usije fikria tena kupeleka hela mkuu.
 
Asante kwa ushauri mkuu,kuhusu kulipa nilishasema nitalipa mwanzoni mwa mwezi wa NNE,tena hata sio laki tano nataka nilipe m1 kabisa,Mzee alichosema yeye ni kwamba hataki hela nusu,anasema kama inawezekana nichukue hiyo hela niitunze kwa mtu ikitimia ndo nimpatie!!
 
Cha kufanya we endelea na harusi tu mkuu.

Huyo baba mkwe seems ni kimeo, anataka kumtumia binti yake kama kitega uchumi.

Ila ukishamaliz tu fasta piga mimba ya pili, utakuwa umekata longo longo zote
 
Huyo anaitwa mzee pesa mbele...

Baba mke kama huyo atakusumbua sana...

Hutakaa uwe na amani...

Cc: mahondaw
Mkuu huyo babamkwe hawezi kunisumbua sababu familia ya mkewangu aliitelekeza muda.anafanya kama kumkomoa mkewake( mama wa mkewangu)
 
mkuu kosa unalo kubwa , ndoa haifungwi kabla hujalipa nusu mahali ukiacha ile posa uliyo toa , mahali laazima itolewe nusu ndipo ufikrie habari ya ndoa, Unajua why mzee amekomaa na mahali yake ....??? Mzee anajua kabisa ukisha funga ndoa itakuwa ngumu kupata chake....., pia utakuwa na maujukum mengi pia , kulea familia, (kama umepanga) kulipa kodi ya nyumba , upeleke watoto shule, na n.k kwa picha hii si dhani kama utapata nguvu ya kulipa mahali. Binfsi nashuri upeleke nusu hata laki tano inawatosha sana, ukitoka hapo ndiyo mazima usije fikria tena kupeleka hela mkuu.
Kuka likee...kimsingi na kiutaratibu...ulitakiwa ujiandae kwanza kwny suala la maharii...malizana nao kwanza...kumbuka mkweo ana haki ya kuidai yote.TUsifanye kama formalities kuwa mahari haitolewi yote...kimsingi ni busara tuu ya kiafrika huwa inatumika..

At least ungetoa hata robo tatu..kwa wazee wengine huchukulia kuwa hicho ulichokifanya ni dharau..kumbuka umeshakaa na binti yake mwaka mzima na "kumzalisha" bila ridhaa yake,na bado ulipoamua kufuata taratibu unasuasua..Sijui kama umelipishwa faini.
Ila,kama umepangiwa mahari milioni 2..lipa hata 1.7 basi.

Suala la harusi ni lako muaoji.Sijui imekuwaje mpaka ukakubali kumuachia baba mkwe kama ulivyosema kwny uzi wako wa msingi...utadharaulika siku mkizinguana na mkeo....(Mark my words)
 
Cha kufanya we endelea na harusi tu mkuu.

Huyo baba mkwe seems ni kimeo, anataka kumtumia binti yake kama kitega uchumi.

Ila ukishamaliz tu fasta piga mimba ya pili, utakuwa umekata longo longo zote
Hahaha poa poa mkuu
 
Jitahidi umpatie Baba Mkwe hela yake ili ndoa yenu ipate kuwa na baraka.
 
Back
Top Bottom