Nyendeke
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 1,552
- 2,844
Poleni na majukumu Wanajanvi..,
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza, kuna dada mmoja ambae ni rafiki yangu alikuja kuniomba ushauri juu ya Mume wake ambae ni Mlevi kupindukia yaani hana muda wa kuijali familia kwa chochote kile kunzia Lishe, Mavazi, Malazi, Ada za Shule za watoto n.k, yeye anachojali ni Pombe tu, dada anazidi kulalamika kua Mumewe ana Mshahara mkubwa kiasi kama ungetumika kwa malengo basi mipango yao yote ingekwenda vizuri ila ndio hivyo tena jamaa kila akitoka kazini anapitia Bar anarudshwa usiku wa manane kwenye Mkokoteni akiwa ameutwika vilivyo na hajitambui.
Dada nae kipato chake ni kidogo kiasi hawezi kumudu majukumu hayo na amejaribu kwenda hata kazini kwake na kukutana na Bosi wa huyo Mume wake ili kama inawezekana apewe asilimia kadhaa katika Mshahara wake ila hajapata ushirikiano wowote kutoka kwa huyo Bosi ambae ni Mkurugenzi katika taasisi kubwa ya Serikali.
Pia familia yake imejaribu kukaa nae vikao takribani vitano kuhusiana na swala hilo Jamaa anakuwa muungwana na kuahidi kuwa ataacha ila akirudi kesho yake ameutwika zaid ya jana.
Hivyo Wandugu nisiwachoshe sana dada anahitaji msaada wenu wakupata dawa ya kumuachisha Pombe ama Ushauri utakaoweza kuinusuru familia yake.
Natanguliza shukrani Wakuu!!