Msaada: Aina gani ya laptop nzuri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Aina gani ya laptop nzuri?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by IT Guru, Mar 15, 2011.

 1. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Habari zenu wanajamvi. Natumai wote wazima kabisa. Mimi nahitaji ushaur kutoka kwa wazoefu wa laptop. Aina gan ya laptop ina ubora kwa sasa. Natangulisha shukran zangu
   
 2. L

  Leney JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 315
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mr.Cool,
  mahitaji ya laptob yanadepend sana na mnunuzi... jana nilikuwa namsikiliza mama yangu ananitajia aina ya laptop anayotaka akasema anataka ya ukubwa wa 10 inch, yani itoshe kwenye mkoba, nikamuuliza kwani unaitaka ya nini hasa, akaniambia yeye mwenyewe anataka tu laptop hata cha maana cha kuifanyia hana, atasoma magazeti na kusikiliza mahubiri ya mwakasege...LOL

  So wewe je unahitaji nini zaidi? durability, perfomance, graphics, constant video steaming, e-reading and browsing, dvelopment, yani hapa utapata msaada ukisema utakuwa unaitumia hasa kwa activities gani? kwa hiyo ubora is a relative term.
   
 3. Zasasule

  Zasasule JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  leney i think the guy amekusidia ipi ni imara!
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hapo penye blue pamenikosha sana. Bahati mbaya mini-laptop (za 10 inch) hazina cd/dvd Rom
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwa ushauri wangu nunua HP mkuu.
  Hp ninachoipendea huwa battery yake inadumu sana.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,504
  Trophy Points: 280
  Mr. Cool, ubora wa laptop unategemea unataka kufanyia nini kama ulivyoshauriwa lakini generally naweza kukupa ushauri wa brand gani kutokana na uzoefu wangu na sio utaalamu wala specification. Hii ni listi ya tano bora zangu.
  1. Apple
  2. Sony
  3. Toshiba
  4. Dell
  5. HP
  Hizo zote nimetumia, kila moja ina faida na hasara zake.

  Tukianzia na Apple, faida kubwa ni kwenye video na picha editing, haina mshindani. Program yake ya Final Cut Pro II mpaka sasa bado haijapata mshindani. Mimi binafsi natumia Mac Air Book kijistudio changu kinatumia Mac Book Pro 11 na zote hazijawahi kusumbua kabisa tatizo lake, ukifanya kitu kwenye Mac huwezi kurekebisha kwenye computer nyingine zaidi ya Mac kwani baadhi ya program zake nyingi haziko competible na wengine.

  Nikija kwenye Sony Vaio nazo ziko bombo, haswa upande wa vedio na miziki, haziharibiki ovyo tatizo la Sony ni moja tuu, betri zake hazikai muda mrefu ikikikuhurumia sana, basi itakaa kwa saa nzima tuu. Tatuzo jingine kwa bongo, hakuna authorised service ya sony, hivyo ikisumbua, ukipelela kwa mafundi wetu, mara nyingi huwa ndio mwanzo wa mwisho wa sony sony yako, ila mpaka iharibike ni shughuli!.

  Hizi Mac na Sony zote zina tatizo la ziada, hakuna za bei poa, Tanzania kuna maduka mawili tuu ya Mac, moja liko JM Mall, Elite Computers na jingine Shoppers Plaza, bei zote ni kuanzia M.1 na kupanda juu. Sony zimetapakaa maduka ya Wahindi na bei zinapoa kidogo.

  Toshiba na Dell pia ni laptop nzuri afadhali afadhali na ya mwisho ni HP, hizi kwa joto la bongo ni vimeo!. Nikiwa New Dheli, nilinunua HP Pavillion brand new toka duka la HP nikapewa na warantry ya mwaka mmoja. Nimerudi Bongo nimeitumia less than a year screen ikagoma kuwaka, just black screen. Nikaipeleka kwa HP dealer hapa bongo, kwa kuanzia akaniambia ile warant ni applicable New Dheli sio hapa bongo. Nikakubali kuilipia, wakaniambia display imekufa!. Hapa kwa fundi nilizishuhudia HP nyingine kibao zimekaa mkao wa kifo. Cost ya kuinunua hiyo display kujimlisha usumbufu nikaamua niiache tuu hapo kwa fundi na kuachana kabisa na HP kwenye maisha yangu ya laptop.

  Kwa matumizi ya watoto wa shule, vile vilap top vidogo, vi Atom vya Dell vitawasaidia sana, brand new vinauzwa laki nne kwenye maduka ya wahindi. Kama una jamaa zako nchi za nje, vinauzwa dola 200 tuu, ila kuwa makini na famba za China, zinauzwa Dola 100 tuu ila ni vimeo hatari cheza mbali!.

  Natumaini maelezo hayo yatakusaidia kujua ununue laptop ya jina gani, yaani brand name ipi.

  Pasco.
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kila brand maarufuu zina range of products zinzotofautiana performance , bei na specifaction

  HP tembelea HP Home Laptop PCs at a glance - HP Home & Home Office products uone HP envy, HP home Mini PC and HP pavillion . zote hizi ziko product range na series tofauti tofaiti
  Nachopenda kuhusu HP ni support website yao ni rahiiskutumia nakupata drivers. Pia kwa gharama HP zinaonekana ni nafuu kulinganisha na brand zingine zenye specifaction sawa

  Toshiba kuna satelite , Qosmio Portege, Satlite Pro na Tecra.
  unawezakutembela site hii Laptops, Netbooks & Notebook Computers | Toshiba uone wanatofautisha vipi mtumizi yake . Satelite na Portege are the model to for ukiamua kunuanua Toshiba brand. Kwa bei zipo satelite za kuanzia $ 399 mpaka nyingine zinafika $ 700 na zaidi. Nimetumia Toshba satelite ni laptop imara kulinganisha na baadhi ya HP

  Asus. Nimesoma review za watu mbali mbali online kuhusu laptop brand bora zaidi kwa perfomace naona Asus ndo mshindi. hasa kama wewe ni mtu wa gaming and mulmedia. sijawai kuitumia but sidhani kama hawa wana hata support center yeyote tanzania achilia mbali east africa. Hiki ni kitu cha muhimu . Pianadhni hizo Asus bora bei yake kwa mtanzania wa kawaida hazishikiki. Mfano kuna Asus G73SW-91136Z inafika bei ya £1,700. Kwa bei unawezakupata Toshba au HP mbili standard bila ku sacrife sana performance

  So kwanza fanya onlineshopping kwa kutembelea tovuti kama dell, HP Toshiba, Acer, Then chagua model kama tatu au nne . Leta hapa model ulizochagua. Uliza watu ipi ni bora.
   
 8. X-not

  X-not Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahahaaa! Nimeipenda hiyo, atakuwa anaazima external CD/DVD drive kutoka kwa mtoto wake, au atatumia flash.
   
 9. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Shukran sana wanajamvi. Yani mmenisaidia sana, nimejua vitu vingi kuhusu laptop sasa ambavyo sikuvifahamu kabla. Nawashukuru wote kwa ushaur wenu, utingo, zasasule, x-not, leney, pasco, mtazamaj na ndibalema. Ahsanteni sana
   
 10. c

  cc_africa Senior Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nokia 3g laptop
   
 11. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  aise ndo kwanza naijua saa hivi hii. Shukrani mkuu, Ila kwa hapa tanzania inapatikana kwel?
   
 12. Brakelyn

  Brakelyn JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,236
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145


  ukisema maduka mawili tu Tanzania nzima unakuwa unakosea mkubwa..maduka kama Sound & Vision, Benson Co. na Computec ltd ya Arusha yanauza computer za Mac..
  Mr. Cool, do visit this notebook check website so u can do more comparison between different laptop Brands, utaweza kujua ni laptop ipi yenye Graphics Card nzuri zaidi, portability, CPU performance, Business Laptop, Gaming and Multimedia na utapata advice ya kununua laptop..
  ( FAQ / Tips / Technics - Notebookcheck.net Tech), cheers.
   
 13. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  oh ngoja niipitie sasa, thank u very much Brakelyn.
   
 14. A

  Al-shabaab JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2013
  Joined: Aug 24, 2013
  Messages: 1,704
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Ushauri mzuri
   
 15. costerntine

  costerntine Senior Member

  #15
  Oct 31, 2013
  Joined: May 5, 2013
  Messages: 163
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  HP by dr.dre
   
 16. S

  Silent Sinner Member

  #16
  Nov 1, 2013
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Je, battery ziko poa? Nkimaanisha muda wa utunzaji umeme.
   
 17. u

  utantambua JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2013
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sishauri HP sizipendi, wi-fi hazishiki, nimetumia mbili tatu hivi, zote ukiturn on wi-fi hazikubali, nime-google naona hilo ni tatizo la wengi mtandaoni pia.
   
 18. costerntine

  costerntine Senior Member

  #18
  Nov 5, 2013
  Joined: May 5, 2013
  Messages: 163
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tatizo no mtumiaji aliye kuuzia usitegemee adopter ya wifi iwe Haipo au imekufa alafu ukatalajia ifanyekazi.lazima ikatae maana kuzichomoa makukuwekea mbovu nirahisi.HP hawana matatizo lands ukinunua zain machinations Ndogo hata driver zinasumbua.ninja zain mitumba ingawa being Zainabu shabiliana.Manana nkuna mtu nilitaka kumuuzia laptop Acer Kwa laki6 akasema sibora niende dukanitu nkasema ok.baadae akaleta malalamiko Kuwa inamsumbua.nikamwambia joyous Ndogo tofaut ya mtumbani NA dukani.hivyo bei nafuu lazima ikugharimu
   
 19. simango

  simango Member

  #19
  May 13, 2017
  Joined: Oct 20, 2014
  Messages: 93
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25
  mkuu mimi natumia macbook pro nimenunua juzi tu ni ya mtumba lakini bado iko fresh

  macbook pro 13 inch mid 2012
  processor 2.5 ghz intel core i5
  memory 4 gb 1600 mhz ddr3
  graphics intel hd graphics 4000 1536 mb

  vipi hii mkuu itafaa kwa matumizi ya kawaida au ina uwezo mdogo sana
   
 20. chizcom

  chizcom JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2017
  Joined: Jul 31, 2016
  Messages: 1,050
  Likes Received: 859
  Trophy Points: 280
  kwa kazi hipi na kwa ajili ya kitu gani
   
Loading...