Nasikitika sana kwamba warembo hawa walidanganywa wakaingia kichwakichwa kwenye mapigano wasojua sababu, chanzo wala hatima yake, sasa wakati niandikapo comment hii nahisi wengi wao wameuawa kwa makombora ya jeshi la serikali waloichokoza yakisaidiwa na majeshi ya nchi rafiki na wapenda amani; kama wamenusurika kifo, watakuwa mafichoni wakiomba Mungu serikali na jeshi la DRC wawaonee huruma! Wako wapi walowadanganya, wakawanunulia sare, siraha, chakula, na kuwalipa vijiposho vya uongo na kweli ili tu wao waendelee kuchuma rasilimali za DRC? Nadhani rafiki ya JK, Mr. PK (shame on him) huko aliko haamini kilichowatokea M23, kama ana akili awashauri wavue magwanda rasmi na kurudia maisha ya kiraia, wakaungane na waCongo wenzao kuijenga nchi yao, vita kamwe si suruhisho la matatizo yao! Na kwa upande wake Mr. PK, namshauri aache uroho wa mali za jirani zake, na aache ndoto za kutaka kuwa "superior race in the region"