Hivi kuna mtu yeyote wa kuniambia
ile taarifa kuwa Ngasa kafaulu majaribio
huko maerekani
na atakwenda January imeishia wapi?
naona sasa ni April kama sikosei na Ngasa yupo tu Azam anaendelea...
what happened?....
OCHA wa Azam FC, Stewart Hall
amekanusha taarifa kuwa kiungo wa timu
hiyo, Mrisho Ngassa alifuzu majaribio ya
kucheza soka la kulipwa aliyoyafanya
mwaka jana nchini Marekani katika klabu
ya Seattle Sounders.
Ngassa ambaye alipata nafasi ya kucheza
dhidi ya Manchester United alipokuwa
kwenye majaribio hayo, ilielezwa kuwa
amefanya vizuri na angeitwa kufanya
mazungumzo juu ya kusajiliwa mwishoni
mwa msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa,
Stewart alisema wenyeji wa Ngassa katika
majaribio hayo walifurahishwa na
kiwango kilichoonyeshwa na winga huyo
lakini hakuwa na ubora wa kucheza katika
Ligi Kuu ya Marekani.
"Nilishangazwa na taarifa zilizokuwa
zimeenea mara baada ya Ngassa kumaliza
majaribio yake, hakufuzu, kilichotokea ni
kwamba walimsifia kwa kiwango
alichoonyesha katika mazoezi waliyompa,"
alisema Stewart na kuongeza:
"Ukiangalia Ngassa anatoka katika ligi
yenye ubora mdogo ukilinganisha na ile ya
Marekani, jambo ambalo lingemlazimu
kufanya kazi ya ziada ili kuweza kufikia
kiwango cha kucheza ligi hiyo.
"Nadhani hilo pia ndilo lililosababisha
acheze chini ya kiwango katika msimu huu
wa Ligi Kuu ya Bara kwa kuwa bado
alikuwa na ndoto za kwenda kucheza soka
la kulipwa nje."
Viongozi wa Azam FC, waliwahi kusema
Ngassa alifuzu baada ya kucheza katika
mechi ya kirafiki ya Seattle Sounders dhidi
ya Manchester United ya England.
Chanzo: Gazeti la Champion Ijumaa