Huey freeman
JF-Expert Member
- Sep 20, 2013
- 593
- 248
Nina wasi wasi nyimbo ya mrisho mpoto ni kuhusu katiba au vyama vya upinzani hasa hasa chadema walio itwa ikulu kutokana na mizozo ya katiba , wote nadhani tunajua jina la mjomba linamaanisha nani. pili nyimbo za mrisho mpoto zimekua zina husu jamii na siasa..mashairi yanasema hivi ;...................................... waite wakalishe chini, waambie wao hawamo japo walikula.....mjomba kuna baadhi michezo ukishindana mwenyewe lazima uwe mshindi lakini kwa mchezo ule uliwahitaji ili kuongeza mashabiki na washangiliaji walio na sauti zisizokauka...walivyoanza mjomba hakuna alie dhani kwanza walifika mapema mmoja wao aka andikisha jina lake kwa niaba ya wengine japo wote wanamajina yao na hayafanani....waliingia wakajipanga kwa sauti zao ya kwanza mpaka ya nne wakaanzisha mapambio watu wakilia wao wanatoa pole tu, na waandishi kwa utashi wao wakaandika msiba umefana kweli hakuna alie lia nje ya key...mjomba ushauri wangu waite....waambie muungwana hanuni kwa mashavu hununa moyoni....wao hawahusiki wala hawamo waje tu kua mashahidi kwakua nao walikuepo na walikula japo kua hawakujua wapi ulimtoa mbuzi yule.. mjomba ushahidi wao utakusaidia katika vitu viwili kuingia katika historia au kushinda kesi....................................bado sijajua kama niko sahihi sana ila nimeamua kuwaletea wana intelijensia wa jamii forum pamoja tutafakari maneno haya na myatolee ufafanuzi sababu mrisho mpoto mwenyewe kamwe hataweza kusema alichokimaanisha kwa sababu za kiusalama that is how he work and how he will always work. ahsanteni.