Mrisho Mpoto amepoteza dira au anaona tusichokiona wengi kwa Magufuli?

BRUCE LEE

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
2,096
1,333
Ndugu wama jamvi, nauliza swali hili kwakua mtajwa hapo juu amekua haeleweki tokea serikali hii ya awamu ya tano, wengi tunamfaham Mrisho Mpoto na namna gani alivyo mzuri katika matumizi ya fasihi kufikisha ujumbe pamoja na kuikosoa serikali, alijipatia umaarufu mkubwa sana katika utawala uliopita baada ya kua anafikisha ujumbe kwa kutumia mashairi yake ya mjomba, kiukweli wengi tulimpenda saana na kuhisi pengine na yeye ni mmoja kati ya wazalendo wachache waliobaki na wenye uthubutu wa kutumia vipaji na uelewa wao katika kuirekebisha jamii hasa tabaka tawala bila kua na hofu.

Nilichokiona leo moshi, ni tofauti na nilivyozea kumuona na kumsikia mrisho mpoto, nimeona unafiki kabisa katika mashairi yake, na pia nimeuona uongo wa dhahiri pamoja na kumsifia saana mheshimiwa Rais mpaka kufikia kumpa cheo kipya kua rais wa sasa ni mteule kutoka kwa Mungu na pia ameshusha toka mbinguni hivyo basi yupo sahihi saana na ni rais pekee ambao hajawahi tokea hapa tanzania pengine na afrika kwa ujumla.

swali linalo niumiza zaidi ni kwamba je Mrisho Mpoto katumwa au kajituma mwenyewe kuongea yale maneno? kashinikizwa au kaongea kwa utashi wake?

nimeanza kua na mashaka ya huko tunapoelekea maana kitendo cha kuwatumia watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii kama mrisho mpoto kutuaminisha kua rais ni bora sana na pia ni mteule wa mungu na ndio maana hata mvua imenyesha hapo uwanjani ni dalili tosha hata siku rais akiingiwa na tamaa ya kutaka kufanana na wenzake akina kagame, museven na kabila ili katiba ibadilishwe na akae muda mrefu, watu hawa akina mpoto wakitumika tunaweza ingiwa kwenye matatizo makubwa ya utawala wa ki imla.

naomba kuwasilisha.
 
Wewe humpendi,na unasababu zako ambazo labda hatuzijui. Lakini usitake wote wasimpende,kama mpoto kaona hivyo na wewe ona vile,
Kuhusu hayo mambo ya uchaguzi kwa upande wangu mie natamani hata iwe ni miaka 20 kabisa,sipendi rabsha za uchaguzi mie,na huwezi kunibadilisha mtazamo.
Wewe ni mtu mzima acha kabisa kushikiwa akili na huyo mpoto,kuwa na maamuzi yako kwani nani anajua kilichobora kwako zaidi yako?
 
kwa hiyo tumuamini mpoto kua rais wa sasa ni mteule wa mungu na kashushwa toka mbinguni?
 
Ndugu wama jamvi, nauliza swali hili kwakua mtajwa hapo juu amekua haeleweki tokea serikali hii ya awamu ya tano, wengi tunamfaham Mrisho Mpoto na namna gani alivyo mzuri katika matumizi ya fasihi kufikisha ujumbe pamoja na kuikosoa serikali, alijipatia umaarufu mkubwa sana katika utawala uliopita baada ya kua anafikisha ujumbe kwa kutumia mashairi yake ya mjomba, kiukweli wengi tulimpenda saana na kuhisi pengine na yeye ni mmoja kati ya wazalendo wachache waliobaki na wenye uthubutu wa kutumia vipaji na uelewa wao katika kuirekebisha jamii hasa tabaka tawala bila kua na hofu.

Nilichokiona leo moshi, ni tofauti na nilivyozea kumuona na kumsikia mrisho mpoto, nimeona unafiki kabisa katika mashairi yake, na pia nimeuona uongo wa dhahiri pamoja na kumsifia saana mheshimiwa Rais mpaka kufikia kumpa cheo kipya kua rais wa sasa ni mteule kutoka kwa Mungu na pia ameshusha toka mbinguni hivyo basi yupo sahihi saana na ni rais pekee ambao hajawahi tokea hapa tanzania pengine na afrika kwa ujumla.

swali linalo niumiza zaidi ni kwamba je Mrisho Mpoto katumwa au kajituma mwenyewe kuongea yale maneno? kashinikizwa au kaongea kwa utashi wake?

nimeanza kua na mashaka ya huko tunapoelekea maana kitendo cha kuwatumia watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii kama mrisho mpoto kutuaminisha kua rais ni bora sana na pia ni mteule wa mungu na ndio maana hata mvua imenyesha hapo uwanjani ni dalili tosha hata siku rais akiingiwa na tamaa ya kutaka kufanana na wenzake akina kagame, museven na kabila ili katiba ibadilishwe na akae muda mrefu, watu hawa akina mpoto wakitumika tunaweza ingiwa kwenye matatizo makubwa ya utawala wa ki imla.

naomba kuwasilisha.
Sasa huyo mpoto yupo kwenye system kapewa siniha la pilau watz tunalalamika na kuponda tukiwa nje ya system ya ufisadi tu.jamaa nae anaosha shavu tu hailuusiwi kushangaa
 
Twafwaaa
 
Back
Top Bottom