70.
“Baby, katika maisha yangu sijawahi kupata raha ninayopata..?”
“True..? (Kweli..?)”
“Yes baby. Napenda tuendelee tena hata ukitaka mpaka asubuhi. Tuendelee tu baby kwani mwenzio nasikia uhhh..!! uhhh…!! Uhhh..!! uhhh..!!! malizia baby mwenzio nah..”
Alice akamkumbatia Aloyce kwa mara ya pili. Akamkumbatia kwa nguvu zake zote uku akitoa makucha yake nakuanza kumparaza kuanzia mgongoni mwake. Utamu ukamnogea sambamba na mwili wake kumsisimka, akachomoa meno yake na kuhamishia mpaka shingoni mwa Aloyce. Kwa utamu wa mapenzi aliokuwa nao Alice akajikuta amemuweka Aloyce alama ya mapenzi. Ikawachukuwa saa mbili nzima wakiwa kitandani uku kila mmoja akijiona yupo katika bahari ya mapenzi. Bahari ambayo ina kila kitu, mtumbwi, maboya na fimbo zake. Walipomaliza kufanya mapenzi wakapeana pongezi kila mmoja kwa kupeana ndimi zao sambamba na mate.
“Mupenzi sasa tunaweza pumzika..”
“Sawa baby wangu utakavyo..yaani usiku huu sintoweza kuusahau maishani mwangu kwani umenifanya kuwa mwanamke kweli aliyekamilika. Nakupenda sana Aloyce..”
“Hata mie penda sana kuanzia sasa na kuendelea nahitaji nikuoneshe kwa tendo..”
BAADA YA MWAKA MMOJA
Maisha ya Aloyce na Alice yakawa mazuri sana. Mama yake wa kufikia,Janet akawa bega kwa bega na wao. Raisi wa Rwanda, Kagwa Rwisereka ambaye ndiye baba yake na Aloyce akawa anajua mahusiano kati ya mtoto wake Aloyce na Alice. Katika maisha ya Alice hakuwahi hata kushikana mkono na rais yeyote lakini sasa kwake yakawa kama mazoea kila baada ya wiki yeye na Aloyce ni lazima waingie ikulu kumsalimia rais Kagwa Rwisereka. Chuo cha Loyce Trainging Collage sasa kikawa chini ya Alice. Alice akakabidhiwa kusimamia miradi mingi mbali mbali. Mingi kati ya hiyo alimpa mama yake amsaidie kusimamia. Watu wote maarufu nchini Rwanda wakawa wanamtambua Alice kama mchumba wa Aloyce. Kamwe hakupenda majigambo wala kumnyanyasa mtu yeyote kwa pesa alizokuwa nazo. Mipango mikubwa ikawa ni kutaka kuanza vikao vya harusi kati ya Alice na Aloyce. Taarifa za kutaka kuoana zikasambaa zaidi karibia Rwanda yote wakawa wanalitambua hilo. Baba yake aloyce, Kagwa Rwisereka akawa ameshajitolea kusimamia na kuendesha harusi yote kuanzia ukumbi, chakula, usafiri na vinywaji na hata kuwaalika marais wenzake. Aloyce akafurahia sana. Mipango ya harusi na vikao vikaanza taratibu. Janet akawa kama msemaji mkuu badala ya Alice. Alimdanganya mambo mengi sana Aloyce. Kwa mujibu wa Janet, Aloyce akawa anajua kuwa Alice hana baba, alishafariki hivyo anaishi na mama tu na ndiye Janet.
Miezi mitatu kabla ya Ndoa yao mara Alice akaanza kujiona tofauti. Amani ikaanza kumpotea kutokana na ndoto ambazo zilikuwa zikimuandama mfululizo. Ndoto mbaya juu ya maisha yake. Ndoto kubwa iliomsumbua ni juu ya mauaji alioyafanya kipindi cha nyuma akiwa anashiriki mashindano ya mrembo wa Tanzania. Mauaji ya mashiriki mwenzake Jamila Said. Mashindano yaliompelekea Alice kuua kabla siku yenyewe ya mashindano ili apate kushida taji la membo wa Tanzania. Duku duku likamjaa sana moyoni, ila alipokuwa akitembea Alice akawa anahisi anaongozana na Jamila. Hata usiku akilala na mchumba wake Aloyce bado alikuwa akijihisi Jamila yupo pembeni yake uku akimuongelesha. Ndoto zikamzidia na kumnyanyasa hali iliomfanya akose kabisa raha ya usingizi. Kichwa chake Chote kikatawaliwa na jina la Jamila. Akajitahidi japo kulala lakini kwa bahati mbaya akashtuka usingizini na kutaja jina la Jamila. Akatoka usiku huo huo nakuelekea mpaka chumbani kwa mama yake napo alipofika tu mlangoni akahisi ametokewa na mzimu wa Jamila. Alice akadondoka chini nakuanza kutapatapa. Kile kifafa chake cha muda mrefu kikachukua nafasi yake. Akaanza kutapatapa uku mdomoni akitoa mapovu na kujinyonga nyonga mithili ya nyoka wa kwenye maji. Usiku huo huo Aloyce akashtuka kutoka usingizini nakujikuta yupo peke yake kitandani.
“Alice muke yangu..??, Alice..??”
Akaita sana uku akitoka nakuelekea kumtafuta bafuni bila mafanikio. Akaenda mpaka sebuleni napo hakumuona ndipo akasikia sauti ya Alice ikiguna chumbani mwa Janet. Kwa ujasiri aliokuwa nao Aloyce akajikuta ameufungua mlango bila hata ya kupiga hodi. Macho yake yakakutana uso kwa uso na mchumba wake, Alice akitapatapa uku akiupiga ukuta kwa mateke na mdomoni akitoa povu jingi.
“Tubebe hii mama, nini natokea..? ebu tuipeleke hospitali..”
“Twende tumuwaishe mwanangu..”
Aloyce na Janet wakambeba Alice. Alice akawa na nguvu zaidi kushinda wao kwa kujitupa. Ikabidi waite askari wa getini wakaja wakasaidiana kumbeba nakumpakiza kwenye gari na safari ya kuelekea hospitali ikaanza. Haikuwa mbali sana kwani kwa mwendo wa dakika tano wakawa wameshafika. Wakamshusha nakusaidiwa na manesi kumpakiza kwenye machela lakini Alice akawa tayari ameshapoteza fahamu na lile povu liliokuwa likimtoka mdomoni likabadilika nakuwa damu damu nzito na nyeusi. Wakamkabidhi daktari na kisha wao kutoka nje wakisubiria alice atibiwe.
“I cant..!!, Nataka kuelewa muke yangu inakuwaje..?”
“Aloyce mwanangu, ni story ndefu lakini naomba nieleweke. Nakuomba tena unisikilize ili tujue namna ya kumsaidia..”
“Go on, …endelea Janet..??”
“Mwanangu Alice toka nimemzaa ana matatizo ya kifafa na huwa anapoteza fahamu anapopata hali ya kushtuka. Hatakiwi kupigiwa makelel sana na hata kupewa habari za kushtua moyo wake. Na hata hivyo nilijua kashapona kutokana na daktari aliyemtibiwa mara ya mwisho kuniambia kuwa amepona hataangauka tena..”
Mama wa kufuikia na Alice,Janet. Akajikaza na kutoa maneno ya uongo ili kuweza kumchochoea Aloyce aelewe na kutuliza hasira ambazo zilikuwa zimempanda.
“Na mbona hamukuniambia..? kuki..? kuki Janet..?(kwanini)”
Aloyce alilia sana. Akarudi mpaka wodini alipokuwa amelala Alice hajitambui kwa kuwekewa mirija ya kutolea hewa(oxygen). Daktari alikua ameshatoka hivyo ni manesi pekee ndio walikuwa wamemzunguka Alice. Walipomwona Aloyce wakampisha.
“Alice, Alice nakupenda sana muke angu.. you’re the only one in my life(wewe ni wa pekee maishani mwangu).. sipendi ikakupoteza mupenzi angu..”
Aloyce akalia sana mithili ya mtoto mdogo akinyang’anywa kitu chake cha kuchezea. Akajiona ni mtu wa kukata tamaa kwa matatizo aliokuwa nayo Alice. Aliithamini sana bahati aliokuwa nayo ya kuishi na mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania. Akajiona kamwe hawezi kumpata msichana kama Alice. Kwa upole na ukarimu aliokuwa nao, ucheshi na hata alipendwa na kila mtu hata baba yake.
*********
Taarifa juu ya kuanguka kwa ugonjwa wa kifafa ghafla kwa Alice na kisha kuwahishwa hospitali ya Theodore Hospital pembeni kidogo ya mji wa Butare nchini Rwanda zikawa zimeshamfikia rais wa Rwanda Kagwa Rwisereka, baba wa Aloyce. Alizipokea kwa masikitiko makubwa sana na alikuwa na roho ya chafu. Akaona endapo Aloyce atafunga ndoa na Alice basi itakuwa aibu kubwa sana haswa kwa yeye alivyokuwa na madaraka makubwa ya kuiongoza nchi ya Rwanda. Akaona ugonjwa wa kifafa aliokuwa nao Alice utakuwa doa kubwa sana katika familia yao. Akalifikiria sana swala la mtoto wake kunyanyasika na mapenzi tena kwa binti ambaye si wa nchini mwao. Mawazo yake yakachanganua sana juu ya swala hilo. Kamwe halikumuingia akilini. Halmashauri ya kichwa chake haikuafikiana na hilo swala. Alichomaua kukifanya alipiga simu moja ka moja kwa aloyce.
“..Akana Aloyce.. (Mwanangu Aloyce)“
“Yego data ( Naam baba)”
“Nakuomba ikuje ikulu mara moja..??”
Aloyce akaonekana kuitii amri ya baba yake. Akamuangalia sana Alice kwa mara ya pili. Alice alikuwa bado hajarudiwa na fahamu hivyo Aloyce akamshika eneo la usoni na kumbusu. Safari ya kutokea hospitali mpaka ikulu alipokuwa baba yake hapakuwa mbali sana. Ikamchukua Aloyce kama nusu saa akawa ameshafika.
“Aloyce..?”
.
“yes baba”
“nasikia hiyo msichana naumwa fafa..? ipo dalili ya yeye pona..?”
“dady, just a long story..(hadithi ndefu baba)”
John akamuhadithia kama alivyokuwa ameambiwa na Janet. Kagwa Rwisereka akasikiliza kwa makini maneno aliokuwa akiambiwa na mwanaye Aloyce juu ya Alice.
“Manangu ipo penda sana mie.. wewe ni pekee..Koya (achana naye) itatutia aibu kubwa sana na gonja yake hiyo..”
“Baba nooo, sipo tayari kumuacha alice, nampenda sana dady, yeye ndie mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania na sintokuja kupata kama yeye dady..?”
“Hiyo gonjwa ya fafa huwa haina tiba. Haiponi hiyo and her life itakuwa vivyo hivyo.. itakusumbua sana na mwishoe itakufia believe me manangu.. just leave, iache ikwende kwao Tanzania tapata ingine..”
Maneno yale yalimkosesha sana Aloyce nguvu. Akayafikiria sana mambo ambayo aliyapanga yeye na Alice. Ahadi walizokuwa wamewekeana ndani ya mwaka mmoja. Harusi kubwa na ya kifahari ambayo baba yake Aloyce Kagwa Rwisereka ndiye alikuwa ametoa ahadi ya kuigharamia leo hii ndio huyo hataki tena mwanamke aoe msichana mwenye kifafa. Aloyce aliumia sana. Akabaki nji panda bila ya kuelewa afanyaje. Kamwe hakuwahi kumbishia baba yake. Akatoka mule ikulu uku akiwa ametii amri ya baba yake japokuwa alikuwa na hasira sana. Akaingia ndani ya gari na kuliwasha kwa hasira sana akielekea hospitali alipokuwa amewaacha Alice na mama yake.
“Sina jinsi acha iende kuwafukuza yote. Mungu kubwa sana ipo Nampata ingine soon. My dad itabaki kuwa dady na nitazidi kumheshimu na sitaki kamwe nimuuzi.. Alice nitaipenda ‘ariko’(lakini) wacha irudi tu kwao, no way out..”
Aloyce akajikuta akizungumza mwenyewe njiani akiendesha gari. Haikumchukuwa mwendo wa nusu saa kama ilivyokuwa mara ya mwisho. Kwa sasa ikamchukua dakika kumi na tatu tu kuingia hospitali ya Theodore. Akamkuta Alice ameshastuka anaangaza macho huku na kule uku bado kawekewa mirija ya kupumulia. Janet alikuwa pembeni yake. Aloyce akawaangalia kwa uchungu na hasira uku machozi yakimtoka kila akifikiria amri aliopewa na baba yake.
“Janet, Alice iko penda sana nyinyi, penda sana. ‘Ariko’(lakini) kuanzia sasa na…”
Janet akabaki mdomo wazi akimtolea macho Aloyce vivyo hivyo na Alice.
“Hata sisi tunakupenda sana kwani vipi mbona umekuja uko na hali hiyo kuna nini tena Aloyce..??”
“Pana kitu. Mimi penda sana nyinyi na Alice penda na wewe..”
Aloyce akajikuta anarudia rudia maneno. Akili yake yote ikawa imezungukwa na amri ya baba yake. Amri ya yeye kuachana na mpenzi wake anayempenda sana kutoka moyoni. Mpenzi ambaye alipata shida mpaka kuhakikisha anakuwa mikononi mwake kutoka Tanzania mpaka Rwanda. Kila akiuangalia uzuri wa Alice na akijenga picha kichwani kwake kuwa ndiye mrembo nambari moja kwa uzuri Tanzania roho yake ilikuwa ikimuuma sana.
“Janet..??, Janet embu ikuje mara moja hapa pembeni..??”
Aloye akamvuta Janet kwa pembeni kumnong’oneza kitu.
“Najua kuwa Alice iko umwa sana, sana na gonjwa ake ni fafa, is it..?”
“Kweli kabisa Aloyce..”
“My dad iko chukia sana hiyo gonjwa na Alice..? na ndio iliniita baada kusikia kuwa Alice gonjwa sana kwa hiyo fafa. na mimi siko tiyari kukosana na dady yangu wala kuacha hii Alice potee..”
“Aloyce..? ugonjwa wa kifafa ni kama ugonjwa mwingine tu. Unaweza kupona taratibu na kuhusu baba yako wewe mwambie kuwa Alice atapona tu asiwe na wasi wasi..”
Aloyce akakaa kimya zaidi ya dakika tatu nzima uku akiinamisha kichwa chake chini.
“Anyway..!! itamwambia pana shaka..”
Aloye hakuwa na jibu lolote zaidi ya kujiuma uma nakumfariji Janet ili tu aridhike. Akili yake bado ilikuwa imevurugwa. Akajikuta akibaki peke yake nyuma uku janet akirudi kitandani alipokuwa amelala Alice.
BAADA YA WIKI
Hali ya Alice ikakaa sawa. Kule kudondoka mara kwa mara kukapungua, japo Aloyce bado aliweka duku duku moyoni mwake. Hakuwa tayari kumuona Alice akirudi kwao Tanzania nakumuacha mpweke kisa maamuzi ya baba yake. Hali ile Ikamfanya awaambie ukweli wote juu ya siri hiyo kubwa kutoka kwa baba yake ambaye alionesha kubadilika na kuyapinga mahusiano yao kutokana na ugonjwa huo wa kifafa. Siku Alice alipoambiwa wazi na Aloyce juu ya kutokupendwa na baba yake Aloyce alidondoka tena kifafa lakini kwa safari hii hawakumpeleka hospitali
itaendelea
BURE SERIES/USER]