Nakerwa sana na staili hii ya kutuhumu watu na kuwalaumu kwa kufuata mkumbo tu. Nchi haitaendeshwa kwa magazeti ya mengi. Kuna vyombo vya kutosha kabisa kusaidia taifa hili likaenda mbele bila ufisadi. Huu ufisadi unaohubiriwa na vyombo vya habari kwa masilahi ya watu na kundi fulani katika nchi yetu mimi nauita upuuzi mtupu.
Chanzo cha habari siyo Gazeti la Mengi. Umeambiwa ni Tanzania Daima inayomilikiwa na Freeman Mbowe. Pia kwa kuongezea tu, Raia Mwema wameandika sana kuhusu hili swala la Mrema mpaka waki-quote barua za Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundo Mbinu. Sasa kipi ambacho ni uzushi? Kama ingekuwa ni uzushi, Katibu Mkuu wa Wizara angemtaka Mrema ajieleze kwanini alifanya maamuzi bila kuishirikisha Wizara?
Kwa staili hii ya kuwatuhumu watu wanaolitumikia taifa bila ushahidi wowote, tunatengeneza utamaduni mbaya sana. Leo nikikuchukia na kama nina mahusiano mazuri na wenye vyombo vya habari basi kazi ya kukumaliza inakuwa rahisi sana.
Wewe ndiyo unasema kwamba hakuna ushahidi, lakini ushahidi upo. Tatizo ni kwamba serikali yetu kwa kushirikiana na vyombo vya dola wamekuwa wakifunika ushahidi ili kesi zisiende mahakamani. Hata pale ambapo pana ushahidi wa wazi kabisa, tumeshuhudia mambo yakiachwa kama yalivyo. Chenge aliishia kujiuzulu, kama alikuwa anazushiwa ilikuwaje akakubali kujiuzulu? Kesi yake mpaka leo imedoda na hakuna kinachoendelea na bado wewe unataka tuamini kwamba ni uzushi?
Wangapi wanachafuliwa majina yao na haya magazeti yenye dhamira na maslahi ya wamiliki. Dr Rashidi kaandikwa wee, lakini huyu ni mmoja wa watu waliokuwa wanadhamira ya dhati ya kuliendesha shirika la umeme kwa mafanikio. Mrema kaandikwa wee, lakini haondolewi kwenye nafasi sasa maana yake nini?
Tuache tabia ya kuharibiana na kushadidia mambo ambayo hatujui kichwa wala miguu.
Kama wanaona kwamba wanachafuliwa majina yao, si waende mahakamani kudai haki. Sumaye alichafuliwa na wanamtandao kwa kutumia gazeti flani hivi, alipoenda mahakamani gazeti liliamuliwa kumlipa fidia. Kama mtu anachafuliwa jina, njia iko wazi kwenda mahakamani kudai haki. Nani ambaye yuko tayari kuchafuliwa jina lake ili kuharibu career yake ama credibility yake?
Tatizo nimeishalisema hapo juu, serikali yetu kwa kushirikiana na vyombo vya dola wamekuwa wakiangalia ni nani apelekwe mahakani na yupi ushahidi wake uchimbuliwe kiasi kwamba akienda mahakamani akose upenyo wa kupona.
Kesi za EPA ushahidi uko wazi, lakini ni kampuni chache ambazo zimefikishwa mahakamani. Akina Malegesi wanaendelea kudunda mtaani na hawajapelekwa mahakamani na hata waliopelekwa mahakamani utashangaa mwisho wa siku wanaachiwa kwa kigezo kwamba hakuna ushahidi ama upande wa mashitaka umeshindwa kuwatia hatiani.
Hukumu ya Liyumba imetolewa na pande mbili, hakimu mmoja kamuona hana hatia, mahakimu wengine 2 wanasema ana hatia. Liyumba alishasukuma mzigo kwa Ballali, na ni wazi Liyumba alikuwa chini ya Ballali hivyo asingefanya maamuzi yoyote bila ya maelekezo ya Ballali. Ukiwauliza PCCB walikuwa wapi wasimhoji Ballali akiwa hai ili wawe mashitaka ambayo ni concrete? Wanasubiri mhusika mkuu anapoteza maisha ndipo wanakuja kupeleka kesi mahakamani. Kesi ikikosa maelezo ya mhusika mkuu, nguvu ya mashitaka inapungua. Liyumba alipofungwa miaka 2, serikali na wapambe wao wanajisifu kwamba wanawashughulikia mafisadi. Kifungo cha miaka 2 hakiendani na hasara ya pesa zilizozama kwenye ujenzi wa Twin Towers, kama kesi hiyo ingeanza zama za uhai wa Ballali wengi wangeunganishwa na wala Liyumba asingefungwa miaka 2 tu.
Hii ni siasa na wizi mtupu!