Mrema na unaibu waziri mkuu

Mozila

Senior Member
Mar 23, 2012
174
47
Katiba ya sasa ya mwaka 1977 haimtambui naibu waziri mkuu,nani alimpa hicho cheo mrema?
 
Katiba ya sasa ya mwaka 1977 haimtambui naibu waziri mkuu,nani alimpa hicho cheo mrema?

We umezaliwa mwaka gani? Alipewa na Rais Mwinyi hilo hujui, halafu hicho cheo kinakuuma au? Tafuta mada ya maana acha wivu
 
Novemba 5th, 1985 hadi Septemba 19th, mwaka 1989.

Kaka, kuna wengine tumekuwa tukifuatilia siasa za Tanzania kabla ya 2006, "JamboForum" ilipoanza, basi niruhusu niendelee na darasa. J. Nyerere aliulizwa, kwa nini umeanzisha cheo ambacho hakipo kwenye Katiba, akajibu, Katiba haijasema awepo, wala haijakataza asiwepo.

Huu utata unakuja kwa sababu sisi hatuna "enumerated powers doctrine" kwenye mfumo wa Katiba yetu, kama baadhi ya nchi, ambapo, kama kitu kwenye Katiba hakijasemwa kwamba kiwepo maana yake kimekatazwa!

Niendelee ama nisiendelee?
 
Novemba 5th, 1985 hadi Septemba 19th, mwaka 1989.

Kaka, kuna wengine tumekuwa tukifuatilia siasa za Tanzania kabla ya 2006, "JamboForum" ilipoanza.

Mimi nimeuliza tu lini. Sikusema chochote kuhusu ufuatiliaji wa siasa za Tanzania kabla ya 2006, "JamboForum" ilipoanza. Licha ya hivyo, hongera kwa kufuatilia siasa za Tanzania kabla ya 2006.
 
Mimi nimeuliza tu lini. Sikusema chochote kuhusu ufuatiliaji wa siasa za Tanzania kabla ya 2006, "JamboForum" ilipoanza. Licha ya hivyo, hongera kwa kufuatilia siasa za Tanzania kabla ya 2006.
ahaa, okay, haya, nakubali yaishe!
 
ahaa, okay, haya, nakubali yaishe!
Hapana. Yasiishe. Wakati wa utawala wa Nyerere Salim alikuwa waziri mkuu kamili. Nimeangalia CV yake inaonyesha Salim alikuwa waziri wa ulinzi 1985-89 chini ya Mwinyi na wakati huo huo akiwa deputy prime minister. Kumbe cheo hicho alikianzisha Mwinyi na si Nyerere.
Alichaguliwa kuwa waziri mkuu baada ya kifo cha Sokoine.
 
Hapana. Yasiishe. Salim hajawahi kuwa naibu waziri mkuu. Alikuwa waziri mkuu kamili. Kama alikuwa naibu niambie ni nani aliyekuwa waziri mkuu wakati huo.
Jasusi, of all the people, sikujua kama na wewe kumbukumbu yako ya siasa/viongozi wetu ni kama hii ya kizazi cha dot.com ambao wameanza kufuatilia siasa siku ilipozinduliwa "JamboForums"! Kwanza kabisa kaka, ukiamua kubisha kitu huwezi ku turn around na kusema "kama alikuwepo"! Ushakataa kwamba hakuwepo! Basi mradi umesema yasiishe, ngoja niendelee kutoa darasa la historia ya nchi yetu kwa kizazi cha dot.com!

Naanza na hansard za Bunge, June 24, mwaka wa 2011, Mhe. A. Mrema, (TLP, Vunjo) ambae alikuwa analalamika bungeni kwamba hajapewa mafao yake ya Unaibu Waziri Mkuu .

Hansard, Bunge la Jamhuri: "Mheshimiwa Mwenyekiti...
ukiacha kazi utapewa asilimia 80 ya mafao yako ya mshahara wako, nipeni basi hata asilimia 20. Mnasema hiki cheo changu hakikuwa kwenye Katiba, Rais ndiye anaanzisha cheo. Hata Mawaziri wetu wanaanzishwa kwa decree ya Rais. Ilikuwaje cheo ambacho Mwalimu Nyerere alianzisha, akasimamia akakaa pale Dkt. Salum Ahmed Salum, Naibu Waziri Mkuu wa pili Agustino Lyatonga Mrema."

Sasa kwa nini hakusimama hata mbunge mmoja kutoa taarifa kwamba "Mrema unaongopea bunge, "wewe ndio ulikuwa Naibu Waziri Mkuu wa kwanza"? Hicho ni kidhibiti cha kwanza kwamba Mrema hakuwa wa kwanza.

Nina vidhibiti vingine ambavyo sio vya yeye mwenyewe Mrema, kama bado tunahitaji somo, lakini ka mnakubali yaishe semeni!

Endelea. Lakini Mrema was wrong. Na wabunge wetu si wote wanaozingatia facts. Fact: Salim aliteuliwa kuwa waziri mkuu baada ya kifo cha Sokoine 1984. Fact: Mwalimu alistaafu 1985 na nafasi yake kuchukuliwa na Mwinyi. Fact: Kwa sababu Mwinyi alikuwa Mzanzibari asingeweza kuendelea na Salim kama waziri mkuu wake ndipo alipomchagua Malecela. Fact: Salim alipewa nafasi ya Waziri wa ulinzi na naibu waziri mkuu, ikiwa mara ya kwanza kwa nafasi hiyo kuwepo katika safu ya uongozi Tanzania. Sasa hapo nani anasema kweli? Jasusi au Mrema? Endelea.
 
Jasusi,

..Salim Salim alikuwa waziri wa ulinzi, na naibu waziri mkuu, wakati wa awamu ya kwanza ya mzee mwinyi. kipindi hicho joseph warioba alikuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa raisi.

..agustino mrema alikuwa naibu wa waziri mkuu cygwiyemisi john malecela ambaye pia alikuwa makamu wa kwanza wa raisi. baada ya reshufle iliyomuondoa malecela kwenye uwaziri mkuu akaja cleopa msuya ambaye hakusaidiwa na naibu waziri mkuu.

NB:

..mrema aliteuliwa naibu waziri mkuu katikati ya kipindi cha uwaziri mkuu wa cygwiyemisi malecela. kulitokea malalamiko toka kwa mawaziri wenzake kwamba mrema anawaingilia ktk majukumu yao. sasa ili kuzima malalamiko hayo raisi mwinyi akaona amteue kuwa naibu waziri mkuu.
 
Kwa hiyo ni kweli ama si kweli kwamba unaibu waziri mkuu ulianza enzi za Nyerere kama bwana Bu'yaka anavyodai? Au na wewe ni mdotcom hivyo hujui....?
 
...Fact: Salim alipewa nafasi ya Waziri wa ulinzi na naibu waziri mkuu, ikiwa mara ya kwanza kwa nafasi hiyo kuwepo katika safu ya uongozi Tanzania.
Kwa hiyo umekubali?

Sasa ulikuwa unabisha nini Jasusi!

Haina shida.

Ngoja tuwasaidieni wale wa kizazi cha point-and-click (nyooshea-na-bonyeza) kuelewa historia yetu.

Hii ifuatayo ni kutoka tovuti ya Wizara ya Ulinzi. Nyooshea na bonyeza:

Kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1989

sallim.jpg

Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alikuwa Mhe. Salim Ahmed Salim. Mhe. Salim alihamishiwa Wizara hii mwaka 1985 na hivyo kuwa naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi. Dk. Salim aliondoka Wizara yetu baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika

Niendelee ama nisiendelee?
 
Dah! Embu ngoja niweke kweye data zangu nihifadhi hizi kumbukumbu kweli Jf ni darasa!
 
Kinacho nishangaza ni kwamba hicho cheo kilikuwepo miaka ya 80, ina maana mwinyi alikuwa na madaraka makubwa kuliko mkapa na kikwete ya kumchagua naibu pm?
 
Back
Top Bottom