Mrema na unaibu waziri mkuu

Kwa hiyo umekubali?

Sasa ulikuwa unabisha nini Jasusi!


Haina shida.

Ngoja tuwasaidieni wale wa kizazi cha point-and-click (nyooshea-na-bonyeza) kuelewa historia yetu.

Hii ifuatayo ni kutoka tovuti ya Wizara ya Ulinzi. Nyooshea na bonyeza:

Kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1989

sallim.jpg



Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alikuwa Mhe. Salim Ahmed Salim. Mhe. Salim alihamishiwa Wizara hii mwaka 1985 na hivyo kuwa naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi. Dk. Salim aliondoka Wizara yetu baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika

Niendelee ama nisiendelee?

Sasa kipindi hicho i mean 1985-1989 Rais alikuwa nani? usikimbilie kuita dot.com...blah blah...
 
Endelea. Lakini point is: Nyerere hakupanga cheo cha naibu waziri mkuu. Ni Mwinyi. Kwa hili Mrema amekosea.
 
Ili kukata mzizi wa fitna tunahitaji tarehe. Tarehe za lini Nyerere alistaafu, lini Mwinyi alianza kuwa rais, na lini Salim A. Salim alikuwa 'naibu waziri mkuu' kama inavyodaiwa hapa.
 
Ili kukata mzizi wa fitna tunahitaji tarehe. Tarehe za lini Nyerere alistaafu, lini Mwinyi alianza kuwa rais, na lini Salim A. Salim alikuwa 'naibu waziri mkuu' kama inavyodaiwa hapa.
Nyani,
Mbona hii kazi rahisi? Mwalimu alistaafu October 1985. Mengine utajazia mwenyewe.
 
Ni kweli Salim alipewa unaibu waziri mkuu wakati warioba akiwa waziri mkuu na mrema pia alipewa unaibu waziri mkuu ni baada ya kutokea malalmiko ya kuwa anaingilia kazi zisizo zake nafikiri wengi wanakumbuka malumbano kati yake na mama Mary Chipsi Chipungahelo lakini ukweli hiko cheo hakitambuliwi kikatiba ila tu kwa sababu tulikuwa na Rais aliyekuwa anaendesha mambo kiswahili ndio maana aliweka vyeo kama hivyo. Kuna kipindi Mwinyi alimteua waziri mtu ambaye alikuwa anamuingiza mpirani bure kipindi kile yupo ubaoni baada ya kelele nyingi ikabidi wamtoe kwa sababu za kimaadili sitamtaja mtu huyo.

Wakati Mrema ni waziri wa mambo ya ndani alikuwa anafanya mamaamuzi mengi kinyume na sheria hiyo ilisababisha apewe naibu waziri Jaji Mweisumo ili kuzuia serikali kuingia katika migogoro mengi ya kisheria.

Kitendo cha mrema kuendelea kudai mafao kwa cheo ambacho hakikuwa kinatambulika kisheria si tu ni cha unafiki bali pia kinathibitisha kilichofanya ajiuzulu ni kule kutolewa kwenye uwaziri wa mambo ya ndani ambako kulikuwa na loophole nyingi na pia kuona hakuna uwezekano wa yeye kugombea urais Kumbuka huyu mtu akiwa kigoma ndiye aliyesema atakayetoka CCM ni mwendawazimu pia akiwa waziri wa mambo ya ndani alimpigia debe mtu ambaye baada ya kushinda uchaguzi iligundulika sio raia halali.Kama kweli anajali taifa lake aachane na madai ambayo yatazidi kuwakamua walipa kodi wa tanzania.
 
Ni kweli Salim alipewa unaibu waziri mkuu wakati warioba akiwa waziri mkuu na mrema pia alipewa unaibu waziri mkuu ni baada ya kutokea malalmiko ya kuwa anaingilia kazi zisizo zake nafikiri wengi wanakumbuka malumbano kati yake na mama Mary Chipsi Chipungahelo lakini ukweli hiko cheo hakitambuliwi kikatiba ila tu kwa sababu tulikuwa na Rais aliyekuwa anaendesha mambo kiswahili ndio maana aliweka vyeo kama hivyo.Kuna kipindi Mwinyi alimteua waziri mtu ambaye alikuwa anamuing
https://www.jamiiforums.com/newreply.php?do=newreply&p=4348317
 
Katiba haimtabui naibu yeyote yule.
ujue viongozi hawakuanza leo ku-abuse katiba leo, na wakati wa Mzee Mwinyi kama mnakumbuka alikuwa na 'kautaratibu kake' ka kusikiliza matatizo ya wananchi pale Lumumba na mara nyingi tu ali-nullify maamuzi halali ya Mahakama!

Na tukumbuke kwa uvunjaji huu kuna wenzetu wanaweza wakawa wako jela leo au mifupa yao iko Mabwepande kwa masuala haya haya yasiyoeleweka. Huwa wao wanasema "usicheze na serikali wewe".
 
Ili kukata mzizi wa fitna tunahitaji tarehe. Tarehe za lini Nyerere alistaafu, lini Mwinyi alianza kuwa rais, na lini Salim A. Salim alikuwa 'naibu waziri mkuu' kama inavyodaiwa hapa.


Nyani Ngabu,

..hakuna haja ya kuwa too specific kuhusu masuala ya tarehe.

..Salim Salim aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Mzee Ali Mwinyi, which was late 1985.

..Kumbuka kuwa Salim Salim ndiyo alichukua nafasi ya Edward Sokoine ambaye alifariki akiwa waziri mkuu.

..Kipindi Salim akiwa waziri mkuu, Nyerere alikuwa Raisi, na Mwinyi alikuwa raisi wa ZNZ na makamu wa muungano.

..Mwinyi alilazimika kuteua waziri mkuu toka bara baada ya kuchukua madaraka toka kwa Mwalimu Nyerere. Katiba ilikuwa inaelekeza kwamba ikiwa Raisi atatoka ZNZ basi waziri mkuu atatokea Tanganyika na ndiye atakayekuwa makamu wa kwanza wa raisi wa muungano.

..katika mazingira hayo, Joseph Warioba, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa raisi. Salim Salim aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu na waziri wa ulinzi.

NB:

..Mzee Mwinyi alikuwa na mawaziri wakuu na makamu wa kwanza wa raisi wafuatao: Joseph Warioba, Cygwiyemisi John Malecela, na Cleopa Msuya.

..katika kipindi hicho Maraisi wa Zanzibar na makamu wa pili wa Raisi walikuwa ni, Sheikh Idiris Abdul Wakil, na Dr.Salmin Amour.
 
Nyani Ngabu,

..hakuna haja ya kuwa too specific kuhusu masuala ya tarehe.

..Salim Salim aliteuliwa kuwa naibu waziri mkuu wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Mzee Ali Mwinyi, which was late 1985.

Kwa hiyo Bu'yaka anatudanganya anaposema kwamba hicho cheo cha unaibu waziri mkuu kilianza enzi za Nyerere?
 
Kwa hiyo Bu'yaka anatudanganya anaposema kwamba hicho cheo cha unaibu waziri mkuu kilianza enzi za Nyerere?

Nyani Ngabu,

..I wouldnt say that.

..inasemekana kuwa Nyerere ndiyo alishinikiza Warioba ateuliwe. alipoambiwa Warioba hana uzoefu aka-suggest Salim Salim awe naibu waziri mkuu. kwa msingi huo Bu'yaka is slightly correct.
 
Nyani Ngabu,

..I wouldnt say that.

..inasemekana kuwa Nyerere ndiyo alishinikiza Warioba ateuliwe. alipoambiwa Warioba hana uzoefu aka-suggest Salim Salim awe naibu waziri mkuu. kwa msingi huo Bu'yaka is slightly correct.

Hayo ya kusemekana huwa ni mengi sana na mara nyingi hayana ushahidi. Tuongelee yanayojulikana na yenye ushahidi.

Kama wakati Nyerere akiwa bado rais hakukuwa na naibu waziri mkuu hata mmoja basi hicho cheo hakikuanza chini ya utawala wake. Kwa msingi huu Bu'yaka (aka.....) anatudanganya.
 
Ngoja na mimi nipindishe hii mada kidogo lakini niko hukohuko kwenye histori ya nchi yetu Tanzania! Naomba kuuliza hivi hiki cheo alichowahi kupewa marehemu Mfaume Rashidi Kawawa waziri asiyekua na wizara maalumu kwenye katiba hii tuliyonayo hiki cheo kipo au ilikua ni kaupendeleo fulani kutoka kwa marehemu JK nyerere??

Both Rest In Peace Amen! Samahani kama nimetibua lakini yote nikutaka kuelewa japokua mimi sio kizazi cha Dot.Com!

Bu'yaka: naomba uendelee!
 
Bu'yaka kadanganywa na Mrema naye anataka atudanganye kama anavyotuita dotcom!
Nyerere alikuwa anawananga viongozi wanaoionea haya katiba kwenye moja ya hotuba zake,kumbe na mwenyewe alikuwa anaionea haya kama alishinikiza Salim apewe unaibu waziri mkuu?
 
Nyani Ngabu,

..I wouldnt say that.

..inasemekana kuwa Nyerere ndiyo alishinikiza Warioba ateuliwe. alipoambiwa Warioba hana uzoefu aka-suggest Salim Salim awe naibu waziri mkuu. kwa msingi huo Bu'yaka is slightly correct.
jokaKuu,
Nyerere hakushinikiza Warioba achaguliwe kuwa waziri mkuu. Salim Ahmed Salim ndiye aliyeshinikiza. Kuna wakati tulikuwa naye NY halafu ghafla akaondoka kurudi Bongo.

Nikawauliza Wazanzibari walio karibu naye mbona kaondoka haraka, mmoja akaniambia amesikia kuwa Mkapa ndiye chaguo la Mwinyi kuwa waziri mkuu na anaenda kumshauri Mwinyi aachane na Mkapa na hence Warioba akachaguliwa kuwa waziri mkuu.

Sasa unaweza kuelewa kwa nini Mkapa naye alilipiza kisasi Salim asiwe rais wa Tanzania. Na Nyerere pia hakushauri Salim awe naibu waziri mkuu. Huo ulikuwa uamuzi wa Mwinyi peke yake. Mrema is wrong.
 
Back
Top Bottom